in , ,

Leicester: Tunataka wachapa kazi

Mabingwa wa England, Leicester City wamesema mpango wao kwa msimu ujao
ni kusajili wachezaji wanaochapa kazi na wanaojua kile wanachotakiwa
kufanya na mpira, si kuchukua majina makubwa.

Mkuu wa usajili katika klabu waliotwaa ubingwa mara ya kwanza majuzi
katika historia yao ya miaka 132, Steve Walsh, amesema kwamba mchezaji
hatasajiliwa kwa sababu tu anajulikana kuwa na uwezo, bali mtazamo
wake.

“Suala hapa ni kuhakikisha kwamba wachezaji tunaowaleta wana mwelekeo
tunaoutaka hapa, wanamudu kutekeleza majukumu tunayowapa wakati wote,
tuwe na umiliki au pasipo na umiliki wa mpira dimbani,” anasema.

Walsh ambaye pia ni mmoja wa makocha wasaidizi wa Claudio Ranieri,
alisaini mkataba mpya Jumapili hii na anasifiwa kwa kazi aliyofanya ya
kufanikiwa kusajili wachezaji wazuri kama Riyad Mahrez kutoka klabu ya
daraja la pili nchini Ufaransa, Le Harve, kwa £400,000 Januari, 2014.

Kikosi cha Leicester kilichotwaa ubingwa kimekusanywa kwa pauni
milioni 57, kiasi ambacho klabu nyingine ziliweza kusajili mchezaji
mmoja. Hiki ndicho kikosi rahisi zaidi kuliko cha klabu zote zilizo
katika nusu ya kwanza ya jedwali la msimamo wa ligi kuu hapa.

“Ingekuwa unataka kupata wachezaji wote wazuri zaidi tu, basi ingekuwa
rahisi kutumia wang’amua vipaji au sio? Lazima uangalie wachezaji hao
kwa macho tofauti na kuona unaweza kupata nini.

“Tunacho kinasaba. Kwangu si suala la uwezo wa mchezaji kwenye boli,
isipokuwa ni wamejiandaa na wana uwezo gani wa kusaidia timu wakati
hatuna mpira huo. Ni kwa sababu hiyo lazima kuangalia tabia ya
mchezaji; ikiwa mmoja anajiandaa kufanya kazi kubwa wakati hatunao
mpira, ni wazi kwamba anatufaa.

“Watu wanadhani tunacheza wawili kwenye kiungo, mie nawaambia;
‘hapana, tunacheza na Danny Drinkwater katikati na N’Golo upande wa
pili, na hii hutufanya tuwe kama tuna wachezaji 12 dimbani,” anasema.

Kante alikuwa akicheza ligi Caen, Ufaransa na alisajiliwa kwa pauni
milioni 5.6 tu. Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex
Ferguson amemtaka Kante kuwa mmoja wa viungo wazuri zaidi msimu huu
katika EPL, kutokana na kipawa chake cha kuutafuta na kuumiliki mpira
pamoja na kasi kwenye mashambulizi ya kushitukiza iliyosaidia ubingwa
kwenda King Power Stadium.

Kiungo huyo aliwasili muda mfupi baada ya kuteuliwa kwa Ranieri kuwa
kocha. Walsh anaeleza kwamba walibishana na Ranieri juu ya Kante,
lakini hatimaye wakakubaliana kumsajili na ameonesha uwezo wake
mkubwa.

Walsh, mwalimu wa zamani aliyezaliwa Lancashire na ambaye ndiye
alimng’amua Jose Mourinho, amekuwa na Leicester kwa nyakati mbili
tofauti tangu 2008, ambapo kilele cha mafanikio kimekuwa kutengeneza
kikosi kilichokuja kutwaa ubingwa, akianza nacho mwanzo hadi mwisho.

“Sven Goran Eriksson alimleta Kasper Schmeichel 2011, lakini licha ya
yeye na wale waliopanda kutoka kwenye kikosi cha akademia yetu kama
Andy King na Jeff Schlupp, tulifanya ung’amuzi pia.

“Christian Fuchs, yule beki wa kushoto tuliyempata bure kutoka
Schalke, alifunga dhidi ya Real Madrid kwenye michuano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya kule Bernabeu mwaka jana. Ni nahodha wa Austria,
alitaka kuja na kweli amefanya kazi kubwa,” anasema.

Walsh alimfuata kocha Nigel Pearson Leicester 2008 wakafanya naye
kazi kisha Hull 2010 halafu akarudi King Power Stadium mwaka mmoja
tena baadaye. Pearson na Walsh walifanya kazi pamoja kwa miaka tisa.
Pearson aliondoka, na Walsh akabaki na Ranieri hadi wakatwaa ubingwa.

Anasema walisikitika kufukuzwakazi kwa Person mwisho wa msimu
uliopitaa ambapo walinusurika kushuka daraja na ujio wa Ranieri bado
haukuwa umewaangazia kwamba ungekuwa na kubwa kwao, hivyo matarajio
yalikuwa haba.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Bayern waanza usajili

Tanzania Sports

Man United hoi