in , , ,

Kocha Laudrup atupiwa virago Swansea

Kocha Michael Laudrup wa Swansea amefukuzwa kazi na nafasi yake itashikwa kwa muda na Nahodha wa Timu, Garry Monk.

Laudrup ameondolewa wakati timu ikijiandaa kukabiliana na watani zao wa jadi katika Wales, Cardiff City wikiendi hii.

Habari hizi zimekuja siku moja tu baada ya Mwenyekiti wa Swansea, Huw Jenkins kukanusha madai kwamba walikuwa wakijadili hatima ya kocha huyo raia wa Denmark aliyewika kwenye soka kwa kucheza Barcelona na Real Madrid.

Laudrup amepata kuwa kocha msaidizi kwenye timu ya taifa lake na kocha wa Brondby, Getafe, Spartak Moscow, Real Mallorca na Swansea.

Licha ya klabu mbili hizo kubwa za Hispania, Laudrup amechezea KB, Brondby, Juventus, Lazio, Vissel Kobe na Ajax.

Huyu ndiye mchezaji wa kwanza kutwaa ubingwa wa La Liga mara tano mfululizo akichezea klabu mbili tofauti.

Pamekuwa na tetesi za kufukuzwa kwa Laudrup tangu Swansea walipofungwa 2-0 na West Ham Jumamosi iliyopita, kikiwa ni kipigo cha sita kwa msimu huu na sasa wanashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi.

Hata hivyo, Manchester United wamefungwa mara nane na wanashika nafasi ya saba lakini hawana wazo la kumfukuza kocha wao, David Moyes.

Palikuwa na tetesi awali kwamba Monk anayeheshimiwa klabuni hapo angepewa majukumu kwenye benchi la ufundi baadaye, lakini sasa amejikuta akivaa viatu vya kocha mkuu.

Monk atasaidiwa na mshambuliaji mahiri wa zamani wa klabu hiyo, Alan Curtis wakati watakapojaribu kulipa kisasi cha kufungwa 1-0 na mahasimu wao kwenye mzunguko wa kwanza.

Laudrup alichukua nafasi hiyo kutoka kwa kocha wa sasa wa Liverpool, Brendan Rodgers Juni 2012 na akafanikiwa kuwapatia Kombe la Ligi, taji kubwa la kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Aliwapeleka kwenye Ligi ya Europa ambapo waliwapiga Valencia ya Hispania 3-0 na sasa watakabiliana na Napoli ya Italia katika hatua ya timu 32 zilizobaki.

Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 kwa Swansea kumfukuza kocha, lakini kwa muda mrefu pamekuwapo na sintofahamu juu ya Laudrup na klabu, akidaiwa kutakiwa na klabu kubwa ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti alisema kwamba wamejadiliana na Laudrup na kubaini kwamba mazingira yaliyopo hayatamwezesha kuiongoza timu katika mechi zilizobaki na kupata matokeo wanayoyataka.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

MTIBWA SUGAR, SIMBA KUUMANA MOROGORO

Simba avutwa sharubu Moro