in , , ,

Itazame miguu ya Che Malone Fondoh

Washabiki wa Simba wanamkumbuka vizuri sana Victor Costa  mwenye jina la utani la nyumba. Beki huyo alikuwa na uwezo wa kupiga chenga ndani ya boksi lake na kuwatoroka washambuliaji. Ulikuwa umahiri wa hali ya juu alipokuwa akicheza mpira. Kumtazama Victor Costa ilikuwa kama filamu kali ya kusisimua inayokuachia tabasamu. Tangu alipokuwa Mtibwa Sugar, Victor Costa alikuwa nyumba haswa. Alikuwa na utulivu wa akili,kujiamini na kupiga pasi za uhakika. Ni kipaji cha aina yake kutokea Tanzania. Wakati nakufikirisha kuhusu Victor Costa natamani uitazame miguu ya nyota mpya wa Simba na raia wa Cameroon, Che Malone Fondoh. 

NAMBA 20

Huyu ni mchezaji mpya kabisa anavaa jezi namba 20. Ni mchezaji ambaye anakwenda kucheza Ligi Kuu Tanzania kwa mara ya kwanza na hana uzoefu nayo. Lakini mechi mbili za Simba Day dhidi ya Power Dynamos ya Zambia na nusu fainali ya mashindano ya Ngao ya Hisani dhidi ya Singida Fountain Gate ameonesha sababu za kwanini uongozi wa Simba ulimsajili. Kwa haraka nyota huyo ana utulivu wa kutosha, anapiga pasi za uhakika, anajiamini,anakokota mpira vizuri na anaifanya Simba ijuvunie kumsajili.

CHE MALONE KAMA VICTOR COSTA

Tanzania Sports

Kitu kingine muhimu alichonacho Che Malone ni nguvu za mwili na maarifa yake. Ni vitu viwili ambavyo Victor Costa alikuwa mahiri, mtulivu na mwenye maarifa ya kutosha. Che Malone ameleta utulivu mkubwa kwenye safu ya ulinzi. Amekuwa mtulivu katika mechi zote mbili, na kila anapotiwa presha na wapinzani wake haonekani kuwa na papara. Kwa mfano katika mchezo dhidi ya Power Dynamos, TANZANIASPORTS inazo takwimu zake kuwa alipiga pasi takribani 50 za uhakika. Huu ni umahiri wa aina yake kwa beki wa kati. Katika mchezo wao dhidi ya Singida Fountain Gate alikuwa anaamba mbaa eneo lote la ulinzi. Alikwenda kusahihisha makosa ya Mohammed Hussein upande wa kushoto na kudhibiti kashikashi. Huyu ni beki mwenye sifa kubwa ya kutulia.

SIMBA WAMETIBU UGONJWA

Kwa miaka mitano mfululizo Simba wamekuwa wakifungwa mabao ya faulo. Kumekuwa na changamoto ya kukabiliana na mashambuluizi ya mipira ya juu. Hii ina maana mgawanyo wa majukumu wa kuondoa hatari zote za hewani na chini haukuwa sawia. Lakini sasa Che Malone Fondoh anaonekana kutibu ugonjwa huu. Ni mrefu kwa kimo, anapambana kimabavu na wapinzani. Anaruka na kuokoa hatari za hewani, eneo ambalo Simba imekuwa ikitatizwa mno kwenye mashindano ya kimataifa. Usajili wa Che Malone unawapa heko viongozi wa Simba kwani unaonekana kuwa msaada mkubwa kwenye mashindano ya kimataifa ikizingatiwa inakabiliwa na African Super League, Ligi Kuu, Kombe la ASFC.

MIGUU IMARA NA KUJIAMINI

Uwezo wa kutuliza mipira, kutoa pasi na kusafisha hatari kwa umakini ni vitu vichache vilivyoonekana. Ukitazama uchezaji wake utaona Che Malone anajiamini mno, nap engine wahenga wangempa angalizo kwa kujiamini kupita kiasi. Ni nyota ambaye anajua hafahamiki udhaifu wake uko wapi, lakini kwa haraka huenda ikamuwia vigumu kukabiliana na wachezaji wenye kasi kuliko yeye. 

Hata hivyo Ligi Kuu Tanzania haina wachezaji wa aina hiyo, labda Peter Banda angelikuwa kwenye kiwango bora ni mojawapo wa wachezaji wenye mbio nyingi na uwezo wa kukaa na mpira mguuni. Che Malone ni beki wa nguvu, anaweza kucheza kwenye mifumo tofauti kadiri mwalimu anavyoamua, lakini anakabiliwa na kujiamini kupita kiasi. Huenda hilo hata benchi la ufundi wameliona, kwani litamsaidia kuondoa makosa madogo kutokea siku zijazo.

LIGI KUU

Kwa mara nyingine tena Ligi Kuu Tanzania inatangazika kwa kusajili wachezaji kutoka mataifa mengine kwa vile kuna fursa nyingi za kushiriki mashindano ya kimataifa. Kwa msingi huo wachezaji watazidi kumiminika wenyewe kuomba kusajiliwa kwa kufanyiwa majaribio. Ni dhahiri Cameroon italifuatilia soka la Tanzania. Halafu timu ya Tanzania ipo African Super League.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Yanga bila Mayele, Azam bila mipango, refa na kigugumizi

Tanzania Sports

Simba kuna vita kali, msimu utawaka moto