in , ,

Bundesliga inarejea

Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga inatarajiwa kurejea kuanzia mapema mwezi ujao kwa ajili ya kuhitimisha mechi zilizosalia.

Ligi katika nchi nyingi kote duniani zimesitishwa kutokana na virusi hatari vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu iliyoendelea kuua maelfu ya watu katika pande mbalimbali za dunia.

Lakini Ujerumani walijizatiti tangu mapema kwa kuchukulia kwa umakini mkubwa virusi hivyo, kwa kutumia mfumo wake imara wa huduma za afya, na sasa wapo tayari kurudi uwanjani, wakisema kwamba Mei 9 inaweza kuwa siku ya kuanza mechi zilizosalia.

Ujerumani ni kana kwamba waliongoza kwenye mapambano dhidi ya Covid-19 kwa kuanza kupima mapema kabisa na kutoa huduma zote muhimu kwa waliokuwa na dalili au kuambukizwa uhonjwa huo na matokeo yake wamekuwa na vifo vichache na pia wagonjwa wachache mahututi.

Mambo sasa yanarudi kama kawaida, tofauti na kwenye mataifa mengine ya Ulaya na Amerika, ambapo serikali na taasisi za afya pamoja na wafadhili wanahangaika kudhibiti virusi na ugonjwa huo.

Bodi ya Ligi ya Ujerumani (DFL) wanaosimamia Bundesliga na Ligi daraja la Pili wamesema kwamba wamedhamiria kuona msimu unaisha vyema. Wajumbe viongozi wa klabu zao 36 za soka ya kulipwa walikutana jana Alhamisi kujadili juu ya jinsi ya kuendelea kwa msimu huu wa soka wa 2019/2020.

Hata hivyo, bado mamlaka za soka za taifa hilo zna maswali mengi kabla ya kuwasaha taa ya kijani kuashiria kuanza kwa mechi hizo. Maswali ni pamoja na ikiwa mechi zitachezwa bila watazamaji au kwamba watazamaji wataruhusiwa.

“Ikiwa ni kuannza Mei 9, basi tupo tayari. Ikiwa ni baadaye, tutakuwa tayari vilevile. Kwetu sie tunaweza kufikia kutoa uamuzi kutegemeana na wanasiasa watakavyoamua. Sio sisi wa kuamua juu ya lini, lakini tupo tayari. Mechi bila washabiki si kile kitu ambacho tungependelea sana – lakini kwa sasa tutakubaliana na kile ambacho kinawezekana,” akasema Mtendaji Mkuu wa DFL, Christian Seifert.

Mechi ya mwisho ya Bundesliga kabla ya kusitishwa mikusanyiko, ilikuwa baina ya Borussia Monchengladbach na Cologne, ikifanyika Machi 11 bila kuwapo watazamaji uwanjani. Kwa msingi huu ni kwamba uamuzi wa kuanza kwa ligi hiyo utategemea serikali kufungua njia.

Hivi karibuni, siasa za Ujerumani ziliamua kwamba matukio makubwa yenye umati wa watu yasiruhusiwe hadi itakapotangazwa vinginevyo. Pamoja na kwamba maradhi kwa kiasi kikubwa yameisha au si tishio, umakini wa Ujerumani umefanya taifa hilo kuzuia mikusanyiko mikubwa hadi Oktoba mwaka huu.

Kwa maana hiyo njia pekee ya kumaliza Bundesliga mapema ni kucheza bila washabiki ambao, hata hivyo, watafuatilia kwenye televisheni majumbani mwao. Watakaoruhusiwa kuingia uwanjani ni wachezaji, makocha, matabibu, waamuzi, watoto wa kubeba mipira na wafanyakazi wa uwanja husika.

Wengine watakaoruhusiwa ni watu wa idara za ufundi, maofisa usalama na wale wanaofanya kazi kwa ajili ya kurusha matangazo ya televisheni bila kusahau watu wa VAR. maofisa wa Bundesliga wanakadiria kwamba kiasi cha watu 300 kitahitajika kuingia uwanjani kwa kila mechi.

Nchini Ujerumani, majimbo 16 yenye uhuru kiasi ndiyo huamua idadi ya watu wanaoruhusiwa kuwa katka mikusanyiko. Uamuzi juu ya idadi hiyo kwa sasa utafanywa mwishoni mwa mwezi huu, ikimaanisha wiki ijayo.

Serikali za majimbo husika pia ndizo zitakuwa na uamuzi wa mwisho juu ya mipango ya DFL, ikimaanisha zinaweza kuipiga stop, lakini wanajua jinsi klabuz a soka zinavyoogelea katika matatizo ya kiuchumi wakati hu una inadhaniwa kwamba zitaruhusu maombi ya klabu husika.

“Wikiendi yenye soka ni nzuri sana, tena kwa mbali bila wikiendi isiyokuwa na soka. Ndiyo maana naweza kupata picha ya mechi zinazochezwa bila kuwapo watazamaji uwanjani,” akasema Markus Soder – Kiongozi wa Jimbo la Bavaria.

Yeye na Armin Laschet, Kiongozi wa North Rhine-Westphalia, wameshaweka wazi kwamba wanadhani ni vyema kwa Bundesliga kuanza mapema, hata kama ni Mei 9, watu waweze kutazama soka hata kama ni kwenye televisheni.

Soder na Laschet wametangulia kutoa kauli hizo wakijua kwamba Serikali ya Shirikisho la Ujerumani pamoja na wakuu wa majimbo yote 16 wanakutana mwishoni mwa mwezi huu. Inadhaniwa kwamba wanaweza kutoka na uamuzi wa kuruhusu mechi za soka kuchezwa kuanzia mwezi ujao au vinginevyo.

Wiki chache zilizopita, DFL waliunda kamati maalumu kwa ajili ya kuchunguza na kupanga ni protokali gani muhimu zinazotakiwa ili kuanza kwa ligi. Kamati hiyo ilipendekeza kwamba uwanja ugawanywe kwenye maeneo matatu. Ni watu 100 tu wataruhusiwa kuwa katika kila eneo moja kati ya hayo matatu.

Eneo la ndani ni kwa ajili ya wachezaji 22, wachezaji wa akiba 18, waamuzi watano na watu wengine kadiri ya 53 hivi. Majukwaa ndilo eneo la pili wakati lile linalozunguka uwanja wote kwa ujumla likiwa la tatu.

Mipango mingine inajumuisha na upimaji wa mara kwa mara wa wachezaji na makocha kubaini uwapo wa virusi au vinginevyo. Kazi hiyo itafanywa wakati, baada na kabla ya mazoezi na pia kabla ya mechi. Mtaalamu wa kemia na masuala ya viumbo hai, Alexander Kekule kutoka Chuo Kikuu cha Martin Luther, Halle, anakisia kwamba DFL itahitaji hadi vipimo 20,000 na hatua maridhawa kwa ajili ya kuendesha mechi hizo wakati huu janga likiwa halijaisha kabisa.

Baadhi ya watu wanaona kwamba kuanza ligi sasa ni mapema mno, wakati ambapo bado watu wanaendelea kupimwa na kuhudumiwa, ambapo kwa wiki watu 640,000 hupimwa ili kuhakikisha hali za afya zao zinajengwa. Baadhi ya viongozi wa klabu wameonesha kwamba wanataka mipango ya kurudia ligi ianze.

Klabu zinakabiliwa na hali mbaya ya uchumi. Wenye haki nyingi zaidi za matangazo ya televisheni – Sky, Eurosport na watangazaji wa umma – ARD na ZDF, bado hawajalipa kiasi cha fedha kwa klabu ambazo ni €304m (£265m).

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

‘Saudia wasiuziwe Newcastle’

Tanzania Sports

Usajili fedha kidogo