TAKRIBANI miaka 7 sasa mashabiki wa Ligi Kuu wameshuhudia kandanda safi kutoka kwa vilabu vyake wakiongozwa na Simba na makocha gwiji wa ufundi wamewachizisha wadau wengi. Kwa miaka minne mfululizo Simba walikuwa akicheza soka la aina yake, walitamba Ligi Kuu, wakatikisa Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwa timu ya kuogopek. Umahiri wa Simba uliwaleta vigogo wa soka hapa nchini kama vile Al Ahly, Kaizer Chifesm,Orlando Pirates, Raja Casablanca na timu nyinginezo.
Kutoka Ligi ya Mabingwa hadi Kombe la Shirikisho kote Simba wakatamba. Watani wao jadi Yanga wakapokea jahazi kwa kuanzia Ligi Kuu hadi Kombe la Shirikisho kisha Ligi ya Mabingwa. Kote nchini makocha waliozifundisha timu hizo waliwachizisha mashabiki na wadau wa soka. Makocha hao walifanya kila juhudi kuhakikisha timu zao zinafanya vizuri kwenye mashindano ya Kimataifa.
Pengine sifa hizo pia ziwafikie viongozi wa vilabu husika. kwa misimu mitatu mfululizo Yanga walicheza soka la aina yake wakiwa na kocha Nasredine Nabi kabla ya kupokelewa na Miguel Gamondi. Si siri makocha hawa waliwapagawisha mashabiki wa Yanga na wadau wa soka nchini. Yanga walifika fainali ya Kombe la shirikisho licha ya ushindi wao ugenini wa 1-0 pale jijini Algeria bado hawakufanikiwa kunyakua kombe hilo baada ya kuruhusu kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza.
Nabi aliondoka Yanga, kisha akaja Miguel Gamondi. Kocha huyo kama alivyokuwa kwa mwenzake aliwapagawisha wanaYanga. Mashabiki wanapomkubali na kumhusudu kocha wao maana yake wanamwamini hata katika nyakati ngumu na kwamba anaweza kutatua changamoto zinazoikabili timu yake. Katika kikosi cha Yanga kuna wachezaji mchanganyiko na wenye umri tofauti ambao wanao uwezo wa kuleta matokeo chanya.
Kwenye mashindano ya Kimataifa msimu huu wameanza na kocha mpya baada ya kutimuliwa Miguel Gamondi. Kocha Gamondi alitimuliwa baada ya kuzabwa mabao 3-1 na Tabora United. Kwa msingi huo menejimenti ya Yanga iliamua kumwajiri kocha mpya mwenye mafanikio ya kuifisha timu kwenye nafasi ya sita ya Ligi Kuu Afrika kusini, Sead Ramovic aliyekuwa klabu ya TX Galaxy.
Kuondoka kwa Gamondi kulishtua wengi na mashabiki waliamini ndiye mtu pekee anayaweza kupambania timu yao hna kurejesha furaha. Kiubinadamu mashabiki hao walitegemea ile hali ya kujiamini aliyokuwa nayo Gamondi ndiyo ilipaswa kuwafanya watembee kifua mbele. Kwa muda wote aliokuwa akifanya kazi nchini Tanzania Gamondi alionesha weledi na heshima yake kwa taaluma. Pengine uongozi wa Yanga uliona makosa kadhaa lakini walichukua uamuzi mzito kwenye jambo lilohitaji umakini na tafakari ya kina.
Mashabiki wa Yanga bado wanajiamini?
Sasa Yanga wapo kwenye mikono ya Sead Ramovic, je hali ya mashabiki wa Yanga kujiamini bado ingalipo? Kulijibu swali hili lazima tutumie takwimu sahihi. Chini ya Sead Ramovic Yanga wamecheza michezo mitatu ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika michezo hiyo Yanga wameambulia pointi moja pekee kwenye mchezo wao dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mchezo huo ulimalizika 1-1. Michezo mingine miwili iliyotangulia, dhidi ya Al Hilal ilishuhudiwa wakipigwa mabao 2-0 kwenye dimba la Benjamin Mkapa. Mchezo wa pili ulikuwa ugenini dhidi ya MC Alger ya Algeria ambao Yanga walikung’utwa na hivyo kupoteza michezo miwili. Katika amzingira hayo ziliibuka pande mbili.
Upande mmoja ulilalamika kwanini uongozi ulifanya haraka kumuondoa Miguel Gamondi, na mwingine ulikubaliana na uamuzi wa uongozi kwa kile walichokiita tangu msimu uanze timu haikuwa vizuri. Twende mbele sasa, Yanga wana maisha mengine chini ya Ramovic, je wanajiamini kama mwanzoni? Kwenye mechi za Ligi Kuu Ramovic anaweza kushinda mechi kadhaa kama ilivyokuwa kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons wikiendi hii ambako waliibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Je kwa ushindi huo mashabiki wa Yanga wanaweza kumwamini kocha huyo? Katika mazingira ya kawaida lazima Ramovic afanye kazi ya ziada kurejesha furaha ya wanaYanga. Hili linaweza kuwa jukumu jepesi kama watapata matokeo mazuri kiwanjani. Lakini je kocha mwenyewe anazungumza na mashabiki? Ana bondi nao kwa timu anayoiongoza? Jambo hili ni kazi ya mpira kuchezwa kiwanjani ukiwa na ushawishi.
Je Ramovic ni mahiri kiufundi?
Kwenye mechi tatu za Ligi ya Mabingwa hatujaona maajabu au ugwiji wowote kutoka kwa kocha huyo. Pengine ni sababu ya ugeni, timu mpya,fikra mpya,mbinu mpya na maizngira mapya hivyo inaweza kumchukua muda kuingiza mifumo yake ya uchezaji. Katika ufuindi alianza na kuwapanga mabeki wawili nyuma wakati wa kushambulia, kisha akaja na watatu na sasa annarudisha mabeki wanne kwenye kushambuliwa.
Katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons aliwajaribu mabeki watatu wa kucheza kwa wakati mmoja; alianza na Nickson Kibabage na Farid Mussa, kisha akamtoa Farid Mussa na kumwingiza Boka. Kwahiyo Kibabage akasogezwa mbele kama winga wa kushoto, huku nafasi ya beki wa kushoto ikienda kwa Boka. Wote hawa wana akili nzuri kushambulia. Bila shaka kocha huyu anajaribisha mbinu zake. Vilevile eneo la kushoto lilikuwa linatumiwa na Kibwana Shomari ambaye alikuwa na kazi ya kuziba nafasi pale Kibabage anaposhambulia. Kisha Kibabage anaporudi katika nafasi yake, Kibwana anaingia eneo la kiungo mkabaji kusaidia ulinzi kwa kuelekea kulia na katikati.
Jambo lingine analoliingiza ni mabadiliko ya wachezaji, amekifanya kikosi chake wachezaji karibu wote wapate nafasi ya kucheza ili kuonesha umahiri wao. Hii kwa lugha ya kisoka linaitwa ‘rotations’, kitu amabcho Miguel Gamondi alianza kukifanya kwenye mchezo dhidi ya Tabora United, lakini hakukuwa na utayari wala uwiano wa ubora kati ya kikosi cha kwanza na akiba.
Hapa tulipo, bado Ramovic iliteke mioyo ya mashabiki wa Yanga anatakiw akufanya kazi ya ziada. wanaYanga wammechizishwa na makocha wenye umahiri na wamefanya makubwa. Naye Ramovic afanye makubwa bila shaka ataaminiwa na mashabiki wengi. Sasa hivi wanamchekea tu kupoza machungu. Kila la heri.
Comments
Loading…