KWA mara nyingine tena klabu ya Azam imeshindwa kufurukuta katika mashindano ya kimataifa baada ya kukosa bao moja tu la kuwavusha katika hatua nyingine na kupoteza nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa hatua inayofuata. Licha ya kupata ushindi wa mabao 2-1 ndani ya dakika 90, lakini ni Bahir Dar Kanema ya Ethiopia ndiyo iliyofuzu kwa hatua ya pili baada ya kuibuka na ushindi wa matuta 4-3 dhidi ya Azam.

Katika mchezo wa kwanza Azam walifungwa mabao 2-1. TANZANIASPORTS inafahamu kuwa kwa matokeo ya Azam imerudia makosa ya msimu uliopita ambako licha ya kushinda mabao 2-0, hayakutosha kuivusha timu hiyo kwani mchezo wa kwanza ilifungwa mabao 3-0. Katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Azam Complex kuna masuala kadhaa yamejitokeza na kuibua maswali juu ya mustakabali wa klabu hiyo kwenye mashindano ya kimataifa.

KURUDIA MAKOSA

Tanzania Sports

Msimu uliopita 2022/2023 Azam walikwenda nchini Libya kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho. Katika mchezo wa kwanza dhidi ya wenyeji wao Al Akhadar wakiwa na kocha wao Julien Chavalier waliichapa Azam mabao 3-0. Mchezo wa marudiano ulifanyika jijini Dar es salaam ambako Azam waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Azam walihiaji mabao manne ili kuitupa nje klabu ya Al Akhadar. Lakini ishindwa hata kusawazisha kwa kuongoza bao tatu ili matokeo yangesoma 3-3 na mchezo ungeongezwa muda. Filimbi ya mwisho ilipopulizwa Azam hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kukubali matokeo. Msimu wa 2023/2024, Azam wametolewa kwa mtindo uleule. Katika mchezo wa kwanza walifungwa mabao 2-1, huku matarajio yakiwekwa kwenye mchezo wa marudiano lakini wakaishia kuambulia 3-3. Namna wageni walivyopata bao na kuinua matumaini yao kuwa 2-1 inashangaza. 

KUZUBAA NA KURIDHIKA

Kosa kubwa walilofanya wachezaji wake ni kudhani mchi iliisha baada ya wao kupata bao la pili. Azam walipata mabao yake ndani ya dakika 30 na kuwafanya wadhani kutakuwa na karamu ya mabao. Wachezaji wa Azam walionekana kuzubaa mara kwa mara, kupoteza pasi au kutofika kwa walengwa. Ilifika wakati wachezaji wa Azam walikuwa wanapoteana eneo la kiungo. Kwa mfano wageni walipata bao baada ya safu ya kiungo kujazana bila mpangilio ndani ya eneo la 18, badala ya kukaba wapinzani, wao wakataka kuziba nafasi wakiwa wameshachelewa. Mchezaji wa Kanema aliona makosa ya ulinzi hivyo kupenyeza pasi kwa mshambuliaji wao.

Kuzubaa kwa wachezaji huenda kunatokana na uzoefu mdogo kuhusu mashindano ya kimataifa, lakini ukiangalia sifa za wachezaji wenyewe unaona wazi wanatakiwa kuonesha thamani ya ugeni wao. 

YOUSPH DABO ANA WALAKINI

Azam inavyo vipaji lakini ilikuwa timu inayocheza haina mpangilio. Katika dakika 45 za kwanza Azam hawakuweza kupigiana pasi wenyewe kwa wenyewe angalau 10 mfululizo. Kukosa uwezo wa kutuliza mpira na kutawala mchezo kulisababisha timu ionekane nzito, kiasi kwamba hapakuwa na kasi, mpangilio wa mashambulizi au kuonesha kuwa ni timu inayofundishwa ikapangika na kupanga mambo yake. Kocha wa Azam Yousoph Dabo anacho kibarua cha kuthibitisha kwanini amepewa kazi ya kuinoa timu hiyo. Anatakiwa kuonesha ubora kwa kuifanya Azam icheze kimbinu na mpangilio uanaoeleweka. Lakini hali ya sawa Azam wanacheza cheza tu, hakuna umahiri wa kiufundi kwa timu mzima.  

Kwa upande mwingine Yousoph Dabo anamchezesha Feisal Salum namba 10 kwa namna anavyocheza inamfanya awe mzigo kwa timu, kiasi kwamba alikuwa anazidiwa kwa kukimbia uwanjani na Prince Dube. Hii ina maana Feisal hakuwa kwenye kasi sawa na Dube, hivyo kuleta hoja kwamba afadhali angepangwa namba 8.

AZAM MBELE YA YANGA, SIMBA

Unapowatazama Azam wakicheza dhidi ya klabu kongwe za Simba au Yanga unaona wazi wanacheza kwa nguvu na kukamia mechi hizo. Mechi zao dhidi ya Yanga na Simba zinakuwa za kusisimua,kukamiana na shughuli pevu. Lakini linapofika suala la mashindano ya kimataifa mambo yanabadilika. Azam inakuwa timu isiyodhaminika wala kutegemewa kuwa inaweza kupindua meza. Namna Azam wanavyofungwa mabao kimataifa au hata Ligi Kuu Tanzania kuna mambo yanazua maswali.  Mpira wanaocheza Azam wanapokutana na timu za Simba na Yanga ni tofauti na kile wanachokifanya kwenye mashindano ya kimataifa.

PRINCE DUBE ATACHOKA

Ligi kuu Tanzania inao washambuliaji wengi, lakini Prince Dube ni mmoja wachezaji wanaosisimua anapocheza. Ni mshambuliaji ambaye kocha anafaidika kwa maarifa na muono wa mbali,kasi,mashuti, vichwa,kujituma. Kama mshambuliaji wa Azam Prince Dube angekuwa anachezea klabu za Yanga au Simba, bila shaka msimu mzima angekuwa anafunga zaidi ya mabao 25. Prince Dube ni aina ya mshambuliaji ambaye anakupa maarifa mengi, anakaba, anashambulia, anafunga mabao magumu, anapambana na ,mabeki. Lakini Prince Dube yuko kwenye timu ambayo inashindwa kumpa anachotaka. Mwishowe naye atachoka.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Mbappe

Vita kali PSG na Real Madrid

Tanzania Sports

Watanashati Yanga kuwavimbia El Marreikh?