in , , ,

KUFUZU KOMBE LA MATAIFA AFRIKA


Kongo wawachinja Nigeria
*Uganda wawabana Ghana, Cameroon safi
*Cape Verde waanza tena kuchanua vizuri

Mabingwa wa Soka wa Afrika, Nigeria wameangukia pua, baada ya kukubali kichapo kutoka kwa Kongo Brazzville kwenye mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kongo walisimama imara kwenye mechi iliyopigwa mjini Calabar na kuibuka na ushindi wa 3-2, na kuweka rekodi mpya mbaya kwa Nigeria.

Hii ni mara ya kwanza katika miaka 33 Nigeria wanapoteza mechi ya kiushindani
The Super Eagles walianguka katika hali isiyo ya kawaida, na pengine hii ni tafsiri ya mgogoro mkubwa unaofuka kwenye soka ya nchi hiyo na shirikisho la taifa la mchezo huo.

Nigeria walianza kuongoza katika dakika ya 13 kwa bao la Efe Ambrose, lakini Prince Oniangue akawasawazishia Mashetani Wekundu dakika mbili tu baadaye.

Ilikuwa mechi ngumu iliyochezwa kwenye uwanja wenye mabonde na vilima kiasi cha kufanya umiliki wa mpira kuwa mgumu.

Muda mfupi baada ya kipa Austin Ejide kufanya kazi nzuri ya kumzuia Francis Nganga kufunga, wageni walisonga mbele kwa bao la dakika ya 40 lililofungwa na Thievy Bifouma.

Wakati Nigeria wakijiuliza, Bifouma aliwafyatua tena kwa kutia kimiani bao la tatu katika dakika ya 53 kwa penati baada ya kuchezea rafu na Ogenyi Onazi.

Nigeria waliendelea kujitahidi na Gbolahan Salami alichomoa bao moja wakati mechi ikiwa imebakiza dakika tano kumalizika.

Nahodha mpya wa Nigeria, Austin Ejide alikiri kwamba hawakucheza vizuri ikilinganishwa na wageni Kongo, akisema waliwadharau na hivyo wakaadhibiwa.

Bifouma anasema walifanya kazi yao ipasavyo wakijua walikuwa wakikabiliana na moja ya timu kubwa zaidi barani Afrika na sasa watatupia macho mechi ijayo dhidi ya Sudan Jumatano hii.

Katika mechi nyingine iliyochezwa Kumasi, Ghana, wenyeji waliishia kuzomewa muda mwingi wa mechi yao baada ya kwenda sare na Uganda kwa 1-1.

Wawakilishi hao wa Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka huu walikabiliana na upinzani mkali kutoka Uganda kwenye dimba la Baba Yara.

Uganda Cranes walipata bao lao kupitia kwa Tony Mawejje lakini Andre Ayew akawasawazishia Black Stars muda mfupi tu baada ya kuanza kipindi cha pili.

Cameroon walianza vyema maisha mapya bila Samuel Eto’o kwa kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jijini Lubumbashi. Mabao yao yalifungwa na Clinton N’jie anayekipiga Ufaransa na Vincent Aboubakar wa Porto ya Ureno.

Matokeo mengine ya mechi za wikiendi hii ni Ethiopia kulala 2-1 mikononi mwa Algeria, Zambia na Msumbiji kwenda suluhu na Gabon kuwanyuka Angola 1-0.

Burkina Faso waliwaadhibu Lesotho 2-0, Niger wakafunzwa soka na Cape Verde na kulala 3-1, Ivory Coast wakachanua kwa kuwafunga Sierra Leone 2-1, Tunisia wakawapiga Botswana 2-1, huku mechi baina ya Mali na Malawi ikiahirishwa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Costa, Sturridge majeruhi

Ujerumani wawazidi Scotland