HAKUNA ubishi timu nyingi za Ligi Kuu zinaonesha mchezo mzuri kila zinapocheza. Jumapili hii Yanga walikuwa wenyeji wa Fountain Gate. Katika timu 16 za Ligi Kuu zote kwa namna fulani zinajaribu kuonesha mabaidliko ya kiufundi na kubeba hadhi ya ubora wa Ligi.
TANZANIASPORTS ilikuwa inashuhudia mchezo wa kukata shoka kati ya Fountaine Gate na bingwa mtetezi Yanga. Mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 5-0. Ni ushindi mnono lakini Fountain Gates iliwaletea washabiki kitu kizuri sana ambacho kinakuwa kielelezo cha ubora wa Ligi Kuu. Je ni mambo gani ambayo klabu hiyo imejaribu kuyafanya kwenye mchezo wake dhidi ya Yanga licha ya kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao.
Je Fountain walitumia mfumo gani dhidi ya Yanga?
Fountain Gate walicheza katika mfumo wa kujilinda ambapo sehemu kubwa ya wachezaji wake walikuwa wanazuia mianya ambayo ingesababisha wafungwe mabao zaidi. Kwahiyo kufungwa mabao matano na wao kushindwa kufumania nyavu ni dhahiri wamejatihadi katika mkakati wao. Wanapokuwa na mpira wanachezaji na mabeki watatu nyuma ambapo mbele yao kunakuwa na viungo watatu wanaofanya jumla ya kuwa na wachezaji 6.
Eneo katikati au kwenye mstari wa uwanja wa katikati kulikuwa na wachezaji wawili ambao wanakamilisha jumla ya 8. Wachezaji wawili walikaa nyuma pembeni na kuliacha eneo la kiungo likiwa linawaathiri mara kwa mara. Kwa maana Fountain walitumia mfumo 3-3-1-2-1. Wachezaji wawili wa mbele walikuwa na jukumu la kujihami kuanzia mstari wa katikati, huku wawili wa nyuma yao wakiwa wanaelekea pembeni kushoto na kulia kuwazuia mabeki wa pembeni wa Yanga.
Pia wachezaji watatu walicheza kwenye duara mita chache kutoka katikati ya dimba. Hawa watatu ndiyo walikuwa na kazi ya kupambana na viungo wa Yanga pamoja na kudhibiti wapishi wa mabao yao. hata hivyo juhudi zao hazikuleta mafanikio kwa asilimia 100 kwnai walijikuta wakipoteza mipira mingi katika eneo la katikati. Mipango yao ilifia miguu mwa watatu hao ambao ni mara chache walifanikiwa kuvuka kuelekea lango ya Yanga.
Kiufundi kuwapanga wachezaji watatu eneo la kiungo, kisha wawili kuwapeleka kulia na kushoto kulikuwa na maana eneo la kiungo mshambuliaji lilikuwa wazi, kwani washambuliaji wawili waliokuwa mbele na ambao waliunda mfumo wa 4-3-2-1 pale walipojaribu kushambulia walijikuta wakirudishwa nyuma mara kwa mara kwani mpira haukuwa upande wao. Katika mpangilio wa kiufundi hawakuwa wabaya kutumikia mfumo.
Je, umahiri wa Fountain Gate upo eneo gani?
Kila timu inapofungwa ina sababu zake. Kila timu inaposhinda inakuwa na sababu zake. Lakini kila timu inapofungwa kunakuwa na mambo mazuri yanayoangaliwa. Hali kadhalika timu inaposhinda unaangaliwa umahiri wake, na kidogo udhaifu walionao. Fountain Gate katika dakika 65 hadi 67 walikuwa wamepiga basi 21 mtawalia. Pasi hizo zilipigwa katika eneo lao kutoka nyuma hadi katikati ya uwanja. Upigaji wa pasi ulikuwa ni kuunda mtiririko au mpango wa kusaka bao kuelekea lango la aduni. Ni kiwnago cha juu cha timu kupiga pasi mfululizo katika mchezo huo.
Hata hivyo uwezo huo uliishia katika eneo lao pekee, kulia na kushoto na katikati kwa viungo. Kwa maana hiyo msingi wa kwanza wa Fountain Gate ulikuwa kujihami na kupunguza kasi ya Yanga. Walitaka kucheza kama Barcelona lakini walikumbana na timu ambayo inasaka ushindi kwa udi na uvumba tena ikicheza bila hata kujali uundaji wa mashambuliazi ya mabao.
Kutoka katikati ya dimba (mstari wa katikati0 kuelekea kwenye eneo la 18 la Yanga, Fountain walifanikiwa kupigiana pasi 6 mtawalia. Zaidi ya hapo hawakuwa na uwezo wa kupiga pasi nyingi kila wlaipovuka eneo lao kwenda langoni mwa Yanga. Ni sahihi kusema uwezo wao wa kupiga pasi nyingi ulikuwa kwenye eneo lao, lakini upande wa adui wlaiishia pasi chiniya 6 kabla hawajanyang’anywa na Yanga.
Je ni jambo gani linalovutia Fountain Gate?
Hii ni timu ambayo unaona wazi inafundishwa mpira. Wachezaji wanafundiwa kujiamini. Wanapokea pasi na kutengeneza nafasi zaidi za kupewa pasi. Wanafungua uwanja, wanafuata mpira na kutaka kuwapeleka wengine. Eneo lililowagharimu ni kiungo. Viungo wa Fountain kila waliposogea eneo lao la 18 kupokea basi walijikuta wamezizingirwa na viungo wa Yanga. Laiti wangekuwa wanacheza na timu nyingine basi uwezo wa kuwafunga ungeonekana.
Timu hii inacheza na kupanga mipango kuanzia nyuma, ni mchezo wa Kiulaya ulaya na kuonesha kuwa mechi zinazooneshwa zinawavutia wengine nje ya mipaka. Mbali ya kujiamini, timu hii inapenda kucheza kwa uhuru. Yaani Fountain wanataka mpira uchezwe wanavyotaka wao, wapewe pasi kisha watulie, watoa pasi, waachie njia ya kwenda iwe pembeni kushoto au kulia. Uhuru ndicho wlaichokitaka, lakini hawakukipata kwa Yanga.
Je ubora wa uwanja una nafasi gani?
Kucheza kama Founatin Gate unatakiwa kuwa kwenye kiwnaja kizuri. Kiuchezaji Fountain walionekana kuburudika kutumia uwnaja wa KMC Complex kwani uliwafanya watandaze soka maridadi lakini hawakuwa na uwezo wa kuwashinda Yanga ambao wlaitibua mipango kwa kuwapangia wachezaji 6 katikati ya kiwanja kuelekea langoni mwa Fountain. Uwanja wa KMC Complex ni mzuri na unawapa uhuru wachezaji kucheza kwa utulivu.
Udhaifu wa Fountain, kutimuliwa kocha wao
Hakuna ubishi makosa binafsi ya wachezaji yamewagharimu. Makosa hayo ni pamoja na ukosefu wa umakini, kushindwa kuendana na kasi ya Yanga pale walipopokonywa mpira. Pia timu hiyo ilikosa uimara katika eneo la kiungo kwani liliwapa uhuru mno Yanga kwa vile mpango wa Fountain ulikuwa kuwazuia mabeki wa pembeni wa Yanga. Kosa lingine ni kushindwa kugundua mianya inayowapa Yanga kupata mabao, na hivyo kujikuta wakibanduliwa mabao matano kwa nunge. yote kwa yote ni miongoni mwa timu za kufurahisha katika Ligi Kuu. Huenda ikawa sababu hiyo ndiyo imechangia benchi la ufundi la klabu ya Fountain Gate lililokuwa chini ya Kocha Mohammed Muya kuvunjwa na kuanza msako wa kocha mpya. Hata angekuwa kocha gani lazima angejipanga kuzuia zaidi dhidi ya Yanga hii na Fountain wamejitahidi kuunda timu nzuri. Kila la heri Mohammed Muya na wasaidizi wake huko waendako
Comments
Loading…