Menu
in , , ,

FERNANDEZ NA MTIHANI KUDUMU SIMBA

MSIMU wa Ligi unapomalizika, kinachofuta ni mjadala kuhusu nafasi mbalimbali za wachezaji kwenye vikosi vya timu zao. Kila kitu inafanya tathimini kuhusu ushiriki wa Kila mchezaji. Kila kocha anakuwa na mapenzekezo mbalimbali ya kuimarisha timu yake. Pia uongozi unakuwa na tathimini yao ambayo wanaitumia kulinganisha na kile ambacho benchi la Ufundi inapendekeza. 

Kwa mfano Simba, Yanga na Azam ndizo timu zenye mvuto katika usajili. Ni timu ambazo zinahitaji wachezaji waliokamalika na ndio maana baadhi ya chipukizi hawafui dafu kikosini kwa Sababu mbalimbali. 

Benchi Ufundi linapotoa mapendekezo, mara nyingi kunakuwa na wachezaji ambao wanaathirika moja Kwa moja. 

Ligi Kuu imeshuhudia nyota mbalimbali waliotokea nje ya nchi wakishindwa kufurukuta licha ya kusifiwa mno. Sababu za kushindwa kufurukuta zinaweza kusababishwa na mchezaji mwenyewe ikiwa ni mvivu, mabadiliko ya kinbinu ya kocha, ushindani wa namba katika kikosi cha kwanza na mazingira mageni Kwa mchezaji. Katika mukutadha huo, wapo wachezaji ambao wanakabiliwa na wakati mgumu pale kocha anapovutiwa na utendaji wa kazi wa wengine na kusababisha mwingine kusugua benchi. 

Tanzania Sports

Augustine Okrah hakuwa mchezaji mbaya lakini kwenye kikosi cha Yanga kulikuwa na wachezaji wenye kiwango kikubwa kumzidi nyota huyo. Vilevile kwa muundo wa timu ya Yanga kwa miaka ya karibuni mawinga asilia wamekuwa wakipata shida kutoboa kikosini hasa namna makocha wanavyotumia viungo wao wengine kuziba nafasi zao. 

Katika mazingira hayo, Okrah ni mwathirika wa mbinu za Kocha kama ilivyo Kwa Dennis Nkane wa Yanga ambaye anakabiliwa na changamoto mbili; mfumo wa kocha na ushindani wa namba kikosini. 

Katika mukutadha huo jina la Deborah Fernandez wa Simba ni miongoni mwa nyota walioathiriwa na mambo makuu matatu; ushindani wa namba, mabadiliko ya kimbinu na uimara wa mchezaji mwenyewe Kwa maana ya kutoelemewa na majeraha. 

Fernandez ni kiungo mshambuliaji ambaye nafasi yake inawindwa na wachezaji wengi kikosini. Ni nyota ambaye alianza vyema Kwenye mechi za Simba za kirafiki pamoja na Ligi Kuu na Mashindano ya Kimataifa hatua za awali. 

Lakini kadiri ulivyokuwa unakwenda Deborah Fernandez alianza kuwa mchezaji wa akiba alichukua nafasi za viungo kama vile Jean Ahoua, Fabrice Ngoma au Yusuf Kagoma. 

Fernandez alikuwa akicheza Kwa madaha, uwezo Mkubwa, mashuti makali, chenga na mchezaji ambaye alisaidia ulinzi. 

Timu inahitaji huduma ya wachezaji wote kwenye kikosi chao. Mechi za Ligi Kuu, mashindano ya Kombe la Shirikisho pamoja na Kombe la CRDB ni miongoni mwa mechi ambazo zinahitaji mabadiliko ya mara kwa mara ili kuwapumzisha baadhi ya wachezaji na kuwapa nafasi wengine. Kwahiyo kocha Fadlu Davids alihitaji wachezaji wote wawe imara na wajue kutimia nafasi wanazopewa kucheza na kutekeleza majukumu yao. 

Fernandez hakutolewa kikosi cha kwanza Kwa sababu ya kukosa uwezo bali kushindwa mbele ya wachezaji waliomzidi uwezo pamoja na mbinu za Mwalimu. Hakuwa Fernandez peke yake, hata Mzamiru Yassin ni mmoja wa wachezaji ambao wamepoteza namba katika kikosi cha kwanza. 

Huwezi kumpanga Mzamiru Yassin ikiwa Yusuf Kagoma ana afya njema. Huwezi kumpanga Fernandez ikiwa Fabrice Ngoma na Jean Ahoua wapo imara kiafya.

Suala lingine ni uwajibikaji kiwanjani. Fernandez alipoteza namba sababu ya kuzidiwa kilometa za kukimbizana na wapinzani ndani ya kiwanja pamoja na kwenda maili za ziada zenye matokeo kwa timu. 

Kwanini? 

Jean Ahoua alikuwa anaweza kucheza namba kumi na 8 katika nyakati tofauti. Nafasi yake aliitendea haki Kwa kupachika mabao muhimu Kwa timu yake ikiwemo la nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Stellenbosch ya Afrika kusini. 

Hii Ina maana Fadlu Davids alihitaji mchezaji ambaye atakuwa karibu na Jean Ahoua ili aweze kusogea langoni mwa adui. Jean Ahoua alikuwa na bahati ya kulindwa na Yusuf Kagoma na Fabrice Ngoma hali ambayo ilimfanya awe mchezaji wa kiungo anayewasumbua wapinzani. 

Makosa ambayo wapinzani wa Simba walifanya ni kutaka kumdhibiti Jean Ahoua badala ya kuziba vyanzo vya usumbufu wake yaani viungo Ngoma na Kagoma. Kwa maana hiyo Jean Ahoua alimlazimisha Kocha Fadlu Davids kuunda timu inayomzunguka yeye. 

Jean Ahoua alipachika mabao, alotengeneza mabao, alisababisha hatari nyingi langoni mwa adui Kwa sababu alikuwa na uwezo huo huku akilindwa na viungo wawili Kagoma na Ngoma. 

Katika mazingira hayo Mwalimu wa Simba alihitaji huduma ya Jean Ahoua kuliko ya Debora Fernandez. Huo ukawa mwanzao wa kupotea Kwa kiungo mshambuliaji Deborah Fernandez. 

Timu haikumzunguka yeye, Wala haikujengwa kumzunguka yeye. Badala ya ilijengwa kumzunguka Jean Ahoua ambaye alikuwa anatoa huduma nzuri katika safu ya ushambuliaji na kupachika mabao au kusababisha hatari mara nyingi katika lango la adui. 

Kwa maana hiyo wakati msimu umemalizika, Deborah Fernandez ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatakiwa kuwa na wasiwasi. Mchezaji ambaye anatakiwa kuitisha kikao na kocha wake Fadlu Davids ili kufahamu mwelekeo wa kimbinu msimu ujao. Fernandez anatakiwa kuomba kikao hicho ili kumwezesha kujua mahitaji ya kocha wake msimu ujao, kuanzia mifumo ya uchezaji wa timu na mahitaji ya mchezaji mmoja mmoja.

Vilevile anahitaji kikao na uongozi wa Simba juu ya hatima yake kikosini hapo.

Hata hivyo ikishindikana kumbakiza kikosini hapo,huyu ni mchezaji ambaye anaweza kupelekwa kwa Mkopo timu nyingine ili aangaliwe Kwa jicho la mwisho ikiwa atahimiri ushindani katika timu hiyo.

Uongozi unatakiwa kuchagua ili kumlinda nyota wao wa kigeni ama kumuuza kwenda nje ama kwao. Lakini si mchezaji mbaya ambaye unaweza kumwachia kirahisi bali rundo la vipaji Simba na mfumo vinamnyima nafasi ya mara kwa mara.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version