in , , ,

Kikosi cha England chatajwa

*Waliong’ara Ligi Kuu waitwa

Kocha wa Timu ya Taifa ya England – Three Lions, Roy Hodgson ameteua sura mpya kwa kuzingatia wachezaji walivyofanya kwenye ligi na kuwachanganya na wazoefu.

Uchaguzi wake haukubagua wachezaji kutoka timu zilizoshuka daraja, ikiwa ni tofauti na Tanzania – Taifa Stars, ambapo kocha Mart Nooij ameendelea kuteua kutoka klabu kubwa tu na bado wakatolewa michuano ya Cosafa.

Hodgson, kwa mfano, amewaita mshambuliaji wa Leicester, Jamie Vardy na wa Queen Park Rangers (QPR), Charlie Austin kwa ajlili ya mechi dhidi ya Jamhuri ya Ireland na Slovenia Juni hii.

Vardy, 28, amefunga mabao manne msimu huu na timu yake imenusurika kushuka daraja, wakati Austin, 25, amefunga mabao 17 lakini QPR wameshuka daraja.

Hodgson pia amemwita kipa wa Burnley walioshuka daraja, Tom Heaton, 29, wote ikiwa ni mara yao ya kwanza. Kipa huyu ndiye pekee katika Ligi Kuu ya England hadi sasa amecheza dakika zote za mechi zote msimu huu kwa klabu yake.

Hodgson angeweza kuendelea na kikosi cha awali, kwani England hawajafungwa katika michezo tisa, ambapo wameshinda mechi zao tano za kufuzu kwa michuano ya Euro 2016.

Vijana wa Hodgson wanaongoza kwenye kundi lao la G, wakiwa alama sita juu ya wanaowafuata ambao ni Slovenia. Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Uswisi, Lithuania, Slovenia na San Marino.

Mlinzi wa Everton, Leighton Baines ameachwa kwa sababu alifanyiwa upasuaji wa kiwiko cha mguu na atakuwa nje ya uwanja hadi kabla ya mwanzo wa msimu ujao. Mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge naye yu nje kwa majeraha pia.

Winga wa Liverpool aliyezua utata kwa kukataa kuhuisha mkataba wake na klabu hiyo, Raheem Sterling, ameitwa kwenye kikosi cha Hodgson chenye wachezaji 24.

Hodgson amesema amemchukua Austin ili awaoneshe katika mazoezi kipi anaweza kufanya, lakini amesema hawezi kumhakikishia kucheza mechi ya ushindani lakini amemwingiza kwenye kundi baada ya kuona na kusikia vitu vyake vizuri uwanjani.

Akasema Vardy aliyecheza mechi 33 za Ligi Kuu ya England ana kasi na anajituma sana uwanjani na kwamba ana kiwango kinachovutia makocha na sasa anataka amjue vizuri zaidi.

Mwingine aliyeitwa ni Harry Kane (20) wa Tottenham Hotspur, ambaye ni raia wa England anayeongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi kuliko Austin (17).
Kikosi kizima cha England na klabu za wachezaji kwenye mabao ni kama inavyoonekana hapa chini:

Magolikipa: Rob Green (QPR), Joe Hart (Manchester City), Tom Heaton (Burnley).

Walinzi: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Southampton), Kieran Gibbs (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Chris Smalling (Manchester United).

Viungo: Ross Barkley (Everton), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), Ryan Mason (Spurs), James Milner (Manchester City), Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham), Theo Walcott (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal).

Washambuliaji: Charlie Austin (QPR), Wayne Rooney (Manchester United), Jamie Vardy (Leicester), Danny Welbeck (Arsenal).

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Barcelona watenga £50m Arsenal kumtwaa Ramsey

Manchester United matumbo joto