in , , ,

KASHFA YA MLUNGULA FIFA:

*Uchafu zaidi wawekwa wazi

*Mshirika wa Blatter akunja $1.5m

Kashfa ya mlungula inayoliandama Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) imezidi kuumuka, baada ya kutolewa madai ya rushwa katika mchakato wa kupata mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2002.

Madai yanayotolewa sasa na kuzidi kuupaka matope uongozi wa miaka 17 wa Rais Sepp Blatter ni kwamba ilibidi Japan walilipe Shirikisho la Soka la Amerika dola milioni 1.5 ili kupata kura yao kwa uenyeji wa fainali za 2002.

Gazeti la Hispania limechunguza na kuanika kwamba Japan walilipa shirikisho hilo, CONMEBOL, baada ya kuelezwa na baadhi ya ‘watu wa Fifa’ kwamba mambo mle hayaendi kirahisi na kwamba mkono mtupu haulambwi.

Hali hiyo inaongeza doa kwa Fifa ambayo tayari inatuhumiwa kuhusisha mlungula kwenye mchakato wa uenyeji wa fainali za 2018 na 2022 nchini Urusi na Qatar kwa mtiririko huo.

Japan waliandaa fainali hizo sambamba na Korea Kusini na inaelezwa kwamba baada ya fedha hizo kuchukuliwa na maofisa waliokuwa pia na vyeo ndani ya Fifa, zilivutwa na kuingizwa kwenye akaunti binafsi ya Rais wa shirikisho hilo, Nicolas Leoz.

Mmoja wa maofisa wa Fifa walio karibu zaidi na Leoz ni Mbrazili Ricardo Teixeira anayethibitisha kwamba kulikuwa na mazonge kwenye mchakato wa kura kwa ajili ya fainali za 2018 na 2022.

Teixeira anasema kwamba kwa matukio hayo, lazima uchunguzi wa jinai ufanyike ili hatimaye wahusika wapelekwe mahakamani kujibu mashitaka yao.

Leoz anatoka nchini Paraguay na amewekwa katika kizuizi cha nyumbani mwake wakati akisubiri kusafirishwa kwenda Marekani kujibu mashitaka yanayomkabili.

Pamoja na kupokea rushwa, msaidizi huyo wa Blatter anatakiwa kujibu madai kadhaa ya utakatishaji fedha. Inadaiwa kwamba mfanyakazi wa zamani wa CONMEBOL ambaye hakutajwa jina ndiye alitoa nyaraka zilizotoboa siri hiyo.

Leoz amekaa madarakani katika soka kwa miaka 27, na sasa akiwa na umri wa miaka 86 ndipo inabainika kwamba alikuwa akihamisha mamilioni ya dola za Marekani kutoka akaunti za shirikisho kwenda zake binafsi na za washirika wake.

Aliachia ngazi mwaka juzi kutokana na maradhi, akiwa na umri wa miaka 83 akiwa mshirika mkubwa wa Blatter mwenye umri wa miaka 79 na aliwania tena urais wa Fifa na kushinda mwezi uliopita.

Ataachia ngazi karibuni kutokana na kashfa zinazoizunguka Fifa.

Inaelezwa kwamba dola hizo milioni 1.5 zililipwa na aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Japan, Ken Naganuma ili zigawanywe kwa nchi 10 wanachama wa CONMEBOL, lakini baada ya kufanikiwa kuwashawishi, Leoz alitia fedha hizo mfukoni.

Kuna waraka umetolewa ukionesha kwamba Leoz alihamisha £750,000 kwenye akaunti yake na mkewe, Maria Clemencia Perez. Nyingine zilitolewa kwa Eduardo de Luca, Katibu Mkuu wa CONMEBOL na Zorana Danis, mshirika wa ofisa wa Fifa anayeshitakiwa kwa mlungula, Chuck Blazer.

Leoz alikitaka Chama cha Soka (FA) cha England kufanya mpango apewe tuzo na Malkia Elizabeth II lakini pia Kombe la FA lipewa jina lake ili awsaidie England kupata uenyeji wa fainali za 2018.

Kamati ya Maadili ya Fifa ilielezwa juu ya masuala hayo pamoja na waliokuwa wakiunga mkono uenyeji wa Hispania na Ureno kwa 2018 ndio walikuwa wakiunga mkono Qatar kwa 2022, lakini haikuona kosa lolote.

Shirika la Upelelezi la Marekani linawataka maofisa wa zamani wa Fifa, Jack Warner, Leoz, Alejandro Burzaco, Hugo Jinkis, Mariano Jinkis na Jose Margulies na tayari Interpol wamejulishwa kuwasaka popote walipo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Neymar arudishwa nyumbani

MAAMUZI YA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF LEO