in , , , ,

Drogba atafuta timu

*Mangala awakataa Manchester City
*Arsenal wamwendea Karim Benzema

Mshambuliaji mkongwe wa Ivory Coast, Didier Drogba ametangaza kuihama klabu yake ya Galatasaray.

Drogba aliyepata kuwika na Chelsea kabla ya kutoongezewa mkataba na kuamua kuondoka, ameweka wazi wikiendi hii kwamba anaondoka Uturuki.

Tayari amewaaga washabiki wake wa nchini humo, akisema alifarijika na jinsi walivyokaa naye na alihisi yupo nyumbani lakini wakati umefika kwake kuondoka.

Drogba (36) amekuwa akihusishwa na kurudi kwenye Ligi Kuu ya England na kwa namna ya pekee kwenye klabu aliyochezea ya Chelsea, hasa kwa vile Jose Mourinho naye amerejea huko.

Zipo taarifa zisizothibitishwa kwamba Mourinho amekuwa akitaka kumrejesha mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast Stamford Bridge.

Drogba anayekwenda Brazil kwa ajili ya kuwakilisha nchi yake kwenye Kombe la Dunia, anaweza kuvutia timu nyingine iwapo atafanya vyema huko.

Hata hivyo, anakabiliwa na ushindani wa wachezaji wengine wa Ivory Coast katika nafasi yake ya ushambuliaji.

Hata hivyo, kwa mara kadhaa Drogba amekuwa na majeraha sawa na ilivyo kwa mwanasoka bora wa Afrika anayechezea Ivory Coast, Yaya Toure aliyetolewa kwenye mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya West Ham.

Kocha wa Ivory Coast, Sabri Lamouche ameeleza wasiwasi wake juu ya wachezaji hao wawili kuwa fiti muda wote wa mashindano hayo makubwa zaidi duniani katika soka.

Drogba ndiye alifunga penati ya mwisho iliyowapatia Chelsea ubingwa wa Ulaya msimu wa 2012 na huenda akajiunga na wakongwe wengine, John Terry na Frank Lampard klabuni Chelsea.

Eliaquim Mangala awakataa Man City

Mabingwa wapya wa England, Manchester City wamekumbana na kizingiti baada ya mlinzi wa Porto, Eliaquim Mangala kukataa kujiunga nao.

Mlinzi huyo anayethaminiwa katika bei ya pauni milioni 35 alitafutwa na Man City tangu wakati wa usajili wa dirisha dogo Januari mwaka huu ikashindikana.

Baada ya kutwaa kombe wiki iliyopita, City walianza mikakati yao lakini Mangala anasema kwamba angependa kujiunga na Chelsea kuliko City, kwani anataka kuishi London.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 amesema suala la klabu gani atachezea linawekwa kando hadi akamilishe utumishi wake kwenye timu ya taifa.

Manchester United na Paris St Germain nao pia wameonesha kutaka kumsajili mchezaji huyo. City wanamtaka licha ya kuzuiwa kutumia zaidi ya pauni milioni 49 kwa usajili wa msimu ujao.

Arsenal wamfuata tena Benzema

Katika hatua nyingine, Mabingwa wa Kombe la FA, Arsenal wameanza kumfukuzia mshambuliaji wa kati wa Real Madrid, Karim Benzema.

Inaelezwa kwamba Real Madrid wapo tayari kuwapa Arsenal mchezaji huyo lakini watadai dau la pauni milioni 40.

Real Madrid wanataka kumsajili mpachika mabao wa Liverpool, Luis Suarez lakini watatakiwa kutafuta kitita cha fedha ili kuwashawishi Liverpool kumuuza mchezaji huyo.

Benzema (26) amekuwa na msimu mzuri ambapo amepachika mabao 24 katika mashindano yote lakini Rais Florentino Perez wa Real Madrid anataka kumsajili Suarez ili afanye kazi na Gareth Bale na Cristiano Ronaldo katika safu ya ushambuliaji.

Benzema alibaki na namba yake baada ya mwenzake, Gonzalo Higuain kuuzwa Napoli msimu uliopita huku Mesut Ozil akiuzwa Arsenal.

Arsene Wenger aliyesaini mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuwafundisha Arsenal, anaweza kuwa tayari kutoa kitita hicho ili kumpata Benzema asaidiane na Mfaransa mwenzake, Olivier Giroud aliyebaki mwenyewe kama mshambuliaji wa kati.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Washabiki Arsenal wafunika mitaa

Rais wa Bolivia asajiliwa kucheza soka