Menu
in , ,

Bolt abeba dhahabu Madola

*Kenya pia tishio

Nyota wa kimataifa katika mbio, Usain Bolt amelivisha taifa lake medali ya dhahabu baada ya kumaliza vyema mbio za kupokezana vijiti katika michuano ya Jumuiya ya Madola nchini Uskochi.

Bolt (27) ambaye awali ilidaiwa hangeingia kwenye mashindano hayo, alitua na kuwapa moyo wafuatiliaji, kabla ya kuonesha vitu adimu, akiwa mtu wa mwisho aliyepewa kijiti wakipeperusha bendera ya taifa lao dogo kijiografia.

Baada ya wenzake watatu kufanya vyema katika mbio za mita 400 kwa wanaume wanne, ikimaanisha kila mmoja anakimbia mita 100, kijana huyo ngongoti aliwashangaza wenzake kwa kumaliza mbio hizo ndani ya muda mfupi wa sekunde 37.58.

Waliomtangulia kijiti ni Jason Livermore, Kemar Bailey-Cole Nickel Ashmeade ambao wote walikimbia vyema kabla ya kukifikisha kijiti kwa mtu waliyeamini angewakamilishia salama na kwa ushindi kazi hiyo.

Bolt ameshashinda mara sita medali za dhahabu kwenye michuano ya Olimpiki, ni mshindi mara nane wa mbio za dunia lakini hii ni mara yake ya kwanza kushiriki kwenye Michezo ya Madola jijini Glasgow.

Bolt alikuwa koo kwa koo na mwanariadha wa Uingereza, Danny Talbot, lakini Mjamaica alimpotezea, akiwa anaonekana kukaza meno yake pamoja, akielekeza macho yake kwenye mstari wa ushindi, hivyo Mwingereza akaachwa nyuma.

Wanawake wa Jamaica nao walifanikiwa kuwaliza Wanigeria, kwani Kerron Stewart, Veronica Campbell-Brown, Schillonie Calvert na Shelly-Ann Fraser-Pryce nao walifanya kwenye kwenye mbio kama hizo, wakimwacha Mnigeria Blessing Okagbare akilia kwa kushindwa kuiongoza timu yake kwenye ushindi.
 
WAKENYA WAPO JUU
 
Wakenya Mercy Cherono na Janet Kisa walishinda medali za dhahabu na fedha katika michuano ya wanawake mbio za mita 5,000 kwa mfuatano huo, shaba ikienda kwa Mwingereza Jo Pavey.

“Lengo letu hapa ilikuwa kuja kutwaa medali hizo kwa ajili ya Kenya. Tunatumaini kwamba tutatwaa nyingine nyingi kama si zote kwenye mashindano ya ubingwa wa Afrika,” akasema Chirono.

Wanaume wengine wa Kenya, James Magut na Ronald Kwemoi nao walifanya kweli kwenye mbio za  wanaume kwa mita 1,500 kwa kutwaa dhahabu na fedha katika mtiririko huo. Raia wa Zealander, Nick alitwaa medali ya shaba.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version