in

Kampuni ya Bia (TBL) kutumia mamilioni kufufua Taifa Cup Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imewekeza mamilioni ya fedha kwenye Shirikisho la Soka (TFF), ikiwa ni katika mkakati wa kufufua msisimko wa michuano mikongwe ya Kombe la Taifa kwa kuiwezesha mikoa yote 23 ya soka kushiriki.

TFF na TBL, ambayo itatumia mashindano hayo kutangaza bia ya Safari Lager, juzi walisaini mkataba wa Shilingi bilioni 1.54 wa kudhamini mashindano kwa miaka mitatu.

Kati ya hizo, Shilingi milioni 580 zikitumika kila mwaka kuanzia mwaka huu ambao mashindano hayo yatakayofanyika Dar es salaam.

“Fedha hizo zitatumika kwa ajili ya posho, malazi, usafiri wa kuja Dar es salaam na usafiri wa ndani wakati wa mashindano hayo,” alisema Meneja Masoko wa TBL, David Minja wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo kwenye hoteli ya Royal Palm Movernpick juzi usiku.

“Na ili kuongeza msisimko, bingwa atajinyakulia Sh milioni 30, wakati mshindi wa pili atapata Sh milioni 15 na mshindi wa tatu sh milioni 7.5.”

Zawadi nyingine zitakazotolewa ni kwa mwamuzi bora, ambaye atajinyakulia Sh milioni 2, mchezaji bora, mlinzi bora na mfungaji bora, ambao pia kila mmoja atajinyakulia Sh milioni 2.

“Lengo la Safari Lager ni kuhakikisha mashindano haya yanaleta msisimko Tanzania na kuinua vipaji vya soka,” alisema.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera aliipongeza TFF kwa kazi nzuri ya kuendeleza mchezo huo Tanzania na kusema kuwa lengo zaidi lielekezwe kwenye timu za vijana.

Bendera, pia alivitaka vyama vya mikoa kuchagua wachezaji wenye uwezo badala ya kuangalia sura, ukabila pamoja na kupeana safari na posho wakati mchezaji hana uwezo.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga aliipongeza TBL kwa hatua yakle ya kuendeleza mchezo huo kupitia udhamini wake kwani soka ya Tanzania na popote inaendelea kutokana na udhamini.

Tenga aliitaka mikoa kuunda timu imara kwa ajili ya kuibua vipaji pamoja na kuongeza ushindani kwenye mashindano hayo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply
  1. Nakumbuka miaka ya sabini walitengeneza timu kuchagua wachezaji sehemu walizozaliwa na hiyo ilichangia kiasi kikubwa sana kuinuasoka nchini,nakumbuka akina Sunday Manara na brother wake Kitwana wao walirudi kwa Kigoma na ligi ilipamba moto mkali sana .Kama tukifanya hivyo tena italeta changamoto kubwa sana katika michezo na mikoa iliyokuwa nyuma kimaendeleo ndiyo itakayo kuwambele.Angalieni sehemu kama miji ya Mbeya na Bukoba inawachezaji wengi inatoa ambao wanacheza mpira nje ya mkoa huo,watawika sana kama watu wao wataruhusiwa kuchezea walipotoka.Wazo kama hili najua litaonekana kuashiria ukabila lakini inwezekana kujaribu kitu kama hicho.Tumeishi miaka yote bila ya kuwa na ukabila na wala udini na leo hii sports itakuwaje ituletee ukabila au kututenganisha sisi?,hicho ni kitu kisichowezekana kabisa sisi sio wakenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Premier League – Mascherano charged

Int Football – Ribery ruins Beckham’s big day