Baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika, Ivory Coast walipewa mapumziko ya siku moja kusherehekea ushindi wao.
Rais Alassane Ouatarra alitangaza mapumziko hayo Jumapili kwa ajili ya siku iliyofuata, yakienda sambamba na sherehe jijini Abidjan kuwapokea wachezaji sambamba na kufurahia ubingwa huo kwenye miji mingine, ikiwa umekuja baada ya miaka 22 ya ukame.
Ivory Coast walishinda kwa penati 9-8 katika mechi ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Jumapili usiku nchini Guinea ya Ikweta, baada ya kutoshana nguvu kwa suluhu na Ghana katika muda wa dakika 120.
Ushindi huo ni marejeo ya mwaka 1992, ambapo pia waliwafunga Ghana kwa penati baada ya kushindw akufungana kwenye muda wa kawaida. Mitaa mingi ya Ivory Coast ilifunikwa na shangwe kutoka kwa wananchi waliokuwa wakifuatilia kwenye vituo vya televisheni.
Baada ya wachezaji kuwasili nyumbani Jumatatu hii, walifanyiwa mapokezi rasmi kwenye Uwanja mkubwa uliopo Abidjan, wa Felix Houphouet-Boigny. Hata hivyo, redio zilikuwa zikitangaza baada ya wachezaji kuwasili, zikiwasihi washabiki wasiingie tena uwanjani humo, kwani ulishatosheleza nafasi za watu 35,000.
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetangaza kuwa kufanikisha mashindnao hayo ni kama muujiza, ikizingatiwa kwamba Morocco waliokuwa waandae michuano hiyo walijitoa dakika za mwisho kwa madai ya hofu ya maambukizi ya Ebola, kabla ya Guinea kujitolea kuandaa.
Katibu Mkuu wa CAF, Issa Hayatou, alisema kwake ni muujiza kufanikiwa mashindano hayo katika muda wa pungufu ya miezi miwili. Wametoa pongezi hizo licha ya vurugu zilizozuka mchezoni wakati wa nusu fainali baina ya Ghana na Guinea ya Ikweta, washabiki wa timu mwenyeji wakitaka upendeleo.
Comments
Loading…