Menu
in , , ,

Eberechi Eze aipaisha Arsenal

Tanzania Sports

Mchezaji akiwa na kipaji kama hicho, mambo haya hutokea
Frank ‘amesikitishwa’ na kiwango cha Spurs kwenye kipigo cha 4-1

Mikel Arteta amemsifu Eberechi Eze kwa kuongeza “aura” ndani ya kikosi cha Arsenal baada ya kiungo huyo kufunga hat-trick yake ya kwanza katika maisha yake ya soka na kuiumiza Tottenham, huku ushindi huo ukiwapeleka Arsenal kileleni kwa tofauti ya pointi sita kwenye Ligi Kuu ya England.

Eze alikuwa karibu kusajiliwa na Spurs akitokea Crystal Palace majira ya kiangazi kabla ya dili hilo kuvurugwa na mahasimu wao wa kaskazini mwa London, na mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England akawalipa kisasi mara baada ya Leandro Trossard kufungua ukurasa wa mabao.

‘Dibbling’ ya kuvutia na kumalizia kwa ustadi ilifanya matokeo kuwa 2-0 hadi mapumziko kabla ya Eze kuongeza la pili sekunde 36 baada ya kipindi cha pili kuanza. Alikamilisha hat-trick yake baada ya bao safi la kufutia machozi kutoka kwa Richarlison, huku Tottenham ikionyesha kutokuwa na nia ya kushindana na ikimaliza mchezo ikiwa na hoi kabisa.

“Vitu hutokea kwa sababu,” alisema Arteta, ambaye timu yake ilimaliza nafasi ya pili mara tatu mfululizo kabla ya usajili wa Eze kwa paundi milioni 67.5 majira ya kiangazi. “Baada ya majukumu ya timu ya taifa, alikuwa na mapumziko ya siku mbili, lakini siku moja tu baadae alitaka kufanya mazoezi, alitaka kuboresha nafasi yake ya ubora, alitaka kufanya mazoezi ya ziada na alikuwa ananiuliza maswali kuhusu hili na lile.

“Unapokuwa na mchezaji mwenye kipaji kama hicho, na hamu ya kiwango kile, basi mambo kama haya hutokea. Na anastahili sifa. Nimefurahi sana kwa mafanikio yake, kwa sababu tangu siku aliyokuja, ameleta kitu tofauti ndani ya timu.

“Ni furaha… ni faraja ambayo timu hii ilihitaji na natumai itampa yeye na timu nzima kujiamini zaidi, kwamba wakati wowote anaweza kutupa ushindi. Huo ndiyo uwezo alionao na anapaswa kuutumia kikamilifu.”

Eze, ambaye alikuwa amefunga mabao mawili pekee kwenye mechi zake 15 za mwanzo tangu kujiunga na Arsenal baada ya kuwahi kukataliwa na klabu hiyo akiwa kijana, alisema: “Hii ni siku maalum kwangu. Maneno hayawezi kuielezea siku ya leo. Hicho ndicho nilichokiomba kwa Mungu: hat-trick, na nimeipata. Namshukuru Mungu. Mungu amenipa, hiyo ndiyo imani. Familia yangu yote ipo hapa, na hilo linaiweka siku hii kuwa ya kipekee zaidi kwangu.”

Tottenham walianza mchezo na safu ya ulinzi ya wachezaji watano, lakini Thomas Frank aliacha mfumo huo wakati wa mapumziko, na timu yake ikamaliza ikiwa na miguso minne tu kwenye eneo la hatari la Arsenal.

“Ilikuwa ya kusikitisha sana kwamba hatukucheza vizuri dhidi ya Arsenal, mpinzani wetu mkubwa. Naweza tu kuwaomba radhi mashabiki,” alisema kocha wa Spurs. “Tulijaribu kuja hapa na kuwa wakali, ‘kupress’ juu na kwa vipindi kuwaiga. Hatukuwa wazuri vya kutosha kutoka kwenye hali tuliyokuwa tumejiingiza.”

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version