in , , , ,

Heka heka za msimu mpya nani atakuwa bingwa?

*PRIMERA LA LIGA
*PREMIER LEAGUE
*BUNDESLIGA

Unaanza kufikiria Ligi Kuu England. Unageukia La Liga kule Hispania. Unachungulia Bundesliga. Hujasahau kutazama Serie, Ligue 1 au Ligi ya Mabingwa Afrika na Ulaya.

Michuano ya Kombe la Dunia imemalizaika kilichobaki sasa ni kuangalia ustaarabu mwingine katika ligi mbalimbali barani Ulaya. Tukija Afrika tunafahamu mbio za Ligi ya Mabingwa zimeshika kasi, pamoja na kombe la Caf na kadhalika.

Ukanda wa Afrika Mashariki kuna michuano ya Chalenji na CECAFA/Kagame. Kuna michuano mingine ya Madola na maandalizi ya Olimpiki mwaka 2016 si mbali sana.

PRIMERA LA LIGA

Ligi kuu nchini Hispania imepokea wageni wapya. Mgeni mmoja ni mashuhuri sana duniani, Luis Saurez aliyejiunga na Barcelona. Real Madrid wao wamemchukua Keylor Navas kutoka Levante, pamoja na matarjio yaw engine kutangazwa kwa usajili wa Toni Kroos kutoka Bayern Munich.

Vilevile Atletico Madrid imeondokewa na staa wake Diego Costa pamoja na Tiago Mendes na Felipe Luis anafuata njia. Mikakati ya kila timu inazungumzwa, lakini swali nani atakuwa bingwa wa Ligi Kuu Hispania msimu ujao?

Hiki ni kitendawili kitakachoteguliwa mwezi Mei. Atletico Madrid itatetea ubingwa wake? Vipi Real Madrid ambayo itakuwa na mikakati miwili, kutwaa La Liga na kutetea Ligi ya Mabingwa ambapo tayari mipango ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya 11 imepangwa. Mashabiki wa Real Madrid wamepiga kura, wanataka Angel Di Maria abakie klabuni, lakini Sami Khedira auzwe tu.

Luis Enrique anachukua jukumu la kuinoa Barcelona, na tayari ameruhusu kuondoka kwa Cesc Fabregas. Mashabiki wanasubiri kocha huyo ataleta kitu gani katika klabu yao. Je atakuwa bora kama alivyokuwa kwa mchezaji mwenzake Pep Guardiola? Tusubiri.

PREMIER LEAGUE
20140512-104224.jpg

England kuna mbio za kasi sana. Liverpool imekuwa ikisuka kikosi chake. Moja ya mambo yaliyokuwa yakimwangusha Brendan Rodgers ni namna ya kutumia kikosi kamili, badala yake akajikuta amebakiwa na wachezaji wa kawaida.

Mauzo ya Luis Suarez yanaonekana kuimarisha Liverpool, ingawa bado anahitaji mshambuliaji kamili kumsaidia Daniel Sturridge. Ndiyo, kuna Rickie Lambert, ambaye naamini bado hatoshi.

Kuna viungo na winga, Lazar Markovic na Adam Lallana wataongeza kitu. Kiungo mkabaji bado kinahitaji uimarishwa. Arsenal wamemchukua Alexis Sanchez na wanaendelea kuimarisha kikosi chao.

Ununuzi wa Arsenal utakwua bure kabisa kama hakutakuwa na kiungo mkabaji. Arsene Wenger hana kiungo mkabaji imara zaidi ya Mathew Flamini. Wengi anaowatumia analazimisha tu.

Manchester United wana nguvu ya kocha mpya Louis van Gaal, lakini kuna kazi ya kufanya kwakuwa timu nzima itafumuliwa na kocha huyo mdachi. Chelsea hakuna habari mpya sana, lakini Jose Mourinho hatakubali kukosa ubingwa msimu ujao.

Hapo ndipo ushindani utakapoanza kushika kasi. Kwa vyovyote Mourinho anataka taji moja kati ya manne msimu ujao. Man City wanaendelea kuimarisha timu yao, lakini wasiwasi wangu ni kwamba wachezaji watakuwa wamechoka ifikapo katikati ya msimu. Wachezi muhimu wameshiriki fainali za Kombe la dunia.

BUNDESLIGA

Pep Guardiola ana kazi moja kubwa sana, kutetea ubingwa wake. Msimu uliopita alipata ubingwa mwezi machi, ikiwa ni mapema sana. Lakini inatarajiwa msimu ujao atapata changamoto na swali linalobaki ni namna gani ataweza kutetea ubingwa wake. Kwa vyovyote mashabiki wanangojea kuona nini kitatokea.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Rais Argentina hapendi soka

England yaporomokea nafasi ya 20