in , , ,

Brazil watinga nusu fainali

Brazil wamefanikiwa kukata tiketi ya kucheza nusu fainali, kwa kuwatoa Colombia baada ya kuwafunga 2-1 kwenye robo fainali kali.

Brazil walitawala zaidi kipindi cha kwanza, wakaenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja la dakika ya saba lililofungwa na nahodha Thiago Silva.

Bao hilo lilitokana na mpira wa kona uliochongwa na Neymar ambaye hata hivyo alikuja kuumia na kutolewa nje kwa machela dakika chache kabla ya mchezo kumalizika.

Mchezaji mahiri wa Colombia James Rodriguez alibanwa vilivyo kipindi cha kwanza ambapo Brazil walitamba sana uwanja mzima.

Hata hivyo, katika kipindi cha pili walionekana kuelemewa, huku Colombia wakichanua. Hata hivyo, Brazil walibandika bao la pili kupitia kwa mpira wa adhabu ndogo wa David Luiz uliozama moja kwa moja wavuni.

Colombia hawakukata tamaa, bali walijitahidi kutengeneza nafasi na kushambulia na dakika ya 79 nusura wafunge kama si kipa Julio Cesar kumkwatua mchezaji wa Colombia.

Cesar alipewa kadi ya njano, Colombia wakapata penati iliyotiwa kimiani na Rodriguez ambaye amefikisha mabao sita, akifunga katika kila mechi ya mashindano haya.

Brazil walijihami dakika za mwisho na kuishia na butua butua za hapa na pale, na kipenga cha mwisho kilipopulizwa Rodriguez anayetarajiwa kujiunga Real Madrid aliishia kulia machozi na kutulizwa na wenzake.

Brazil sasa watacheza nusu fainali na Ujerumani waliowafunga Ufaransa kwa tabu 1-0 katika robo fainali ya kwanza Ijumaa hii.
Brazil watamkosa nahodha na beki wao mahiri, Silva kwenye mechi hiyo, kwani alipewa kadi nyingine ya njano.

Atajilaumu mwenyewe kwa kadi hiyo kwa mchezo usio wa kiuungwana alipoingilia mpira wa kipa Ospina wa Colombia alipokuwa akiupiga baada ya kuudaka, ambapo kocha Luiz Felipe Scolari alionesha masikitiko makubwa.

Jumamosi hii Argentina wanachuana na Ubelgiji katika robo fainali ya tatu huku Uholanzi wakikabiliana na Costa Rica katika robo fainali ya mwisho.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Wastaafu wa Real Madrid kuzuru Tanzania

Neymar nje Kombe la Dunia