in , ,

Hatima ya Michael Wambura kujulikana leo..

HATMA ya aliyekuwa ya mgombea wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Simba, Michael Wambura, ambaye alienguliwa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa klabu hiyo inatarajiwa kujulikana leo Jumatatu.

Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Nchini (TFF) inakutana leo kujadili rufaa iliyowasilishwa na Wambura akipinga kuenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba.
Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa kikao cha kamati hiyo inayoongozwa na Wakili, Julius Lugaziya, itakutana leo kuanzia saa 5 asubuhi kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanga, jijini Dar es Salaam.

Mbali na rufaa hiyo ya Wambura, pia jana aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ aliwasilisha rufaa yake TFF dhidi ya viongozi wanaomaliza muda wao na sasa wanawania tena nafasi za uongozi katika uchaguzi huo unaokuja.

Julio amewakatia rufaa Swedy Mkwabi, anayegombea cheo cha Makamu wa Rais, Daniel Manembe, Said Pamba na Ibrahim Masoud ‘Maestro’ wanaowanania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Beki huyo wa zamani wa Simba ambaye naye anawania nafasi ya Makamu wa Rais amewakatia rufaa wagombea hao akieleza kuwa walishiriki katika kikao cha ‘kumpindua’ madarakani Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage.

Julio ameeleza kwamba kitendo hiko kilichofanywa na wajumbe wa Kamati ya Simba kinaenda kinyume na katiba na ndio maana TFF ilitengua maamuzi ya kumsimamisha Rage ambayo yalifanywa na viongozi hao pamoja na wenzao ambao hawajatetea nafasi zao.

Wambura alienguliwa katika uchaguzi huo baada ya kuonekana alisimamishwa uanachama tangu Mei 5 mwaka 2010 kutokana na kufungua kesi kuishitaki Simba.
Na katika kuthibitisha uanachama wake una ‘walakini’ Wambura aliwasilisha barua zakujitetea kwa Kamati ya Uchaguzi zikiwa zinajichanganya na moja ya barua hizo ambayo iliandikwa Septemba 25 mwaka 2012 inadaiwa kuwa ni ya kughushi kutokana na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wekundu wa Msimbazi, Evodius Mtawala, kuikana barua hiyo.

Pia mwanachama wa klabu hiyo, Jackson Sagonge ‘Chacha’ aliliambia gazeti hili kwamba alipeleka malalamiko yake katika Kamati ya Maadili akieleza kuwa mgombea huyo hapaswi kurejeshwa kwa sababu hana maadili ya kuiongoza Simba.
Naye Wambura alisema mwishoni mwa wiki kwamba aliwasiliana malalamiko yake katika kamati hiyo akieleza kwamba ametukanwa na Ndumbaro.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Azim awapasha TFF

Wadhamini waikalia kooni Fifa