in , ,

Blackburn Rovers, Newcastle United, Stoke City, Sunderland, West Brom na Wolves ,Kutangaza utalii wa Tanzania.Kwanini sio Chelsea, Arsenal Man Utd, Man City?

The Blackburn Rovers team which won the FA Cup...Image via Wikipedia

Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Taasisi za Bodi ya Utalii  Tanzania (TTB), TANAPA na Hifadhi ya Ngorongoro, zimeingia mkataba wenye thamani ya Sh. milioni 800 kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii kupitia udhamini wa mechi 114 za Ligi Kuu ya England, matangazo ambayo yameshaanza kurushwa.
Mkataba huo ni mpango maalumu kwa Tanzania kutumia michezo katika kutangaza vivutio vya utalii kote duniani ambapo kwa Afrika, Tanzania ni nchi ya kwanza kutumia aina hiyo ya uhamasishaji katika utalii. 
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Aloyce Nzuki, alisema wameingia mkataba na Kampuni ya Uwakala ya Lantech Services Ltd, ambapo viwanja vya timu sita za ligi hiyo vitahusika katika kurusha matangazo mbalimbali ya vivutio vya utalii vya Tanzania.
Alizitaja timu zitakazohusika kurusha matangazo hayo chini ya uwakala wa kampuni hiyo kuwa ni Blackburn Rovers, Newcastle United , Stoke City, Sunderland, West Brom na Wolves.
Alisema kampeni kuu tatu za uhamasishaji zitatumika kutangaza utalii katika matangazo husika na kuzitaja kuwa ni pamoja na kupanda Mlima Kilimanjaro, wanyama pori na fukwe.
Ni mkataba wa udhamini wa kuonyeshwa kwa matangazo yetu katika mechi za ligi kuu za timu hizo ambapo mechi 114 zitahusika na kampeni tatu kuu za uhamasishaji zitafanyika,” alisema Nzuki.
Alifafanua kuwa matangazo hayo yenye ujumbe unaolenga kampeni hizo tatu, yatakuwa yakionyeshwa kwenye kuta maalumu za matangazo za viwanja vya timu hizo katika mechi tofauti watakayocheza katika msimu huu wa ligi hiyo.
Aliongeza kuwa tayari matangazo hayo yameanza kuonekana katika mechi zilizochezwa na timu husika tangu kuanza kwa ligi hiyo na kutolea mfano wa
matangazo yalioonyeshwa katika mechi za Agosti 14 mwaka huu baina ya Blackburn v Everton, Sunderland v Birmingham na Wolves v Stoke City.
Akizungumzia maamuzi ya udhamini huo, Nzuki alisema ni mikakati ya kawaida ya kujiimarisha kiutendaji na kwamba hatua hiyo imelenga kuongeza mara dufu idadi
ya watalii na hatimaye pato la taifa. Alisema hatua hiyo haimaanishi kuwa walikuwa hawafanyi chochote katika
kujitangaza kimataifa huko nyuma, lakini tukio la kuingiza matangazo husika katika ligi hiyo bora inayoangaliwa na takriban watu bilioni 3 duniani ni cha kujivunia.
Tunajivunia hatua hii kubwa kwani pamoja na jitihada zetu za uhamasishaji za huko nyuma, hatua hii inaonyesha kuwa ya mafanikio zaidi kwetu na taifa kwa ujumla kutokana na idadi kubwa ya watu tutakaowafikia na kupata ujumbe kupitia ligi hiyo,” alisema.
Ligi Kuu ya England ni miongoni mwa ligi bora duniani ambapo takwimu za watafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa takribani watu bilioni 2.85 huangalia ligi hiyo duniani na kwamba mechi zinazohusisha timu kubwa za ligi hiyo huangaliwa na watu milioni 3.5 kwa wakati mmoja duniani.
Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Usain Bolt signs athletics’ “biggest ever” sponsorship deal

Posho za Twiga Stars hazimhusu Rais Kikwete’