Sergio Ramos si mchezaji wa Real Madrid tena. Baada ya miaka 16 kucheza katika klabu hiyo, muda wake umefika mwisho baada ya kutangazwa rasmi kuwa mkataba wake umefika ukingoni. Ramos alikuwa kwneye majadiliano ya muda mrefu na Real Madrid juu ya mkataba wa kuchezea klabu hiyo.
Real Madrid confirm Sergio Ramos departure after 16 years at Santiago Bernabeu
Pande zote mbili zilikuwa zimegoma kukubaliana. Rais wa Real Madrid Florentino Perez hakukubaliana na matakwa ya nahodha wake wa zamani wa kutaka mkataba wa miaka miwili bila kupunguzwa mshahara. Real Madrid ilitaka Ramos akubali mkatba wa mwaka mmoja na mshahara wake kupunguzwa kwa asilimia 10.
Mwenzake Luka Modric alikubali kupunguzwa mshahara na kusaini mkataba wa mwaka mmoja. Wakati majadiliano yakiwa hayajafikiwa, Ramos alikuwa alikuwa akisubiri amabdiliko katika maombi yake. lakini baada ya muda kupita bila kukubali ofay a Real Madrid rais wa timu hiyo anadaiwa kuweka tarehe ya mwisho kwa nyiota huyo kwa kukubali au kukataa.
Wakati Ramos alipoamua kupitisha uamuzi wa klukubali mkataba wa mwaka mmoja, alikwenda kuiambia klabu juu ya uamuzi huo. Hata hivyo Real Madrid ilimjibu kuwa muda uliowekwa umeshapita na sasa hakukuwa na ofa nyingine ya aina yoyote.
Kwa mujibu wa mahojiano ya Ramos na vyombo vya habari vya Hispania, amebainisha kuwa jambo hilo lilimshangaza kwasababu hakuna aliyeona wala kugundua kuwa litatokea. Ikabidi akubali kushindwa na kuaga klabuni hapo akiwa mpweke bila nyota wenzake wala mashabiki kutokana na Ligi kumalizika. Sasa Real Madrid haina naodha mkuu, wamebaki Karim Benzema,Marcelo na Raphael Varane kama wasaidizi.
Tanzaniasports inafanya tathmini juu ya kuondoka kwa Sergio Ramos na faida na hasara zake. Kwamba kocha mpya Carlo Anelotti ataanza kibarua cha kuiandaa timu hiyo kwaajili ya msimu ujao bila Ramos.
FAIDA
Mosi, kuondoka kwa Ramos ni faida kwa wachezaji wengine kupata nafasi ya kucheza katika safu ya ulinzi. Kwa mfano wachezaji Nacho Hernandez na Eder Militao walicheza vizuri katika mechi kadhaa msimu uliopita ambao Ramos alikuwa majeruhi kwa muda mrefu. Ushirikiano wao katika safu ya ulinzi ulionesha katika mechi mbalimbali ngumu na rahisi, lakini walikuwa moto wa kuotea mbali katika mchezo war obo fainali dhidi ya Liverpool.
Vilevile David Alaba amewasili klabuni hapo, kwahiyo naye anakwenda kufaidika. Raphael Varane haijulikani msimu ujao atakuwepo Real Madrid au ataondoka, lakini Mfaransa huyo anatarajiwa kunufaika na kuondoka kwa Ramos kwa sababu atakuwa kiongozi katika safu ya ulinzi akiwa na uzoefu.
Pili, kupunguza gharama za mshahara mkubwa. Real Madrid imekabaliwa na wakati mgumu kiuchumi kutokana na ugonjwa corona. Wachezaji wamekuwa wakiombwa kupunguzwa asilimia kumi katika mishahara ya ikiwa na lengo la kupunguza gharama nyinginezo ikiwemo uendeshaji.
Hata hivyo kuondoka Sergio Ramos kunaipa nafasi timu hiyo kutumia fedha zilizopangwa kutumika kama mshahara ili kufanya shughuli zingine. Hilo lina maana mwenye mshahara mkubwa kwa sasa ni Gareth Bale ambaye bado hatima yake haijulikani kama atabaki au ataondoka klabuni. Perez ana mikakati ya kukusanya fedha ili kumnunua Kylina Mbappe hivyo bila shaka ameanza kupunguza ghamara klabuni kwa kuruhusu Ramos aondoke.
Tatu, nahodha mpya. Baada ya miaka 6 ya unahodha wa Sergio Ramos, Real Madrid inaelekea upande mwingine na mchezaji mwingine atakabidhiwa jukumu la kuongoza wachezaji wenzake ndani nan je ya kiwnaja.
Ni uamuzi ambao umepitishwa kuwa ni wakati wa klabu kuwa na nahodha mpya, ambapo kwa mtiririko cheo hicho kinakwenda kwa Marcelo, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake. Wachezaji wanadhaniwa kuteuliwa unahodha wa Real Madrid ni Toni Kroos, Casemiro,Luka Modric na Thibaut Courtois.
Nne, kuondokana na shinikizo. Kwa miaka kadhaa kumekuwa na mjadala kuhusu mkataba wa Ramos. Kulikuwa na presha aya aina fulani ndani nan je ya klabu kuanzia juu kwa Rais Perez hadi kocha Zinedine Zidane na Ramos mwenyewe. Kwa sasa presha hiyo imeondolewa.
HASARA
Mosi, kupoteza kiongozi wa timu. Hakuna mchezaji aliyekuwa anaifahamu Real Madrid kama Sergio Ramos. Amekuwa nahodha kwa miaka 6, lakini amekaa klabuni hapo kwa miaka 16. Yaani miaka 10 akiwa mchezaji tu bila unahodha, amewaona manahodha wenzake Iker Cassilas na Fernando Hiero. Katika uchezaji Ramos ametoa uwezo wake wote kwa asilimia 100 hilo halina ubishi. Marco Asensio amekiri Real Madrid imepoteza kiongozi wake ndani ya uwanja na maisha ya kila siku klabuni hapo.
Pili, mshindani asiyekubali kushindwa. Bao alilofnga jijini Lisobon katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid katika dakika ya 94 linakumbukwa zaidi kwani ndilo lililoirudisha timu hiyo mchezoni na baadaye kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 na kutwaa taji La Decima. Ramos anasifika kwa kuzuia kuzungumzia misimu mibaya ya Real Madrid, hata kama timu ikifungwa na kuonesha kushindwa lakini yeye alikuwa na kauli za kutaka kusonga mbele na timu itafanya kila kinachowezekana kushinda.
Tatu, mabao machache. Mbali ya tabia zake za ushindani Ramos amefunga mabao mengi. Licha ya kucheza nafasi ya beki wa kati Ramos kwa kipindi cha miaka 16 ameifungia Real Madrid mabao 101. Ni mchezaji ambaye aliwekwa kwenye mfumo wa kupatikana mabao na Zidane.
Nne, itakuwaje Varane akiondoka. Ramos wakati wote alionekana imara zaidi kimwili na daima alikuwa akijifua ili kukabiliana na wapinzani wanaotumia nguvu zaidi licha ya umri wake wa miaka 35 kudhaniwa amekwisha. Kama Rapahel Varane akiamua kuondoka kutakuwa na pengo kubwa katika safu ya ulinzi. Varane licha ya umri wake, naye alikabiliwa na majeraha mara kwa mara, pia anatakuwa huru kuzungumza na klabu yoyote kuanzia Januari mosi hali ambayo inatengeneza pengo kwenye safu ya ulinzi.