in , , ,

Chelsea wakoleza mbio

Chelsea wameendeleza mbio zao kwenye Ligi Kuu ya England, baada ya kuwatungua Newcastle 2-0 kwa mabao ya Oscar na Diego Costa na kufikisha pointi 49 katika michezo 21.
Vijana hao wa Jose Mourinho wamefungua pengo la pointi mbili kutokana na Manchester City waliokuwa wamefungana nao kwenda sare ya 1-1 na Everton kwenye mchezo mwingine wikiendi hii.
Newcastle walio bila kocha baada ya Alan Pardew kuhamia Crystal Palace walianza mechi vyema na nusura Moussa Sissoko awafungie bao, lakini shuti lake liligonga mwamba, huku Chelsea wakihangaika kujikusanya.

Hata hivyo bao la dakika ya 43 la Oscar lilirejesha nguvu na uimara kwa Chelsea, na Costa alipotia la pili dakika ya 59, ilikuwa kana kwamba mechi imemalizika, kwani Blues walimiliki vyema mpira. Newcastle waliwafunga Chelsea kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza, lakini pamoja na kurejea kwa kipa wao namba moja, Tim Krul hakukuwasaidia.

Everton waliokuwa wakisuasua walishangaza kwa kufanikiwa kwenda sare na mabingwa watetezi Man City, kwenye mechi iliyofanyika katika dimba la Goodison Park. Fernandinho aliwafungia City katika dakika ya 74 lakini Steven Naismith akasawazisha dakika nne tu baadaye na kumtia shime kocha wao, Roberto Martinez.
Katika mechi nyingine, Liverpool walifufuka kwa kuwafunga Sunderland 1-0 kwa bao la Lazar Markovic, kwenye mechi ambayo nahodha Sreven Gerrard wa Liverpool aliumia na kutolewa nje katika dakika ya 45.

Sunderland waliokuwa nyumbani walipata pigo kwa mchezaji wao, Liam Bridcutt kutolewa nje baada ya kulambwa kadi mbili za njano kutokana na mchezo mbaya na kocha wao, Gus Poyet alisema anafikiria kuchukua maamuzi magumu.

Kwenye mechi nyingine Jumamosi hii, Burnley waliwakwangua QPR 2-1, Leicester wakawazidi nguvu Aston Villa 1-0, Swansea wakatoka sare ya 1-1 na West Ham, West Bromwich Albion walio chini ya kocha mpya, Tony Pulis wakawafunga Hull 1-0 huku Crystal Palace wa Alan Pardew wakishangaza kwa kuwafunga Tottenham Hotspur 2-1.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Lampard na utata wa usajili wake

Wilfried Bonny huyoo Man City