in , , , ,

Liverpool wawaadabisha Swansea

*Chelsea, Man U huenda wakakutana FA

Liverpool wamewafanyia Swansea mauaji ya mabao 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Wakicheza nyumbani, Liverpool waliougulia vipigo viwili mechi zilizopita, waliwaadabisha Swansea wanaocheza fainali Wembley katika Kombe la Ligi dhidi ya Bradford wikiendi ijayo.

Kocha Michael Laudrup alimpumzisha mfungaji matata, Michu na wachezaji wengine sita muhimu, akaambulia kuadhibiwa na vijana wa Brendan Rodgers.

Liverpool walitawala kila idara, huku wakipiga mashuti zaidi ya 35 langoni, ikiwa ni mechi ya kwanza kuwashinda waliokuwa juu yao kwenye msimamo wa ligi.

Kwa ushindi huo Liverpool wamefikisha pointi 39 na kushika nafasi ya saba, wakiwaacha Swansea na pointi 37 nyuma yao, lakini wote wamecheza mechi moja kuliko timu nyingine 18.

Liverpool walipata mabao yao kupitia nahodha Steven Gerrard kwa penati, Philippe Coutinho, Jose Enrique, Luis Suarez na Daniel Sturridge kwa penati.

Swansea walikuwa wakifundishwa na Rodgers katika msimu uliopita, lakini katika mechi ya awali walimwadhiri mwalimu wao huyo kwa kuwafunga Liverpool.

Katika Kombe la FA, Chelsea huenda wakakutana na Manchester United kwenye nusu fainali, ikiwa timu hizo mbili zitafuzu kwenye mechi za raundi ya tano.

Ili kufika huko, Chelsea waliowakung’uta Brentford mabao 4-0 Jumapili hii, wanatakiwa kuwafunga Middlesbrough Februari 27.

Ushindi huo utawakutanisha na ama Manchester United au Reading wanaokipiga Jumatatu hii. Everton Jumamosi walinyang’anywa tonge mdomoni na Oldham waliosawazisha bao dakika za majeruhi, hivyo watarudiana.

Mshindi kati yao atakabiliana na Wigan Athletic waliocharuka Jumapili hii pia na kuwafunga Huddersfield mabao 4-1 na kujifariji kwa vile katika EPL wapo eneo la kushuka daraja.

Mabingwa wa England, Manchester City ambao walicharuka Jumapili ii pia na kuwachapa Leeds United mabao 4-0 watawakaribisha Barnsley dimbani Etihad.

Ratiba nyingine inaonesha kwamba Millwall watakipiga na Blackburn Rovers waliowaaibisha Arsenal kwa bao 1-0 Jumamosi hii uwanjani Emirates.

 

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Tenga atoa somo kwa waliochujwa kufuata taratibu…

KAMATI YA MTIGINJOLA YATUPA MAOMBI YA ‘REVIEW’