in

Kocha mpya Taifa Stars afurahia kuivaa Misri

Kocha mpya wa timu ya taifa ya soka, Taifa Stars, Mdenmarak Jan Poulsen, alisema amefurahishwa na taarifa kuwa timu yake itacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Misri itakayopigwa Agosti 11 jijini Cairo, Misri.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam juzi usiku, Poulsen alisema kwamba amefurahia kuwepo kwa mechi hiyo kwani itampa nafasi ya kuwajua vizuri wachezaji wake.
Kocha huyo aliongeza kwamba, mechi hiyo pia itampa nafasi ya kujua namna atakavyokabiliana na Algeria katika mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon na Equatorial Guinea mwaka 2012, kwani anaamini kuwa soka la β€˜waarabu’ hao wa Afrika ya Kaskazini lifanana.
Licha ya kuifurahia mechi hiyo dhidi ya Misri, Poulsen atakumbana na kibarua kigumu kwani rekodi zinaonysha kuwa katika mechi ya mwisho baina ya timu hizo, Stars ilikula kipigo cha 5-1 kutoka kwa β€˜mafarao’ hao, goli la Stars likifungwa na John Bocco.
Wakati huohuo, Poulsen ambaye jana alikuwepo pia kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Yanga ikiwaadhibu Telecom Wanderers kwa kipigo cha 4-1, atakutana na waandishi wa habari wiki hii na kuelezea mikakati yake ya kuiimarisha Stars.
CHANZO: NIPASHE
Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Motivation rocks athletics camp

Wayne Rooney smoking and urinating in the street: it’s no wonder United hero is out of puff