Menu
in , , , ,

KUTETEMA KWA MAYELE KUMEISHA?

Tanzania Sports

Msimu mmoja ulipouita mchezaji mkubwa na maarufu katika ligi kuu ya soka Tanzania bara alikuwa mshambuliaji wa kutoka nchi ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo bwana Fiston Kalala Mayele. Mshambuliaji huyo alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na umahiri mkubwa ambao aliokuwa nao wa kufunga magoli. Mashabiki wengi wa soka walitokea kuvutiwa na staili yake ya ushangiliaji mabao ambayo ilipewa jina la kutetema. Kila alipofunga goli alishangilia kwa staili yake hiyo na alikuwa anashangiliwa kwa wingi sana na mashabiki wa timu yake.

Mayele alisajiliwa na klabu ya Yanga kutoka klabu ya soka toka jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo inayojulikana kama As Vita. Mechi yake ya kwanza ilikuwa ni kombe la ngao ya hisani ambapo alicheza dhidi ya klabu ya Simba ambapo katika mechi hiyo alicheza kwa umahiri mkubwa na alifanikiwa kushinda goli moja na hivyo kuanza kutangaza jina lake nchini Tanzania. Umahiri wake wa kufunga mabao ulimfanya kuwa na mashabiki wengi sana.

Staili yake kushangilia iligeuka kuwa ni gumzo sana ambapo staili yake hiyo alikuwa anatetemeka kama roboti ambapo mashabiki wake wakaiita “kutetema”. Kutetema ikageuka kama ndio staili ya kushangilia mashabiki wa soka nchini Tanzania ambapo kila lilipokuwa linafungwa goli basi mashabiki nao halikadhalika wakawa wanatetema. Staili hiyo alienda nayo hadi kwenye timu yake ya taifa ya Congo ambapo kila alipofunga goli nako alitetema halikadhalika. Mwanzoni wakati anaingia Yanga katika msimu wake wa kwanza alitengeneza  ushirikiano mzuri na mchezaji wa kimataifa toka Burundi bwana Saido Ntibazonkinza ambapo wawili hao walikuwa ni mwiba kwa timu pinzani na halikadhalika alikuwa anapata assisti pia kutoka kwa Feisal Salum ‘’Fei Toto”. 

Msimu wake wa kwanza alikuwa anapambania kiatu ch mfungaji bora dhidi ya aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Geita Gold wakati huo George Mpole. Ushindani wao wa ufungaji bora kwa kiasi Fulani ulichangamsha ligi kwani watu wengi walikuwa wanaufuatilia kwa hamu kubwa sana. Mashabiki wa klabu ya Simba nao walikuwa wanashangilia Zaidi pindi George Mpole alipokuwa anaongeza idadi ya magoli kwani hawakupenda Mayele awe mfungaji bora wa msimu. Mayele alisaidia klabu yake kubeba ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara katika msimu huo.

Msimu wake wa pili klabu ya Yanga iliachana na Ntibazonkinza ambaye aliachwa kama mchezaji huru na ndipo mchezaji huyo akasaidini kutumikia klabu ya Geita Gold ya huko mkoani Geita. Katika msimu huo Ntibanzonkinza alifanikiwa kufunga idadi ya magoli mengi katika mzunguko wa kwanza wa ligi na katika mzunguko wa pili alihamia klabu ya Simba na wakati akiwa hapo Simba akafanikiwa kufunga magoli  mengi Zaidi na hivyo kumfanya kuwa ndio mfungaji bora wa msimu akiwa amelingana idadi ya magoli na Fiston Kalala mayele. katika msimu huu walilingana idadi ya magoli ambayo yalikuwa ni 17.

  msimu huo wa 2022/2023 halikadhalika jina lake lilizidi kung’ara nchini tanzania kwani kila alipokuwa anapita alikuwa anaimbwa yeye na ilifikia hatua hadi ya kupewa zawadi mfano alipewa ng’ombe na mashabiki wa kanda ya ziwa na pia alipewa ng’ombe na mashabiki wa turiani mkoani Morogoro.  msimu huo halikadhalika aling’ara kwenye mashindano ya kimataifa ambapo alifanikiwa kufunga idadi ya magoli 7 katika kombe la shirikisho la vilabu barani Afrika na kuwa mfungaji bora katika mashindano hayo. msimu ulipoisha Mayele akawa ndie gumzo barani Afrika ambapo vilabu kadhaa vilikuwa vinamtaka ikiwemo Kaizer Chiefs na vinginevyo. katika kinyang’anyiro hicho klabu ya Fc Pyramids ndio iliofanikiwa kumpata na kumsajili kwa gharama za fedha ambazo zilizidi kiasi cha pesa za shilingi za Tanzania milioni 600.

washabiki wengi wa soka walikuwa na matumaini kwamba atawika sana ndani ya kikosi cha Pyramids FC lakini hali imekuwa ni tofauti kwani hajawa na makali ambayo alikuwa nayo Yanga na inaonyesha hali yake ya kujiamini imeanza kupungua kwani alikuwa matamshi kupitia mitandao ya kijamii kuwashutumu wazee wa Yanga kwamba wanamroga na kumfanya asicheze vizuri huko nchini Misri.

Mpaka Mei 16 mwaka huu alikuwa amehusika kwenye jumla ya magoli 10 ambapo alifanikiwa kufunga magoli 8 na kutoa pasi 2 za mabao na hiyo ni katika ligi kuu ya Misri. katika michuano ya klabu bingwa ya soka barani Afrika amefanikiwa kufunga magoli 2 na kutoa assisti 1 ndani ya jumla ya mechi 7 alizocheza.  kiuwiano inaonekana kama kiwango chake kimepungua. na swali wanalojiuliza mashabiki wa soka je ni je kutetema kwa Mayele kumeisha?

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version