in , , ,

Kenya,Uganda wanabebwa na Simba, Yanga

Ukuta wa Simba utaamua ubingwa msimu huu

Kenya kwa mfano, timu zao katika mashindano ya CAF hazina majina makubwa tena

Macho na masikio ya wengi yapo katika ukanda wa Afrika mashariki. Macho na masikio hayo ni kuangalia mwenendo wa mpira wa miguu katika ukanda wetu. Kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa kama AFCON ni jambo kubwa sana. Tanzania imeshaandaa AFCON ya vijana mwaka 2019. Kenya imekuwa mahiri na mwenyeji mara kadhaa kwenye mashindano ya riadha (mbio za nyika) na imetoa mabingwa wa dunia katika mchezo huo pamoja na mchezo mwingine wa Kriketi. Uganda nao wamekuwa wakitamba kwenye riadha na michezo mingine. Kenya na Uganda zimebahatika kuwa na timu mbili zilizowahi kufanya vizuri katika mashindano ya CAF, Gor Mahia (Kenya) na SC Villa (Uganda).

Zamani timu kama Mumias Sugar na Kenya Breweries (Kenya) zilikuwa zinasifika kwa kandanda bora barani Afrika. SC Villa ilikuwa jogoo la kandanda kwa Uganda na alikuwa mwakilishi mzuri wa mashindano ya CAF. Lakini katika hali inayosikitisha miamba hii imetoweka katika ramani ya soka barani Afrika.

Tanzania Sports

Kenya kwa mfano, timu zao katika mashindano ya CAF hazina majina makubwa tena. Katika mchezo uliopita kati ya Al Ahly ya Misri na Gor Mahia ulileta huzuni na maudhi. Gor Mahia ilikubali kipigo cha mabao matatu nyumbani na kutupwa nje ya mashindano ya CAF. Uganda nako hakuna klabu iliyotoboa kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho lwa Klabu Bingwa.

Unaweza kusamehe timu za Rwanda na Burundi ambako hazijafanya vizuri kwa miaka mingi. Ni APR pekee ilijaribu kufurukuta na kujikuta ikitupwa nje ya mashindano na miamba ya Pyramids ya Misri. APR ndiyo waliwatupa nje ya mashindano Azam fc ya Tanzania.

Nchini Jmahuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado zipo timu imara hadi sasa kama vile FC Lupopo, AS Vita, TP Mazembe zimekuwa zikionesha umhiri kwenye michuano ya CAF ingawaje ni Mazembe pekee wamesali msimu huu. DRC ni mwanachama mwenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwahiyo naye anawakilisha ukanda huu. Ukiangalia orodha ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho, utaona majina ni yaleyale toka Tanzania na baadhi ya nchi barani Afrika.

Mfano katika Ligi ya Mabingwa, Yanga wapo kundi A wanapeperusha bendera ya Afrika Mashariki wakiwa sambamba na TP Mazembe na AS Maniema Union. Katika A Yanga wamepangwa na TP MAzembe, A Hilal ya Sudan na MC Alger. Katika kundi B zipo timu za Mamelodi Sundowns, Raja Casablanca, AS FAR, AS Maniema Union. Kundi C kuna timu za Al Ahly, CR Belouizdad, Orlando Pirates na Stade D’abidjan. Kundi D lina timu za ES Tunisia,Pyramids,Sgranda Esperanca na Djoliba AC De Bamako. Ukienda kwenye kombe la Shirikisho pia Simba wanapeperusha bendera ya Afrika mashariki. Simba wapo kundi A sambamba na Sfaxien,CB Constantine, FC Bravos Do Marquis,. Ukienda kundi B kuna RS Berkane, Stade Malien,Stellenbosch FC na CD Lunda-Sul. Kwenye kundi C zipo timu za USM Alger,Asec Mimosas,ASC Jaraaf na Orapa United. Katika kundi D zipo timu za Zamalek SC, Enyimba, Al Masry SC na A. Black Bulls.

Kwenye mashindano yote mawili hakuna timu toka Kenya wala Uganda. Kwenye mashindano ya African Football League pia hakuna timu toka Kenya inayoweza kutoboa wala kukaribia sifa za Simba. Katika mazingira hayo unaona ukanda wa Afrika mashariki unabebwa na Simba na Yanga kwa kila hali. Kabla ya DRC kujiunga kwenye jumuiya ya Afrika mashariki hakukuwa na TP Mazembe. Lakini sasa ukanda huu unazo timu nne za TP Mazembe, AS Maniema Union, Yanga na Simba.

Kwa wenzetu wa Kenya na Uganda hakuna timu zao. Katika nukta hiyo lazima tukiri hii ni changamoto kubwa kwa nchi hizo katika kuinua kiwango cha soka ukanda huu. Wakati tukielekea kuwa wenyeji wa AFCON timu zinazochomoza kwenye mashindano ya CAF inabidi ziwe nyingi na kudhihirisha ukanda huu ni moto wa kuotea mbali. Hii kasumba ya kubebwa bebwa enyi watani zetu badilikeni. Inafika wakati Ligi Kuu Tanzania Bara inaingiza timu nne kwenye mashindano ya CAF lakini Kenya na Uganda bado zinahaha hata kupata nafasi mbili. Mabadiliko yanahitajika ili kuinua ukanda wetu katika kandanda.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Yanga wamenyimwa uhondo CAF

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids

Fadlu Davids apewe pongezi za mapema kwanza