in , ,

EPL: Mabadiliko msimu mpya uwanjani

Baada ya kumalizika kwa Msimu wa Soka wa Ligi Kuu England (EPL) 2018/19, kuna mabadiliko kadhaa kwenye mchezo huo.

Hapana ubishi kwamba kuna baadhi ya maamuzi yaliyofanywa kwenye msimu uliomalizika ambayo kimsingi hayakutakiwa kufanywa wala mabao kukubaliwa, achilia mbali faulo zilizokataliwa au kutolewa kiutata.

Msimu ujao unakuja (japokuwa muda bado) na kuna mambo ambayo wadau wa soka watafurahia, kwani wamekuwa wakiyasibiri kwa muda lakini hayakuwa yameidhinishwa na Bodi ya Kimataifa ya Vyama vya Soka – IFAB).

Inadhaniwa kwamba maidhinisho hayo yatawafanya washabiki kutikisa vichwa kwa kukubaliana zaidi kuliko kutofautiana wakati wa waamuzi kuchukua uamuzi kutokana na masuala ambayo vinginevyo yangekuwa tata.

Tutarajie nini kwenye msimu ujao wa EPL basi sie wapenda soka? Kuanzia msimu ujao ikiwa mpira utamgonga mshambuliaji wakati akijenga muvu ya kufunga bao – iwe makusudi au kwa bahati mbaya – bao litakataliwa. Iwe iwavyo, lakini hiyo itasaidia kuepuka bao kama lile la Fernando Llorente wa Tottenham Hotspur.

Hapatakuwapo tena na suala la mpira kudundwa au kurushwa juu na mwamuzi, badala yake timu ambazo mpira upo kwenye nusu yao watapewa haki ya kupiga, ikitokea mchezaji kaumia au kwa sababu nyingine isiyohusisha kosa la timu, mpira ulisimama. IFAB inasema kwamba mfumo wa sasa wa kurusha au kudunda mpira unatumiwa vibaya.

Hata hivyo, wachezaji wote, isipokuwa wanaoupiga mpira husika, watatakiwa kukaa umbali wa mita nne kutoka eneo mpira unakopigiwa.

Kwenye kubadilisha wachezaji, mchezaji anayetoka nje sasa hatakuwa tena na uamuzi wa kuchagua upande upi atokee; atatakiwa kuondoka uwanjani mara baada ya kuelekezwa na kwa kutumia mwanya wa karibu zaidi ili kuepuka kupoteza muda ambako wachezaji wengi wamekuwa wakifanya hasa baada ya ama kushinda au kwenda sare kwenye mechi wanayohitaji matokeo kama hayo.

Washambuliaji wa timu inayopiga mpira wa adhabu ndogo hawataruhusiwa tena kujipachika kwenye ukuta wa timu inayozuia mpira. Hii imekuwa ikisababisha mikiki miongoni mwa wachezaji. Hakuna chochote cha kuhalalisha mchezaji kukaa na wapinzani wanaozuia kwenye ukuta walioutengeneza.

Ama kuhusu penati, magolikipa watatakiwa kuhakikisha mguu mmoja upo kwenye mstari wa goli na mwingine wanaweza kuuweka popote. Kwa kawaida wamekuwa wakitakiwa kuhakikisha miguu yote imo juu ya chaki, lakini mara chache sana makipa wametimiza hilo, wakiondoka hapo mara baada ya kipenga kupulizwa.

Hata hivyo, IFAB wanasema kwamna kuanzia msimu ujao makipa watazuiwa kushika mitambaa ya panya kabla ya mikwaju ya penati kupigwa. Ama makocha nao sasa watakuwa wanahusika kwenye adhabu sawa na wachezaji, waamuzi wakiwa na haki ya kutoa kadi za njano au nyekundu kwa wachezaji, makocha na hata wafanyakazi wa benchi la ufundi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

EPL: upende usipende ndio hivyo

Tanzania Sports

SIMBA YATETEA UBINGWA LIGI KUU