Joseph Omog vs George Lwandamina: nani kuibuka mshindi
Kocha Mcameruni Joseph Omog na Mzambia Lwandamina, kwa mara ya kwanza watakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi uwanja wa taifa majira ya saa kumi jioni
Makocha hawa wenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya klabu bingwa Afrika, kila mmoja ameanza kuji nasibu kuibuka na ushindi mnono kutokana na maandaliza ya kikosi chao.
Falsafa ya Joseph Omog
Mwalimu huyu ni muhimili wa mfumo wa 4-3-3 kwa muda mwingi, mara nyingi hujaza viungo wengi katikati na mshambuliaji mmoja, pia kuna kipindi utumia mfumo wa 4-4-2 flati kwa kuanza na washambuliaji wawili.
Falsafa ya George Lwandamina
Lwandamina upendelea soka la pasi fupi fupi na mashambulizi ya kushtukiza, mara nyingi uingia na mfumo wa 4-4-2 kwa kupendelea kujenga mashambulizi yake kupitia pembeni.
Rekodi ya Joseph Omog Ligi Kuu
Omog kaitumikia Simba katika mechi 22 za Ligi Kuu amekusanya alama 51, ameshinda mechi 16 sare 3 na kupoteza mechi 3, katika michezo hiyo timu yake imefunga magoli 38 na wao kuruhusu magoli 7 pekee.
Rekodi ya George Lwandamina Ligi Kuu
Mzambia huyu ameanza kukinoa kikosi cha Jangwani katika mzunguko wa pili akichukua nafasi ya Muholanzi Hans, tangu Lwandamina atue Yanga amecheza mechi 6 pekee na kujikusanyia alama 16, ameshinda mechi 5, sare moja bila kufungwa hata mchezo mmoja, timu yake imefunga magoli 15 na kuruhusu goli moja pekee
Mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Omog
Mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Omog ni mlinzi wa kati, Mzimbabwe Method Mwanjale, mlinzi huyu amekifanya kikosi cha mwalimu Omog kuwa na uwiano mzuri kwenye eneo la ulinzi.
Mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Lwandamina
Kwenye kikosi cha Mzambia, Lwandamina kimekusanya nyota kibao katika karibu kila idara, ila mchezaji muhimu kwenye kikosi chake ni winga Simon Msuva, winga huyu ndiye chachu ya ushindi wa Yanga kwa karibu michezo yote, ana pika magoli na kufunga yeye pia.
Kauli ya Omog kuelekea mchezo wa Yanga
“Ukweli kwamba ubingwa wetu msimu huu upo kwenye mchezo dhidi ya Yanga, na tumejipanga kuhakikisha tunashinda hatupo tayari kuona tuna tunafungwa au kutoka sare kwasababu huo ndiyo mchezo pekee mgumu kwetu na endapo tutawafunga itakuwa tumewaacha idadi kubwa ya pointi,”amesema Omog.
Kauli ya Lwandamina kuelekea mchezo wa Simba
“Kitu cha msingi kwetu kabla ya kuwaza ubingwa ni kuiondoa Simba, kwenye nafasi ya kwanza na hilo nina uhakika tunaweza kulitimiza katika mechi tatu zijazo, kutokana na ari tuliyokuwa nayo hivisasa na idadi ndogo ya pointi tuliyokuwa nayo kati yetu na wao,” amesema Lwandamina.