Takribani zimebaki wiki mbili kabla mwakilishi wa chama cha mpira wa wavu nchini TAVA kwenda Marekani kuhudhuria mkutano mkuu wa shirikisho la Dunia la mpira wa wavu FIVB kule Anheim Marekani .
Mkutano huo utakaotanguliwa na mafunzo maalumu ya uongozi tarehe 19 na 20 September 2012 utafuatwa na kikao cha mkutano mkuu tarehe 21 na 22 .
Vyama wanachama zaidi ya 200 toka kote Duniani vitashiriki mafunzo na mkutano mkuu wa uchaguzi.
Ni desturi kwa wawakilishi wa vyama vyetu hususani vya michezo kuhudhuria mikutano hiyo bila mikakati yoyote kutokana na ukweli kuhudhuria mikutano hiyo huwa kama ni shughuli binafsi za viongozi wetu.
Aghalabu hukutana na viongozi wenziwako ili kuweka mikakati hata sio kama ya nchi basi hata ya chama husika.
TAVA ilishiriki mkutano wake wa kwanza ikijigharamia mwaka 1986 kule mjini Praque Czechoslavakia ikiwa na lengo la kujitambulisha katika jamii ya kimataifa . Lakini katika miaka ya hivi karibuni TAVA imekuwa ikipata ruzuku maalum kwa tiketi kuhudhuria mikutano mikuu ya Shirikisho hilo.
Pamoja na ukweli TAVA imekuwa ikishiriki mikutano hiyo bila ya kwenda na mikakati yoyote ingekuwa vyema mwakilishi wetu mwaka huu awe na angalau msimamo ili ulete taswira ya kuendeleza mchezo huo nchini.
Niliwahi kuwa mtendaji wa ngazi ya juu wa TAVA, (katibu mkuu msaidizi na mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya TAVA) Kwa hiyo ninachokisema kina taswila ya jinsi tulivyozoea kufanya kazi na sasa.
Naamini mwakilishi wetu anayetaraji kwenda Cairo kwa mkutano mkuu wa shirikisho la mpira wa wavu Afrika CAVB mwishoni mwa wiki hii yaani tarehe 7 na 8 mwezi huu atatilia maanani masilahi ya nchi kwanza wakati wa kuweka mkakati wan chi za Afrika.
Bahati mbaya nchi nyingi za Afrika ni masikini hivyo basi nchi chache Afrika zisitumie mwanya huo ili kurubuni nchi hizo kwa masilahi yao .
Wakati umefika kwa mabadiliko ya kweli . Uwazi na ukweli lazima uonyweshe katika kuendeleza nchi zetu.
Binafsi nilikuwa na mapendekezo yafuatayo kwa Shirikisho letu la Dunia FIVB katika kuendeleza mpira wa wavu duniani na haswa nchi zetu barani Afrika.
1 Kuendeleza mfuko wa maendeleo kwa nchi wanachama kifedha haswa nchi maskini ili nazo ziweze kusimama kidete haswa kwa timu zao za taifa. Mpango huu ikiwezekana uwe wa miaka minne ili ziweze kushiriki mashindano makubwa ya Dunia na Olimpiki.
2 Kuhakikisha Shirikisho la Dunia la mpira wa wavu FIVB linaweka mpango mkakati yaani strategic planning ikishirikiana na vyama vya taifa NFs
3 Kurekebisha madaraka makubwa waliopewa viongozi wa Bodi ya Shirikisho hilo la Dunia FIVB na ikiwezekana kupunguza gharama za posho zao ili ziende katika mfuko wa maendeleo.
4 Kuangalia muundo wa waajiriwa wa shirikisho hilo na ikiwezekana ni kutoa fursa waajiriwe watu kwa quota toka kila kontineti wenye sifa kamilifu.
5 Kuandaa tamasha kila baada ya miaka miwili kwa nchi wanachama ili kutoa fursa kwa kila nchi kushiriki na kujifunza katika kujiandaa na mashindano makubwa.
Naamini sio yote yanaoweza kupata fursa ya kukubaliwa lakini ni vyema washiriki wetu katika mkutano wa Cairo Egypt na Ainheim USA katika wiki mbili tatu zijazo wakijikita zaidi katika kuona fursa ya maendeleo kwa mchezo wetu nchini.
Comments
Loading…