WIGO wa timu ya Tanzania itakayoshiriki michezo ya Olimpiki ya Beijing imeongezeka baada ya Chama cha Kuogelea Tanzania, TSA kupata nafasi ya upendeleo ya kushiriki michezo hiyo kwa wanamichezo wake.
Akizungumza na Mwananchi jana, Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, TOC, Filbert Bayi alisema mchezo wa kuogelea umeongezwa katika mashindano ya Olimpiki kutokana na wanamichezo wake kufanya vizuri michezo ya dunia huko Manchester, Uingereza.
”Wanamichezo wetu walikwenda Manchester na wamefanya vizuri na sasa wanakwenda Beijing kwenye Michezo ya Olimpiki,” alisema Bayi.
Alisema: ”Hayo ni mashindano makubwa sana na ya kimataifa ambayo yalishirikisha nchi mbalimbali zaidi ya 60 zinashiriki hivyo ni nafasi ya kipekee kwa Tanzania kuweza kujifunza mengi na mapya katika michezo hiyo,” alisema.
Bayi alisema kwa sasa vyama hivyo vipo katika maandalizi mazuri na wanaendelea kuwasiliana na vyama hivyo ili kuandaa washiriki waweze kujiandaa vizuri na mapema ikiwa ni moja ya kuendeleza michezo nchini na kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi.
Tanzania ilikuwa iwakilishwe na ngumi na riadha pekee kwenye michezo hiyo iliyopangwa kuwanza Agosti 8 hadi 24.
Comments
Loading…