in ,

DILI LA MPANZU LIMEBAKI KIDOGO

Leo Tanzania Sports ilipata nafasi ya kutembelea mazoezi ya timu ya Simba SC yaliyofanyika katika uwanja wa mazoezi wa MO Arena uliopo Bunju, Dar Es Salaam. Baada ya mazoezi mkuu wa idara ya habari ya Simba SC , Ahmed Ally alizungumza na waandishi wa habari kikiwemo Tanzania Sports.

Katika mazungumzo hayo, Ahmed Ally alitabainisha kuwa baada ya kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho, Simba SC imeanza kujiandaa na mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC itakayochezwa katika uwanja wa New Aman Stadium uliopo Zanzibar.

Ahmed Ally amedai kuwa Azam FC wajiandae na kifo na hawawezi kukwepa kifo popote pale watakapopeleka mechi. Ahmed Ally amedai kuwa Azam FC hata kama wakipeleka mechi Gombani Pemba, Unguja kifo kitakuwepo pale pale.

Ahmed Ally amedai kuwa licha ya kwamba Azam FC wameanza kujipata kwa sasa baada ya kuanza kwa kusua sua hiyo haimanishi kuwa Azam FC wanaweza kuendelea kushinda kwenye mechi hiyo.

Pia, Ahmed Ally alipoulizwa kuhusu usajili wa Elia Mpanzu mchezaji kutoka Congo amedai mpaka sasa hivi imebaki kitu kidogo tu kwao wao kumsajili mchezaji huyo. Mazungumzo kati ya Simba SC na mchezaji husika mpaka sasa hivi yameshakamilika.

Kitu pekee ambacho kinakwamisha mpaka sasa hivi usajili huu kutokamilika ni mazungumzo kati ya Simba SC na timu inayommiliki Elia Mpanzu. Mazungumzo ya pande hizi mbili bado yanaendelea na wanaweza kufikia hatua ya makubaliano hivi karibuni. Alimalizia Ahmed Ally

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

INATENGENEZWA TP MAZEMBE NDANI YA YANGA?

Tanzania Sports

Manchester City Kwenye Mtihani Mkubwa wa Sheria