in

Je netiboli ni mchezo wa ndani au nje?

Chama cha mchezo wa netiboli nchini Tanzania  (Chaneta) kimesema hakitaweza kufanya michuano ya netiboli ya Dunia ndani ya uwanja wa Taifa (Uwanja mpya )kutokana na  uwanja huo  kukosa kapeti ambalo lingewekwa ndani ya uwanja  huo.

Katibu mkuu wa Chaneta Anna Kibira amesema upatikanaji wa kapeti la  kuchezea netiboli litachukua muda wa miezi sita hivyo mpaka kapeti lipatikane tayari mashindano yatakuwa yameshafanyika.

Kibira amesema kutoka na kukosa kapeti mashindano hayo yatafanyika nje ya uwanja wa TAIFA ambapo watatengeneza magoli pamoja na sehemu ya kukaa mashabiki na timu husika.

Amesema uamuzi huo umeafikiwa baina ya Chaneta na  shirikisho la mchezo wa netiboli Duniani (IFNA) ambao walifika hapa nchini kukagua sehemu ya kufanyia mashindano hayo.

Mpaka sasa nchi nane zimethibitisha kushiriki mashindabno hayo ya Dunia yaliopangwa kufanyika September mwaka huu Jijini Dar es salaama na Tanzania ndio wenyeji wa mashindano hayo.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuanda mashindano makubwa ya mchezo huo wa Netball na hivi sasa harakati za kuanda timu ya Taifa zinaendelea.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Waamuzi kupewa mafunzo

Ronaldo revels in Real welcome