HII ni wiki ya kushuhudia mechi mbalimbali za Kimataifa, ambapo timu za Taifa zinachuana kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe l Dunia mwaka 2026 huko Mexico, Canada na Marekani. Katika fainali za mwaka 2026, zitafanyika kwa ushirikiano wan chi tatu kwa mara ya kwanza. Awali rekodi iliyopo ni nchi mbili kushirikiana katika fainali hizo, ambapo mwaka 2002 Japan na Korea kusini walishirikiana kuandaa.
Wakati macho na masikio yakiwa yanaelekezwa kwenye mechi za kufuzu, TANZANIASPORTS inakuletea uchambuzi kuhusiana na jina la mtu ambaye sasa anaelekea kuwa jinamizi kwenye soka la England. Hakuna ubishi kuwa jina la Eddie Howe ndilo linatajwa zaidi kwneye medani ya soka hapa England. Sababu za kutajwa jina hili ni muhimu kuzielezea kwenye makala haya.
Kuelekea fainali za Kombe la Dunia England itakuwa chini ya darubini kali, huku wakiwa tayari kumpa kazi kocha mwingine. Mabosi wa FA walipoamua kumpa kazi Thomas Tuchel walikosolewa na baadhi ya wachambuzi ambao walidai kocha mzawa ndiye alifaa zaidi kuongoza nchi yao. kulikuwa na mjadala mkubwa sana juu ya nafasi ya kocha mzawa katika timu yao ya Taifa.
Baada ya Gareth Southgate kujiuzulu nafasi yake aliyodumu kwa miaka 9 hivi, ulikuwa wakati mwingine ambao baadhi ya wadau walitaka kuona kocha mzawa anapewa jukumu la kuinoa England. Hata hivyo mabosi wa FA walibainisha tangu walipotangaza nafasi ya kazi ya ukocha England kwamba wanataka kocha ambaye atakuwa na uwezo wa kutwaa mataji makubwa ya Kimataifa; Kombe la Dunia na Kombe la Mataifa ya Ulaya maarufu kama Euro.
Kwanini ni jinamizi la England?
Ni dhahiri huyu ni miongoni mwa mwakocha ambayo kwa hapa England naweza kusema yuko mguu sawa, nje au ndani yaani muda woowote anajua anaweza kupewa timu ya Taifa. Eddie Howe amefanya kazi nzuri katika kikosi cha Newcastle United kwa kutwaa taji la Carabao mbele ya Liverpool kwa ushindi wa mabao 2-1. Kocha huyu amekuwa akitajwa mara kwa mara kuchukua ukocha wa England, lakini FA iliamua kumpa jukumu Thomas Tuchel. Kwa mazingira ya sasa hapa England sitashangaa kuona huyu akiwa ndiye mtarajiwa wa kiti hicho kama mabosi wataamua kurudi kwa kocha wa mzawa. Eddie Howe ndiye anafundisha soka la kiingereza, kama nilivyoeleza mwanzoni kwa kutaja klabu yake ya Newcastle United.
Bila shaka yoyote hili ni jinamizi ambalo litakuwa linarandaranda kwenye midomo ya wadau wa soka England.
Je Eddie Howe ni kocha wa aina gani?
Kama unapenda kuliona soka la kiingereza, basi hakikisha unaitazama Newcastle United. Soka lao ni lile la nguvu-kazi, soka la shoka, vurugu, nguvu na kasi kubwa. Katikati ya dimba anatumia akili ya Kibarazil ya Joelington na Bruno Guimares. Wabrazil hawa wamekuwa chachu na uimara wa klabu ya Newcastle United, huku safu ya ulinzi ikiwa chini ya Dan Burn. Safu ya ushambuliaji inaongozwa na msomali Alexandre Isak. Timu hii ni ile ambayo inacheza mpira wa kiingereza. Mpira wao ni ule wa matokeo zaidi.
Ufundishaji wa kocha huyu umeegemea maeneo matatu; ulinzi imara, viungo wenye jukumu la kufanya kazi chafu na washambuliaji katiri. Katika safu ya ulinzi, Newcastle United wanacheza mpira wa aina yake. Wanapozuia kwenye eneo lao la 18 wanakuwa na mabeki watano, viungo wanne, na mshambuliaji mmoja. Hiyo ina maana mfumo wake wa ulinzi ni ule wa 5-4-1. Mashambulizi mengi ya Newcastle United hupangwa kwa kushtukiza.
Mara nyingi mawinga wake ndiyo wanaoikimbiza timu hiyo. Baada ya viungo Bruno Guimares na Joelington kufanya kazi chafu kwenye eneo la kiungo huwa wanadhibiti mpira na kukukota kwa kasi kuelekea lango la adui. Mara wanapovuka mstari wa katikati ya uwanja, jukumu lao linakuwa limekwisha na hivyo wanakabidhi kwa mawinga. Ukiangalia mabao mengi anayofunga Alexandre Isak ni yale ambayo yanatokana na kazi nzuri ya mawinga. Bruno na Joelington wanapomaliza kazi chafu wanahamishia majukumu kwa mawinga kwahiyo hapo ndipo kasi ya Newcastle Unmited inapoongezeka. Mashambulizi hayo huwa hayadhaniwi kama yanazaa mabao, ndiyo maana unashtukia mpira umeingia wavuni.
Kasi ya Newcastle United inaanza pale Bruno na Joelington wakipewa mpira. Uwezo wao wa kukabiliana kwa matumizi ya nguvu inawafanya waweze kuhifadhi mpira na kutengeneza mashambulizi mazuri. Linapokuja suala la kukaba, Joelington anakuwa na jukumu la kufanya kazi chafu zote; kutibua mipango, kudhibiti wabunifu wa timu pinzani,
Kwahiyo uchezaji na ufundi wa Newcastle United unaweza kuturudisha kwenye kikosi cha Liverpool cha Kenny Dalglish. Hawa wanacheza mpira wa kiingereza ambao Thomas Tuchel anatamani uchezwe timu ya Taifa. Hii ina maana Eddie Howe ndilo jinamizi ambalo litakuwa linamwandama sana Thomas Tuchel. Shinikizo la kuteuliwa Eddie Howe kuinoa timu ya Taifa ya England limekuwa kubwa na kila mara litakuwa linaibuliwa. Ikizingatiwa kwamba sasa hivi ametwaa taji la Carabao, ndiyo imekuwa sababu ya nyongeza ya kilio cha kukabidhiwa timu ya Taifa. Kama Thomas Tuchel anataka England icheze soka la Kiingereza basi anatakiwa kuzungumza na Eddie Howe ama kuitazama Newcastle United inavyocheza.
Comments
Loading…