Brazil wamefuta utegemezi wao kwa Neymar?
Ukitaja fainali za Kombe la Dunia unaitaja Brazil. Wao ndio wanaongoza kutwaa kombe hilo mara tano. Brazil ni nchi ambayo kila taifa linatamani kuchza dhidi yao na kuwafunga. Kila kocha anatamani kuwafunga Brazil ili asifiwe na kukuza wasifu wake. Kwahiyo Brazil ni kama nembo ya fainali za Kombe la Dunia.
Tangu Kombe la Dunia lianzishwe Brazil imeshiriki fainali zote. Hili ni taifa linalowavutia wengi na makocha wanaamini ndilo linalotakiwa kuchungwa kila unapopangwa nao.
Imepita miaka 18 bila kutwaa taji la Kombe la Dunia. Mara mwisho Brazil kutwaa kombe hilo ilikuwa kwenye fainali za mwaka 2002 zilizofanyika nchini Korea kusini na Japan.
Brazil inajipanga upya kupitia vipaji vipya katika ulimwengu wa kandanda. Kizazi kipya ambacho kimekabidhiwa jukumu la kutamba kwenye soka miaka kadhaa ijayo. Wachezaji chipukizi wanataka namba katika timu ya taifa maarufu kama Selecao.
Thiago Silva bado ni nahodha wao, japo ana miaka 36 kwa sasa, na ifikapo fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 atakuwa na miaka 38 zitakazofanyika nchini Qatar.
Ingawaje miaka ya karibuni Brazil haijawa taifa tishio kwenye mashindano linapofika suala la wachezaji ndani ya uwanja, lakini nje ya uwanja jina lao ni kubwa na tishio tosha. Miaka ya karibuni vipaji vya Kibrazil havikuwa tishio, na madhara yake yalionekana kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 lililoandaliwa nchini kwao ambapo walizabwa mabao 7-1 na Ujerumani kwenye mchezo wa nusu fainali.
Tangu wakati huo Brazil imeanza mikakati ya kuibuka upya kwenye mchezo huo kupitia vipaji mbalimbali. mojawpao ni kuhakikisha wanaachana na utegemezi wao kwa supastaa Nermay Junior. Kwanini wana mwelekeo huo?
Iko hivi. Mastaa kadhaa wanacheza Ligi kuu England, lakini linapofika suala la mashindano ya kimataifa mafanikio yao ni hafifu. Kwa sasa wana kizazi kipya, lakini swali la kujiuliza je kizazi hiki kitaweza kuleta mafanikio ikiwemo kutwaa kombe la dunia tena?
WAKONGWE NI DHAHABU
Linapofika suala wachezaji nyota Brazil ni lazima mwelekeo wa ushindi unaanzia kwao. Baadhi ya wachezaji hao wana majina makubwa, wamefanya mambo makubwa, hivyo wanahitaji kuongezewa damu change ili kuibuka na ushindi. Kwa kipindi hiki Thiago Silva ndiye mkongwe zaidi kuliko wote.
Beki huyo wa kati ni kipenzi cha wachezaji wengi chipukizi. Tangu alipoibuka katika soka na kuchaguliwa timu ya taifa, Silva hajawahi kuwaangusha Brazil na wala hajawekwa kando. Ni kama amejimilikisha nafasi hiyo. Kwa sasa ana miaka 36 hii ina maana bado ni mchezaji muhimu katika nafasi yake na wanahitaji mchango wake katika ulinzi ili kuimarisha uwezo wa chipukizi.
Mara nyingi amecheza sambamba na Marquinhois, ambaye wamecheza wote PSG, kisha amewahi kupangwa pamoja na wengine kama Ederr Militao wa Real Madrid. Nyota wote wawili hawajaweza kumwondoa kikosini Thiago Silva. Sasa kama wanamtegemea Silva, je Brazil wataweza kusonga mbele?
Kocha wao Tite ana mikakati ya muda mrefu kuhakikisha Brazil inafanya mambo makubwa kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022. Pengine wataingiza timu yenye ushindani mkali kuliko miaka ya 10 iliyopita. Tite anakabiliwa na kibarua kigumu cha kufanya uamuzi wa uteuzi wa wachezaji.
KUACHA KUMTEGEMEA NEYMAR
Kwa kipindi cha miaka 10 sasa huwezi kuzungumzia Brazil bila kutaja jina la Neymar. Mshambuliaji huyo wa PSG anaipenda nchi yake na amechora tattoo mwilini. Wakati fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 alikabiliwa na presha kubwa mno.
Mabega yake yalibeba mzigo mzito wa mamilioni ya wananchi wa Brazil waliokuwa na matumaini yote kwake. Naye hakuwaangusha, alijitahidi kadiri ya
uwezo wake kabla ya kufanyiwa madhambi kwenye mfupa wa mgongoni yaliyosaabisha ashindwe kuendelea kucheza michezo mingine.
Kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani Neymar hakuweza kucheza. Wabrazil waliamini bila Neymar maisha yao kisoka yalishakwama mbele ya Ujerumani. Baada ya fainali hizo maisha ya Naymer yalionekana kama yamepotea kama nahodha aliyepoteza jaketi la kujiokoa.
Brazil ilijengwa kupitia Neymar tangu akiwa timu za taifa za vijana. kila kitu kilifanywa ili Neymar afanye vizuri. Wachezaji walielewa iliBrazil ipate mafanikio ni lazima Naymer apachike mabao ya ushindi, na pasi ziende kwake.
Licha ya kupata matokeo, benchi la ufundi liliamua kuondo utegemezi huo katika timu. Mawazo ya kumtegemea Neymar kikosini yaliondolea haraka na mwanzo mpya wa mbinu uliwekwa kunusuru taifa hilo.
Tite na wasaidizi wake pamoja Shirikisho la Soka CBF waliona majeraha anyaopata Neymar mara kwa mara yanakwaza maendeleo yao. Baada ya kuondolewa Neymar kwenye mipango ya timu ya taifa mambo mapya yakaanza kuibuka. Kisha Brazil ikatwaa kombe.
Mwaka 2019 Brazil walikuwa wenyeji wa fainali za Copa America. Neymar hakushiriki mashindano hayo baada ya kupata majeraha kwenye mchezo w akirafiki dhidi ya Qatar, hivyo ilikuwa wazi kuwa nyota huyo hatakuwepo kwa muda. Tite alikiongoza kikosi chake kwenye fainali hizo akipanga wachezaji wapya ambao walibeba majukumu yote na kuibuka washindi.
Tangu fainali hizo ilionekana wazi Brazil wameacha kumtegemea Neymar. Kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Bolivia wlaipata ushindi wa mambo 5-0 mwezi Oktoba mwaka huu. Kwahiyo majukumu ya kufunga mabao na kutengeneza yanahusisha wachezaji wote sio mmoja kama ilivyokuwa kwa Neymar. Je, ni dalili ya mwanzo mpya? Muda utaongea.
VIPAJI VIPYA, DAMU CHANGA
Kama nchi, Brazil inasifikakwa vipaji. Haijawahi kuishiwa vipaji hata kama haifanyi vizuri kimataifa. Baada ya kuondokana na utegemezi kwa Neymar, sasa
vipaji vipya vimeingia. Kwenye fainali za Copa Amaerica nyota ya mshambuliaji Everton Soares iling’ara, naye Richarlison akaweka alama nzuri kikosini.
Yupo Rodrygo Goes ambaye anakuja kuipa uhai Brazil kwenye fainali za mwaka 2022. Akiwa na miaka 19 Rodrygo Goes ameibuka kwenye mechi muhimu na kufanya mambo makubwa. Baadhi ya wachambuzi wanasema Rodrygo atachukua nafasi ya Neymar na kuwa mshambuliaji wao mahiri miaka ijayo.
Rwal Madrid walilazimika kulipa kiasi cha pauni milioni 50 kumsajili Rodrygo alipokuwa na miaka 17 akichezea klabu ya Santos. Aliitwa kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Argentina, ambako Brazil walizabwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki. Mastaa wengine walioibuka Brazil ni Lucas Pacqueta (Olumpique Lyon) na Renan Lodi (Atletico Madrid) watachukua nafasi ya Marcelo. Wengine ni Wesley Moraes, Garbiel Menino, Bruno Guimaraes, Pedro, Vinicius Junior na Richarlison.
UZOEFU WA MAKOMBE
Kwa miaka ya karibuni Brazil haiajcheza vizuri na matokeo yake yamekuwa ya kusuasua. Kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi waliishia robo fainali baada ya kufungwa na Ubelgiji.
Brazil walishinda mechi nane na kutoka sare moja. Kwa kiasi fulani takwimu hizo zinawapa nafasi ya kuamini watafanya vizuri fainali zijazo. Tayari mwaka 2019 wamechukua Copa America, wanaongoza kuwania kufuzu kombe la dunia 2022.
Wapo wachezaji wenye uzoefu wa kutwaa makombe kikosini. Gabriel Jesus na Phlippe Coutinho wakipangwa na chipukizi kadhaa kwenye mechi za kufuzu wameonesha kiwango cha kuvutia.
Argentina wanashika nafasi ya pili nyuma ya Brazil. Licha ya kupitia nyakati ngumu, lakini sasa Brazil wameonesha wazi wanakuja kuleta mambo makubwa. Wakifuzu fainali za 2022 bila shaka Tite atashusha kikosi cha maagamizi. Tusubiri.
Comments
Loading…