in , , ,

BRAZIL YA NEYMAR JR NA UKAME WA MAKOCHA

STAA wa Kibrazil Neymar Jr amerejea katika Ligi ya nchi yao. Neymar Jr amerejea katika klabu yake iloyomkuza ya Santos ambayo pia imewahi kuleta kipaji cha Pele kilichotokisa Dunia kwa kandanda safi. 

Soka la Neymar Jr kutoka Santos lilikwenda Barcelona ambako aliunda ‘utatu mtakatifu’ akiwa na Luis Suarez na Lione Messi. Baada ya kucheza Kwa muda Neymar Jr alihalia PSG ya Ufaransa, kabla ya kuelekea katika Soka la Saudi Arabia. Wakati Neymar akirejea Santos, baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Brazil wanaamini kuwa katika fainali zinazo za Kombe la Dunia watacheza kwa ajili ya nyota huyo.

 Savinho winga machachari wa klabu ya Manchester City amedai kuwa wana Kila sababu za kumfurahisha Neymar Jr kwenye fainali za Kombe la Dunia mwakani. 

Hata hivyo sifa kubwa ya Brazil ni kuzalisha wachezaji Wazuri na mahiri duniani. Miongoni mwao ni Ronaldo de Lima, Rivaldo, Robinho, Marcelo, Kaka, Aldair Santos, Vampeta na wengineo. 

Wakati Neymar Jr akirejea kwao Santos, pamoja na mawazo ya Savinho bila shaka yoyote Brazil inaweza kufanya jambo zuri kwenye fainali za Kombe la Dunia mwakan2026, lakini swali linaloulizwa sasa ni, Je wapo tayari kukiri kuwa Soka lao limekosa  makocha mahiri? Katika fainali wanazoshiriki, Brazil wanakuwa na makocha wao.

Fainali za Kombe la Dunia mwakan2002 ndizo za mwisho wa nchi kutwaa taji hilo maarufu. Vilevile walitwaa taji hilo wakiwa na kocha mzawa. Tangu wakati huo Brazil imepitia makocha wengi lakini haijapata mafanikio zaidi ya kuishia hatua ya robo fainali katika fainali zilizopita. Katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 bila shaka wataingia wakiwa na kocha wao Dorival.

Hivi karibuni jina la Felipe Luiz ndilo linalogonga vichwa vya Habari katika michezo. Kama msomaji umemsahau basi napenda kukumbusha Kwamba Felipe Luiz alikuwa beki mahiri wa kushoto na wa muda mrefu katika klabu ya Atletico Madrid chini ya kocha Diego Simeone. 

Felipe Luiz ndiye yule beki ambaye alikuwa anafunga kitambaa cheupe kichwani kuhifadhi nywele zake. Akiwa dimbani alikuwa mtanashati. Kwa uwezo na kipaji Felipe Luiz alikuwa moja ya hazina muhimu ya Atletico Madrid. Baadaye alikuwa kwenda Chelsea lakini hakudumu muda mrefu kabla ya kurejea Atletico Madrid. 

Huyu ni miongoni mwa mabeki Wazuri wa Kibrazil na kipaji chake kilidhihirisha anatoka nchi yenye kutengeneza wachezaji Wazuri. Luiz Felipe, alistaafu Soka na kugeukia maisha ya ukocha. Kwa sasa ndiye maarufu na anafuatuliwa kutokana na jina lake kubwa katika mchezo wa Soka.

Mbali ya sifa hiyo, swali analobebeshwa sasa ni Je anaweza kuwa kocha hodari kutoka Brazil? Je Felipe Luiz anaweza kuziba ombwe la uhaba wa makocha vijana wenye vipaji vya kufundisha? 

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo Wabrazil wanajiuliza. Brazil inapita katika nyakati ngumu kisoka. Wana uhaba wa makocha. Wana uhaba wa vipaji vikubwa. Wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha Soka la Kibrazil linarudi katika chati yake. Wapo wachezaji wanaonunuliwa na kucheza katika Ligi mbalimbali duniani, lakini wengi wao wanacheza timu za chini tofauti na miaka ya nyuma. 

Angalau Manchester City wamemnunua Vitor Reis beki wa kati ambaye anaungana na winga Savinho katika kuwakilisha Brazil. 

Ukiangalia mwenendo wao katika timu ya Taifa unakiri kuwa wanahitaji uwekezaji kwenye nafasi ya ukocha.

Wadau wanakubaliana kuwa changamoto kubwa ya Soka la Brazil ni kuadimika makocha Wazuri ndiyo maana watu kama Mano Menezes bado wanafundisha hadi Leo.

Katika kipindi hiki kigumu Brazil inashuhudia kuibuka Kwa jina la Felipe Luiz ambaye ni kocha wa Flamengo. Chini ya Felipe Luiz klabu ya Flamengo imefanikiwa kunyakua Mataji mawili ndani ya mechi 18 ya ukocha wake. Kwamba kocha huyo ameanza kazi mechi 18 na sasa ametwaa medali mbili. Hapo ndipo vyombo vya Habari na wadau wa Soka wanageuza macho na masikio kuzingatia utendaji wa Felipe Luiz. Je Brazil wanaweza kumwona kocha huyo kijana kama suluhisho la uhaba wa Walimu wa kandanda vijana wenye vipaji? Je washabiki wanaweza kuweka matumaini kwa Felipe Luiz au bado mapema? Hayo ndiyo mambo yanayotawala meza za majadiliano katika Soka la Brazil.

 Pengine maswali hayo yanaweza kuachwa kwa sasa lakini takwimu zake zinajieleza dhahiri shahiri. Sababu bado anao muda wa kuonesha na kudhihirisha kuwa yeye ndiye mwokozi wao. Pia yanaachwa kwa malengo ya kumpunguzia presha kocha huyo, na pengine anayo maeneo mengi ya kuboresha kiwango chake.

Aidha, Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) bila shaka linamwangalia kwa jicho la tatu kocha huyo kijana. Filipe Luiz akiwa kocha wa Flamengo kwa mechi 18, ameshinda 12 , ametoka sare mechi 5, amefungwa mechi moja. Ametwaa Mataji mawili katika fainali mbili.

Hii Ina maana mwanzo wake ni mzuri na CBF wana Kila sababu ya kufuatilia maendeleo yake. Ikumbukwe, Brazil wamewahi kuhusishwa na kumwajiri kocha wa kigeni Pep Guardiola na Carlo Ancelotti, lakini waliamua kuendelea na Dorival. Hii ina maana Felipe Luiz anaibuka kama kocha wa kutupiwa jicho kwa maslahi ya Brazil. Pia Brazil ndiyo timu inayopendwa zaidi duniani kwahiyo Kila mpenzi wa kandanda anatamani kuona Samba likichezwa huku Dunia ikishangilia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

JICHO LA KIUFUNDI KATIKA BAO LA LADAKI CHASAMBI

Tanzania Sports

LAWAMA KWA WAAMUZI DUNIA NZIMA