10: AGYEI na DIDA.
Inawezekena Agyei akawa ingizo sahihi katika kikosi cha Simba katika
round hii ya pili ya ligi kuu Tanzania bara, amekuwa mtu ambaye ni
muhimu sana katika kikosi cha Simba, pamoja na utulivu alionao langoni
lakini pia ni mzuri wa kupanga mabeki, wanatofautiana kitu kimoja tu
na Dida, Dida pamoja na uzoefu alionao ila amekuwa mtu ambaye
anapenda kutema tema mipira.
9: Lwandamina na Omong.
Tofauti kubwa waliyonayo kati ya hawa watu ni kwamba, mmoja wao ana
kikosi muda mrefu kuzidi mwenzake.
Mara nyingi Yanga imekuwa ikitumia upande wa pembeni katika
kutengeneza nafasi za magoli, hii imekuwa ina madhara kwa kiasi
kikubwa sana pindi timu inapobanwa pembeni kwa sababu ubora wa Yanga
upo pembeni, kitu cha muhimu ni kwa Lwandamina kuifanya timu iwe
inatengeneza nafasi nyingi za magoli katika Sehemu mbalimbali mwa
uwanja.
Hii ni tofauti kubwa sana kwa Simba, Simba imekuwa bora zaidi katika
eneo la kiungo wa kati, wachezaji ambao wanacheza katika eneo hili
wamekuwa wakihusika kwa kiasi kikubwa sana katika utengenezaji na
ufungaji wa magoli, pia wamekuwa msaada mkubwa sana Kumchezesha
Kichuya.
8: Nani mtu sahihi kucheza na Kelvin kati ya Bossou na Nadir?
Kelvin hana sifa kubwa ya kuwa kiongozi na ni ngumu Kwake yeye kucheza
na beki ambaye anahitaji kuongozwa kama Dante.
Nafasi kubwa ya Kelvin kuwepo katika mchezo huu ni mkubwa kwa sababu
ya work rate kubwa aliyonayo. Sasa ni mchezaji yupi sahihi wa kucheza
naye leo?
Kwa upande wangu Vincent Bossou ni mtu sahihi, kwa sababu ni mtulivu
zaidi ya Nadir, hachezi rafu sana kama Nadir, pia ni mzuri wa Ku
Clear makosa ya beki mwenzake, ukiachana sifa ya Vincent kuwa
kiongozi kama Nadir alivyo, pia Vincent ni mzuri kwa mipira ya juu
pamoja na matumizi ya nguvu pindi yanapohitajika.
7: Mwanjali na Lufunga?
Wote pamoja ni mabeki ambao ni malibero, kwa kiasi fulani huwa ni
ngumu kwa timu kuchezesha Mabeki ambao ni libero kwa pamoja, lakini
kwa hivi karibuni Lufunga amekuwa akijivua baadhi ya majukumu ya
libero na kumwachia Mwanjali kwa kiasi kikubwa, na hiki ndicho kitu
ambacho anatakiwa akifanye siku ya leo.
6: Ndemla.
Tangia aingie amekuwa na faida kubwa sana kwenye kikosi cha Simba kwa
sababu amefanikiwa kuleta balance nzuri katika eneo la ushambuliaji la
timu ya Simba. Amekuwa akitengeneza nafasi nyingi sana za magoli
pamoja na kufunga.
5: Nani mtu sahihi kati ya Zullu na Said Juma Makapu?
Kwa upande wangu Zullu ni mtu sahihi katika mechi ya leo kwa sababu,
Pamoja na kwamba Zullu amekuwa ni mchezaji mzuri katika majukumu ya
kukaba pia anapiga pasi vizuri tofauti na Makapu ambaye mara nyingi
hupiga square passes nyingi.
4: Kotei na Mkude?
Kati ya vitu ambavyo Simba wanatakiwa kufanya kwa kiasi kikubwa ni wao
kuwaanzisha Mzamiru na Ndemla katika eneo la kati kwa sababu Mzamiru
ni box to box Middfielder ambaye analeta balance ya kukaba na
kushambulia.Ndemla ni mzuri sana kutengeneza nafasi za magoli pamoja
na kufunga magoli.
Sasa kiungo gani wa eneo la kuzuia anauwezo wa kucheza na Mzamiru na Ndemla?
Kwa upande wangu Mkude ni mtu sahihi katika mechi ya leo, kwa sababu
ni mzuri kwenye kukaba na kuanzisha mashambulizi.
3: Tambwe acheze peke yake kwenye hii mechi?
Kati ya vitu ambavyo Yanga watakosea sana ni kumwanzisha Tambwe peke
yake kwa sababu Yanga mara nyingi hutumia Wingers kutafuta magoli, na
timu inapotumia Wingers kutafuta magoli inahitaji vitu viwili, cha
kwanza ni mshambuliaji anaayejua kucheza mipira ya juu, cha pili ni
kuwa na washambuliaji wa kati wawili ambao wanakuwa na uwezo wa
kucheza mipira ya juu, pia kuwa na washambuliaji wawili wa kati
unaipa timu uwezo wa kuwa na watu wengi wa kuitumia mipira inayokuja
eneo la box la timu pinzani. Hivyo Uwepo wa Chirwa na Tambwe kwa
pamoja itakuwa na faida kubwa sana kwa upande wa Yanga.
2: Kuwatumia Mavugo, Luzio na Ajib kwa pamoja kutakuwa na faida kubwa
kwa upande wa Simba?
Nionavyo mimi hawa watu tangia wacheze pamoja katika mechi tatu
zilizopita wamekuwa na Ushirikiano mzuri sana kitu ambacho kimeisaidia
Simba kupata magoli mengi katika mechi tatu zilizopita (magoli 7).
Na kuwaanzisha wote kwa pamoja kunaipa nafasi Simba kuwa na uhakika wa
kupata magoli muda wote.
1: Msuva ndo injini ya Yanga?
Hili halina ubishi kuwa Msuva ndiye mchezaji muhimu sana katika kikosi
cha Yanga. Upande wake wa kulia ambao anacheza na Juma Abdul umekuwa
ni upande ambao mashambulizi mengi ya Yanga yalitokea. Simba
Wakifanikiwa kuziba upande huu watakuwa wamefanikiwa kuziba asilimia
kubwa ya mashambulizi ya Yanga.