in , , ,

Ferguson: Manchester tuna bahati

*United watesa kwa tofauti ya pointi saba

*Wigan, Aston Villa na QPR zalilia mkiani

Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson amekiri kwamba timu yake ina bahati ya kupata ushindi dhidi ya Southampton.

Akizungumza baada United kukomboa bao moja kwa Southampton katika dimba la Old Trafford na kuongeza la ushindi, Ferguson alisema uwanja nao haukuwa mzuri.

Man U sasa wamefanikiwa kung’ang’ania kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL), wakiongoza kwa tofauti ya pointi saba.

Katika mzunguko wa 24, United wamefikisha pointi 59, baada ya Wayne Rooney kurejea kwenye ufumaniaji nyavu, katika mechi hiyo akifunga mara mbili.

United wanafuatiwa na jirani zao, Manchester City wenye pointi 52 ambao walitoka suluhu na Queen Park Rangers (QPR) kwenye mzunguko huo.

Chelsea walioachia faida ya mabao 2-0 waliyokuwa wakiongoza dhidi ya Reading katika dakika nne za mwisho hadi kukubali sare, wanashika nafasi ya tatu kwa pointi 46.

Tottenham Hotspurs nao walivutwa shati Carrow Road nyumbani kwa Norwich kwa sare ya bao 1-1, bado hawajaachia nafasi ya nne waliyoshika kwa muda, wakiwa wamefikisha pointi 42.

Everton walifanikiwa kuwafunga West Bromwich Albion mabao 2-1 na kubaki katika nafasi yao ya tano.

Arsenal walianzishwa mchakamchaka na Liverpool Emirates na kubaki nyuma kwa mabao 2-0, lakini walicharuka kipindi cha pili na kusawazisha mabao hayo kupitia kwa Olivier Giroud na Theo Walcott.

Magoli ya Liverpool yalitiwa kimiani na Luis Suarez na Jordan Henderson. Arsenal wamejikusanyia pointi 38.

Katika michezo mingine ya mzunguko huo, Fulham waliwatandika West Ham United 3-1 na Newcastle United wakawafunga Aston Villa 2-1.

Sunderland walitoka suluhu na Swansea City wakati Stoke City wakitoshana nguvu na Wigan Athletic kwa kufungana mabao 2-2.

Reading wameweza kujinasua kwenye eneo la kushuka daraja, walau kwa sasa, kwani wanashika nafasi ya nne kutoka mkiani na jirani zao Southampton wanashika ya tano kutoka chini kadhalika.

Timu tatu zilizo hatarini ni QPR waliodumu kwa muda mrefu hapo, ambapo sasa wamefikisha pointi 16; Aston Villa na Wigan – wote wakiwa na pointi 20 sawa.

Pointi hizo ni sawa na walizo nazo Reading, lakini vijana wa Madjeski wamejing’atua humo kwa sababu ya uwiano mzuri wa mabao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Dua la Togo lafika

Hispania: Soka yapoza madhila ya uchumi