in

Jacob Mulee ataka athaminiwe kama makocha wazungu…….

Huku akiwa na nafasi ndogo ya kukubali kuja nchini kuwafundisha mabingwa watetezi wa mashindano ya Kombe la Kagame, timu ya Yanga, Mkenya, Jacob Mulee ‘Ghost’ amesema kuwa thamani yake ni zaidi ya makocha wa ‘Wazungu’ ambao klabu hiyo imekuwa ikiwafikiria kuwapa ajira ya kudumu.

Ghost ndiye kocha wa mwisho kuipeleka Kenya katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika Tunisia mwaka 2004 na mwaka 2008 akiwa jijini Dar es Salaam aliifunga Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame na kuchukua ubingwa uliokuwa unawaniwa pia na URA ya Uganda.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Ghost alisema kuwa kwa sasa ana shughuli nyingi anazozifanya na endapo atakubali kuifundisha Yanga ni lazima apate maslahi makubwa ambayo yatafanana na hadhi aliyokuwa nayo na si kama Yanga wanavyomfikiria.

Ghost alisema kuwa viongozi wa klabu za Afrika wamekuwa wakiwapa thamani zaidi makocha Wazungu na kuwaona wazalendo ni watu ‘rahisi’ na yeye kwake hilo haliamini kwa sababu anaifahamu vyema na anauzoefu na kazi ya ukocha.

“Kama nitakubali kima cha chini kitakuwa ni Dola za Marekani 10,000 (sawa na Sh. milioni 16 kwa mwezi) na pia nitataka kuhakikishiwa chanzo cha fedha au mtu ambaye atanilipa huo mshahara,” alisema kocha huyo.

Aliendelea kusema pia hawezi kamwe kukubali ‘ofa’ ya kuifundisha Yanga kwa muda wa wiki mbili na kuongeza kwamba muda huo kamwe hautaweza kuwa kipimo kizuri kwake cha kuipa Yanga matokeo mazuri na kwa sasa yeye ameshapita hatua hiyo.

“Nilikuwa nje ya jiji la Nairobi kutangaza mpira, leo (jana Jumapili) ndio nimerudi mjini na nitazungumza na washauri wangu kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho,” aliongeza Ghost ambaye pia anatangaza katika kituo cha redio cha Jambo FM.

Mwaka juzi Ghost alikuja nchini na timu ya Kenya (Harambee Stars) katika mashindano ya Kombe la Chalenji lakini aliamua kujiuzulu baada ya Chama cha Soka Kenya (KFF) kutowapa wachezaji posho na timu kutofanya maandalizi ya kutosha.

Kwa sasa Yanga iko chini ya Fred Minziro na tayari imeshaanza mazoezi kujiandaa kutetea ubingwa wake wa Kagame ambapo watashuka dimbani kuanzia Julai 14.
Imenakiriwa kutoka NIPASHE.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

England kwaheri….

Nation (Tanzania) Won’t Avoid Olympics