TIMU ya Wanaume ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam ‘The Dream Team’ itaanza kampeni yake kusaka ubingwa wa mchezo huo kwa miji mikuu ya Afrika Mashariki na Kati kwa kuvaana na Kampala.
Mechi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam itahudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwa kama mgeni rasmi.
Simon Msofe, ambaye ni rais wa kamati ya michezo ya miji mikuu alisema jana kuwa maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo yamekamilika na baadhi ya timu zimeshawasili.
” Timu nyingi zimeshawasili kwa ajili ya michuano hiyo na nina imani itafanyika kwa amani ili mshindi apatikane kihalali na kwa haki pasipo lawama.
” Nawaomba hata waamuzi kufuata sheria zote za mchezo huu ili kuepusha malalamiko ya mara kwa mara yanayotokea kwa timu,”alisema Msofe
Aliitaja miji itakayoshriki michuano hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza (Tanzania), Mombasa, Nairobi (Kenya) na Kampala, Uganda.
” Mji wa Mogadishu tulitarajia kuwa nao, lakini hakuna taarifa kuwa kwao kuna machafuko ya kisiasa.
Pia, Kigali (Rwanda) nao walithibitisha, lakini mpaka leo hatuna mawasiliano nao tena,” alisema
Michuano hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro. Wadhamini wengine ni, Omo, Clouds FM, TPI, Airport Night Park na Bank M Limited.
Comments
Loading…