THOMAS Tuchel amepata kazi yenye heshima kubwa duniani katika kazi yake ya ukocha. Kocha huyo aliyeanzia katika klabu ya Borussia Dortmundi si mgeni katika soka la England. Tuchel amepata kufundisha timu ya Chelsea na alifanikiwa kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa hivyo alijua vyema soka la nchi hiyo. Wakati kocha Gareth Southgate alipotangaza kung’atuka wengi waliamini alistahili kuendelea lakini yeye hakuona nafasi hiyo.
Hata chama cha soka nchi hiyo kilitangaza nafasi ya ajira ya ukocha na kutoa kigezo kimojawapo ni yule mwenye sifa kubwa na katwaa ubingwa mara kadhaa. Pengine makocha waliowahi kutwaa Euro na Kombe la Dunia ni wachache ama wamepitwa na wakati lakini kigezo cha Ligi ya Mabingwa kilichompa kazi Thomas Tuchel ni dhahiri kwamba bado wamefanya Kamari ambayo hawajui italeta matokeo gani.
Tuchel anatarajiwa kuanza kazi yake mwezi Januari mwaka 2025 kwa kipindi cha miezi 18 tu kulingana na taarifa za mkataba. Ajira ya Tuchel imeshaibua mjadala mkali ikiwa kocha huyo anaweza kuifikisha kwenye nyakati za shangwe na ubingwa kumzidi Gareth Southgate. Makocha wa kigeni wenye mafanikio England ni Sven Goran Eriksson pekee ambaye alifika robo fainali mara mbili na wengine kama Fabio Capello aliishia hatua ya 16 kwenye kombe la Dunia.
Kocha mzawa mwenye mafanikio ni Gareth Southgate ambaye hadi anaondoka rekodi zake zimejaa tele. Mashindano ya Kimataifa yanapaswa kuwa sehemu ya kujivunia kwa raia wa England. Vipaji vyao na miundo mbinu waliyonayo ni sababu tosha ya kuwafanya waamini kuwa uwezo wa kutwaa mataji wanao. Inawezekana Gareth Southgate hakuchukua kombe lolote, lakini aliwafanya maelfu ya mashabiki wa England kuamini wanaweza.
Pengine Southgate hakuwa kipenzi cha baadhi ya viongozi na mashabiki lakini aliwapa matumaini na furaha England. Chini ya Southgate walishuhudia soka maridadi likitandazwa na wachezaji walifurahia kufanya kazi naye. Wachezaji wengi walijipata na kuelewa sababu za kuamini katika uwezo wao na waliona Southgate ndiye mtu sahihi kwao na aliwaonesha kwa vitendo pale alipowapa nafasi hata wale ambao hawakuamini kama wanaweza kuitw atimu ya Taifa.
Kila mashindano yalipofika Southgate alikwenda na wachezaji wa England akiwa na matumaini na ari ya kushinda taji au kufanya vizuri. Daima alikuwa anavalia tisheti lenye nembo ya Simba watatu, akikumbukwa pia kuwa miongoni mwa wachezaji mahiri wlaiowahi kutokea England na kocha wa aina yake. Wengi walifuta machunga ya Southgate kukosa penalti katika mashindano ya Euro mwaka 1996 katika hatua ya nusu fainali akiwa mchezaji mahiri wa kiungo lakini aliwavutia wengi na kuwapa furaha mashabiki wa England akiwa kocha mwenye weledi na umahiri.
Sasa England imeajiri kocha w akigeni Thomas Tuchel baada ya kuongozwa na mzawa Southgate kwa kipindi cha miaka 9. Thomas Tuchel ni raia wa Ujerumani ambaye kila mmoja anaweza kuhoji uwezo wake kwenye kuongoza timu ya Taifa kwa sababu hana uzoefu huo bali alikuwa mwalimu mzuri kwenye ngazi ya klabu.
Hapa England baadhi ya vyombo vya habari vinasema kucmhagua Tuchel ni uamuzi uliotokana na papara kwani Lee Carsley ambaye ni kaimu kocha mkuu angeliweza kukabidhiwa jukumu hilo. Thomas Tuchel alihusishwa na kuajiriwa katika klabu ya Manchester United lakini hakuweza kwenda huko kwani uongozi wa Old Traford uliamua kumbakiza Eric Ten Hag. Lakini pia inasemekana kuwa haikuwa sahihi kumteua Lee Carsley kuwa kocha mkuu, hata hivyo ujio wa Tuchel unadaiwa kuwa umeborongwa na FA.
Je Tuchel anaweza kuwa kocha bora kwa England?
Wengine wanafikiri kuwa Tuchel amekuja kuchota fedha za England kama ilivyokuwa kwa Sven Goran Ericksson na Fabio Capello kwani hawakuwa na mafanikio makubwa. Yaani wanazi hao wanaona robo fainali alizofika Ericksson sio kitu bali alikwenda kuchota fedha tu. Na wengine wanadai kuwa kocha mzawa ndiye alitakiwa kukabidhiwa jukumu la kuinoa England kwa maslahi ya kulinda mfumo wa uchezaji uliokuwa ukifanywa na Gareth Southgate.
Katika mjadala huo wa Kamari ya England inaelezwa kuna wasiwasi kama watakuw ana uwezo wa kushindana na Hispania au Ufaransa ndani ya kiwanja. Wengine pia wanatamani Pep Guardiola ndiye angelikuwa kocha wa England na kwamba kila mbinu ingelitumika kuhakikisha anapewa kazi hiyo. Hata hivyo tamaa hiyo haijatimia na sasa Tuchel ndiye kocha wao. Malalamiko ya baadhi ya washabiki ni kwamba Tuchel hana misuli ya kuifikisha mbali England ndiyo maana amepewa miezi 18 tu kuthibitisha uwezo wake na kuwa atamudu kutumikia muda mrefu. Wanaopinga uteuzi wa Tuchel wanaona hizi ni nyakati ngumu za England na hakuna matumaini kama wataweza kutembea kifua mbele kama wlaivyokuwa wakifanya enzi za Gareth Southgate.
Comments
Loading…