Manchester United, Arsenal walizwa zaidi
Manchester United wameathiriwa zaidi na majeruhi katika msimu unaoelekea ukingoni wa 2014/15 wakifuatiwa na Arsenal.
United waliokuwa kwenye hali ngumu chini ya Louis van Gaal aliyepokea kazi kutoka kwa David Moyes alianza kwa shida, akishindwa kuweka kikosi sawa na mbaya zaidi akiathiriwa na wachezaji muhimu kuumia.
Wachezaji wa Mashetani Wekundu, hadi Aprili 29 mwaka huu walikuwa wamepata jumla ya majeraha 68, yakiwa ni pamoja na manne kwa nyota wao, Robin van Persie.
Je, hii ndiyo sababu Man U wamekuwa mbali hivyo nyuma ya Chelsea katika mbio za ubingwa? Labda, lakini bila shaka hawakujipanga vizuri pia tangu mwanzo.
Licha ya majeraha hayo, United hawakuwa na ukuta wala mfumo wa kueleweka, hasa katika nusu ya kwanza ya msimu.
Nani wameumia zaidi msimu huu?
Klabu | Majeraha |
Manchester United | 68 |
Arsenal | 66 |
Stoke City | 66 |
Newcastle United | 64 |
Everton | 62 |
West Ham United | 61 |
Liverpool | 52 |
Aston Villa | 51 |
Manchester City | 51 |
Queens Park Rangers | 49 |
West Bromwich Albion | 49 |
Hull City | 48 |
Crystal Palace | 45 |
Chelsea | 43 |
Sunderland | 42 |
Southampton | 38 |
Tottenham Hotspur | 38 |
Swansea City | 31 |
Leicester City | 29 |
Burnley | 24 |
Walioathirika zaidi kwenye klabu hii ni akina nani?
Mchezaji | Majeraha |
Luke Shaw | 6 |
Angel di Maria | 5 |
Robin van Persie | 4 |
Ander Herrera | 4 |
Chris Smalling | 4 |
James Wilson | 4 |
Ashley Young | 4 |
Phil Jones | 4 |
Marcos Rojo | 4 |
Michael Carrick | 3 |
Rafael | 3 |
Wayne Rooney | 3 |
Daley Blind | 3 |
David de Gea | 2 |
Marouane Fellaini | 2 |
Jonny Evans | 2 |
Antonio Valencia | 2 |
Radamel Falcao | 2 |
Adnan Januzaj | 1 |
Victor Valdes | 1 |
Tom Thorpe | 1 |
Juan Mata | 1 |
Luke Shaw alianzia mguu mbaya msimu huu hapo Old Trafford na Kocha Louis Van Gaal alijiaminisha kwamba licha ya majeraha, hakuwa kwenye kiwango kinachotakiwa tangu alipowasili akitoka Southampton msimu uliopita.
Alipata majeraha sita tofauti, ikizingatiwa kiasi kikubwa cha fedha kilichomnunua, na yakaja tena kumkuta Angel Di Maria aliyevunja rekodi ya usajili kwa England yote (pauni milioni 59.7).
Wapo pia wachezaji wengine waandamizi wa United waliokabiliwa na msimu mbaya kwa kuumia, nao ni Ander Herrera, Marcos Rojo, Ashley Young na Chris Smalling, wote wakiwa na majeraha manne tofauti kwa kila mmoja na nahodha Wayne Rooney matatu.
CHELSEA TIMAMU WA MWILI ZAIDI
Tofauti na United, Chelsea waliopaa na kuwaacha wengine mbali kwenye msimamo wa ligi, ndio walikuwa na kikosi chenye wachezaji timamu zaidi wa mwili kuliko klabu nyingine zilizoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wachezaji wa Chelsea wameshapata majeraha 43 tu msimu huu na wapo katika orodha ya timu saba zilizopata majeruhi wachache zaidi.
Idadi inaweza kuonekana ni haki kuwa nao lakini ukizingatia jinsi kocha Jose Mourinho anavyochezesha sana wachezaji wale wale, basi wachezaji wake wana utimamu mzuri wa mwili.
Kwa mfano, Eden Hazard, amecheza mechi zote kwa dakika 90 tangu mwishoni mwa Oktoba mwaka jana na kuumizwa kidogo mara tatu.
Ajabu pia ni kwamba, inaelezwa ndiye anayewindwa kuumizwa zaidi na wachezaji wa timu pinzani. Ameangushwa mara 100 na ndiye ameibuka kuwa mchezaji bora aliyechaguliwa na Chama cha Wanasoka wa Kulipwa (PFA).
Hali hii haimaanishi kwamba Chelsea hawakuwa na matatizo ya wachezaji wake kuumia na kuwa na wasiwasi iwapo wangefanya vyema, maana mshambuliaji wao mahiri Diego Costa amekuwa nje kwa maumivu vipindi saba tofauti, akiwa na shida kubwa ya nyama za paja.
Costa ni wa tatu katika ligi kwa matatizo ya majeraha, wa kwanza akiwa ni mchezaji wa Crystal Palace,’ Joe Ledley na yule wa Stoke, Jon Walters.
Hata hivyo, kuwa nje huko hakujamzuia Mhispaniola huyu aliyezaliwa Brazil kuongoza kwa mabao 19 ya kufunga hadi sasa. Angekuwa timamu muda wote ingekuwaje?
Wachezaji walioumia zaidi EPM msimu huu
Mchezaji | Majeraha |
Joe Ledley | 8 |
Jon Walters | 8 |
Daryl Janmaat | 7 |
Diego Costa | 7 |
James Tomkins | 7 |
Steven Fletcher | 7 |
Alex Oxlade-Chamberlain | 6 |
Andrew Robertson | 6 |
Danny Welbeck | 6 |
Diafra Sakho | 6 |