in , ,

England yataja kikosi

Kocha wa Timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson ametaja kikosi cha timu yake kwa ajili ya mechi dhidi ya Estonia na Lithuania kwa ajili ya kufuzu kwa michuano ya Euro 2016, akimwacha nje mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge.

Sura mpya kwenye kikosi hicho ni pamoja na kiungo wa Tottenham Hotspur, Dele Alli, 19, na mshambuliaji mpya wa Liverpool,  Danny Ings, 23, ambao walipata kuchezea kikosi cha taifa cha U-21.

Sturridge ndio kwanza amepona majeraha ya muda mrefu na kocha wake, Brendan Rodgers alishasema wazi kwamba hangeweza kumudu kuchezea timu mbili hizo kutokana na hali yake. England tayari wamefuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Ufaransa, lakini wanahitaji kulinda heshima yao.

Wengine waliorejeshwa kikosini ni mlinzi wa Southampton, Ryan Bertrand atakayeziba pengo la Luke Shaw wa Manchester United alitevunjika mguu. Wengine walioitwa ni mlinzi wa Manchester United, Phil Jones na kiungo wa Liverpool, Adam Lallana aliyekosa mechi za Septemba dhidi ya San Marino na Uswisi kwa sababu ya kuwa majeruhi.

Mechi zao za mwisho katika hatua hii zitafanyika Oktoba 9 dhidi ya Estonia dimbani Wembley kisha watasafiri kwenda Lithuani siku tatu baada ya hapo.

Kiungo wa Aston Villa, Jack Grealish ambaye ameamua kuchezea England badala ya Jamhuri ya Ireland hakuweza kuitwa kwani inabidi asubiri kupata leseni ya kimataifa.

Wayne Rooney  akiwa na Manager wa England
Wayne Rooney akiwa na Manager wa England

Hodgson amesema mchezaji huyo amefanya uamuzi sahihi, baada ya kuwa amechezea Ireland kwenye U-21 lakini Juni akakataa alipoitwa kwenye kikosi cha wakubwa dhidi ya England.

Kikosi kamili na timu wanazotoka kwenye mabano ni makipa Jack Butland (Stoke City), Joe Hart (Manchester City) na Tom Heaton (Burnley).

Walinzi ni Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Kieran Gibbs (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Chris Smalling (Manchester United) na John Stones (Everton)

Kwa upande wa viungo ni Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Michael Carrick (Manchester United), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Jonjo Shelvey (Swansea City) na Raheem Sterling (Manchester City)

Washambuliaji walioitwa ni Danny Ings (Liverpool), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Wayne Rooney (Manchester United), Jamie Vardy (Leicester City) na Theo Walcott (Arsenal).

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

MATOKEO LIGI KUU BARA

Tanzania Sports

ARSENAL v. MANCHESTER UNITED