Menu
in , , ,

Chile wana mlima mrefu  kurudi katika ubora

Tanzania Sports

UNAMKUMBUKA Marcelo Salas? Hili nijina kubwa katika kandanda. Miongoni mwa wachezaji ambao wanakumbukwa kwa uwezo mzuri katika soka. Salas alikuwa na kasi, chenga, na uwezo wa kucheka na nyavu. Ni mzaliwa wa Chile, ambayo ni maarufu kama La Roja kwenye mchezo wa soka, sawa na Tanzania inavyojiita Taifa Stars. Aliifanya Chile kuwa miongoni mwa timu za kuogopeka sana linapofika suala la fainali za Kombe la Dunia. 

Rekodi za fainali za Kombe la dunia haziwezi kuitenga nchi hii ambayo inasisimua kila inaposhiriki. Ni timu ambayo vigogo wa soka kutoka Amerika kusini hadi Ulaya, Afrika na Asia wanaiogopa. Ni nchi ambayo imezlisha vipaji vingi na kutikisa katika vilabu mbalimbali kwenye soka la kulipwa. Chile unaweza kuibeza sasa, lakini kwenye mchezo huu wa kandanda nchi hii sio ya mchezo. TANZANIASPORTS inaangazia sababu za kuyumba kwa nchi hii kwenye mashindano makubwa duniani, ambapo kwa mara nyingine haitakuwa miongoni mwa zile zitakazoshiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 huko Marekani, Mexico na Canada.

Kizazi dha dhahabu

Ukizungumza Chile, unaweza kuirudisha Bulgaria kwa barani Ulaya. Wakati Bulgaria imepoteana kwenye mchezo wa soka, Chile nayo inahangaika kila kukicha bila mafanikio. Kizazi cha  dhahabu cha akina Marcelo Salas kilikuwa kikionesha cheche zao kwenye fainali za Kombe la Dunia. Lakini kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita pakiwa na mashindano mawili ya fainali za Kombe la Dunia, Chile imeshindwa kufukura. Kizazi cha dhahabu kilichokuwa kikitamba miaka ya nyuma kinaonekana kuondoka katika ramani ya Soka. Kushindwa kufuzu kulimlazimisha nahodha wao Arturo Vidal na staa mwenzake Alexis Sanchez walilazimika kuomba radhi mashabiki wa Chile na kudai kizazi kipya kinatakiwa kuchukua jukumu zito la kuivusha nchi hiyo kwenye nyakati ngumu ili isonge mbele kimafanikio.

Kocha kung’atuka

Kudhihirisha hali ya soka la Chile ni ngumu, kocha wake Marcelo Salas ametanagza kuachia ngazi ili kupisha akili mpya ya kusaidia taifa hilo. Kocha huyo amelazimika kauchia ngazi baada ya Chile kutofuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026. Hatua hiyo ilifika mara baada ya kushuhudia Chile wakziabwa mabao 2-0 na Bolivia jumanne wiki hii. 

“Tuliwaambia viongozi wetu kuhusiana na hatua yetu, lakini kwanza tulitaka kufanikisha Chile ifuzu fainali za kombe la Dunia. Tulikuwa na imani hiyo na viongozi wa shirikisho walituruhusu kupambana ili kuipeleka Chile kwenye fainali za Kombe la Dunia. Isivyo bahati tumeshindwa, na benchi zima la ufundi linaondoka. Matokeo haya yalikuwa kinyume cha matarajio yetu. Kwa kuwa hatuna matokeo mazuri yna kushindwa kwenda Kombe la dunia kwa mara ya tatu hii ina maana tunapaswa kuondoka,” alisema kocha huyo alipozungumza na Shirika la Reuters.

Unapomsikiliza kocha huyu haraka unaona uchungu walionao benchila ufundi kuhusiana na hali ya Chile. Kwa mashabiki wa soka wanapenda ushindani, na walitegemea Chile ingefuzu na kuleta kandanda safi iama inavyofahamika. Lakiani mambo yamekuwa magumu na hivyo benhi zima limeng’oka ili kukaribisha mbinu mpya za kuisaidia Chile.

Miaka kumi migumu

Uchungu wa mashabiki wa soka ni pale wanaokumbuka umahiri wan chi hiyo miaka ya nyuma. Si raia wa Chile pekee bali ulimwengu unatambua namna Chile walivyo mahiri kwenye kandanda lakini mambo yamekuwa magumu kwa kipindi cha miaka 10. Chile walishindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 zilizofanyika nchini Russia kisha wakaangukia pua kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022. Hata hivyo mafanikio yao ya kujivunia ni kutwaa taji la Copa America mwaka 2015 na 2015. Chini ya kocha Gareca ambaye aliteuliwa mwaka 2024, Chile imeshinda mechi moja kati ya michezo 13 ya kalenda ya FIFA.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version