*Aacha tetesi nyingi juu ya anakokwenda
*Manchester City, Real Madrid wafikiriwa
Kocha wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp ameachia ngazi.
Klopp aliyewapeleka vyema Dortmund msimu uliopita, amejikuta akiwa mkiani mwa Bundesliga Februari kabla ya kufufuka kidogo, lakini hali si shwari kama ilivyotarajiwa.
Kocha huyu mwenye umri wa miaka 47 amekuwa akitajwa kabla kwamba angekuwa mrithi wa Arsene Wenger msimu wakati Arsenal wakifanya vibaya na pia baadaye ikaelezwa kwamba siku Mfaransa huyo atakapostaafu atachukua mikoba yake.
Klopp aliyekuwa na mkataba na Dortmund hadi 2018 ameiomba klabu yake kumwacha aondoke zake, akisema kwamba hajachoka, hajawasiliana au kuingia mkataba na klabu nyingine wala kwamba anaenda mapumziko au kujinoa.
Klopp aliyekuwa na mkataba na Dortmund hadi 2018 ameiomba klabu yake kumwacha aondoke zake, akisema kwamba hajachoka, hajawasiliana au kuingia mkataba na klabu nyingine wala kwamba anaenda mapumziko au kujinoa.
Hiyo inamaanisha kwamba yupo tayari kwa jukumu la ukocha kwenye klabu nyingine baada ya kuwa na Wajerumani hao tangu 2008. Anaondoka akiwaacha Dortmund wakiwa pointi 37 nyuma ya vinara na watani zao, Bayern Munich, ikimaanisha kutwaa ubingwa ni ndoto.
Hata kufuzu kwa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (UCL) inaelekea haitawezekana msimu huu, jambo ambalo si kawaida kwa Dortmund ambao pia wamekuwa wakifanya vyema katika hatua za mwanzo. Alikuwa na mkataba hapo hadi 2018.
Amewapa ubingwa wa Ujerumani mara mbili na katika msimu wa 2012/13 aliwaongoza Dortmund kwenye fainali ya UCL lakini sasa wanashika nafasi ya 10 kwenye ligi kuu nchini mwao.
Klopp pia amekuwa gumzo kwamba anaweza kupewa nafasi ya ukocha Manchester City ikiwa wamiliki wake wataamua kumfuta kazi Manuel Pellegrini ambaye timu yake inasuasua kutetea ubingwa, wakiachwa nafasi ya nne nyuma ya Chelsea, Arsenal na Manchester United.
Kadhalika pamekuwa na minong’ono kwamba anaweza kujiunga na Real Madrid ikiwa Kocha Carlo Ancelotti atafukuzwa huko. Pia wengine wanadhani kama Man City watamshawishi Pep Guardiola kuondoka Bayern na kujiunga nao, Bayern wanaweza kumchukua Klopp.
Kadhalika kuna tetesi kwamba Napoli wanaweza kumchukua Mjerumani huyo, kwani kocha wao, Rafa Benitez huenda akarudi England kufundisha moja ya klabu za ligi kuu. Zipo tetesi za Sam Allardyce wa West Ham kuandaliwa kufungishwa virago.
Lakini pia inaelezwa kwingineko kwamba West Ham wanataka kumfuata Kocha wa Swansea, Gary Monk ili achukue mikoba ya Mwingereza Allardyce, maarufu kama Big Sam.
Tetesi nyingine ni kwamba kocha wa zamani wa Aston Villa aliyefukuzwa baada ya timu kufanya vibaya, Paul Lambert anaweza kuchukua nafasi ya Klopp.
Hata hivyo, ikiwa Man City watamwondosha Pellegrini wanaweza kumweka badala yake msaidizi wake, Patrick Vieira na Real Madrid wakimwondoa Ancelotti wanaweza kumrithisha hapo Zinedine Zidane ambaye majuzi amesema angefurahi kuipata nafasi hiyo.
Comments
Loading…