BBC Idhaa ya Kiswahili, kama kawaida inaendelea kutoa burudani ya soka isiyo na kifani kwa mashabiki waliopo Afrika Mashariki na Kati kupitia kipindi chake maarufu, BBC Ulimwengu wa Soka. Kikosi kizima cha BBC Ulimwengu wa Soka – Alex Mureithi, Charles Hilary, Idd Seif, Hassan Mhelela, Peter Musembi and Salim Kikeke, kitakuletea maelezo na matokeo ya mechi zote za ligi kuu ya soka ya England msimu huu, inayoanza Jumamosi Agosti 16. Katika kuanza msimu, BBC Ulimwengu wa Soka itakutangazia moja kwa moja mchezo kati ya Hull itakayocheza na Fulham, kwenye uwanja wa KC. Matangazo ya mchezo huo yataanza saa kumi na nusu Afrika Mashariki.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Solomon Mugera anasema: ” Tulianza matangazo ya moja kwa moja ya ligi kuu ya England mwaka 2006. Wasikilizaji wetu wanatuambia kipindi cha BBC Ulimwengu wa Soka kimewanufaisha kupindukia, kuwaburudisha na kufuatilia vilivyo mechi za soka, na kwa lugha wanayoielewa vyema ya Kiswahili. Tutatangaza tena msimu huu wote, na nina hakika wasikilizaji wetu watafurahia sana”.
Jinsi ya kupata matangazo ya BBC Ulimwengu wa Soka:
Nchini Burundi, BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana mjini Bujumbura kupitia 90.2 FM, na katika 105.2 FM kwa maeneo mengine.
Nchini Kenya, BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana kupitia redio washirika – Radio Simba mjini Nairobi katika 102.7 FM, Sheki FM mjini Mombasa katika 106.6 FM na kupitia West FM mjini Bungoma katika 94.9 FM.
Nchini Rwanda, BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana mjini Kigali katika 93.9 FM, mjini Butare katika 106.1 FM, na mjini Kibuye katika 93.3 FM.
Nchini Tanzania, BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana mjini Zanzibar katika 94.1 FM na Pemba katika 93.5 FM. Vilevile unaweza kupata matangazo haya kupitia radio washirika: Radio Free Africa mjini Dar Es Salaam katika 98.6FM, Mwanza katika 89.8FM, Shinyanga katika 88.2FM, Kagera katika 94.1FM, Arusha katika 89.0FM, Mbeya katika 88.8FM, Dodoma katika 89.0FM, Rukwa katika 89.1FM, Ruvuma katika 89.6FM, Mtwara na Lindi katika 89.0FM, Singida katika 88.3FM, Iringa katika 93.5FM, Tanga katika 99.3FM, Tabora katika 90.0FM, Kigoma katika 90.0FM, Morogoro katika 93.8FM, Kilimanjaro katika 88.2FM, Mara katika 93.5FM na katika 1377 AM/MW kwenye maeneo yote Tanzania. Pia kupitia Radio One mjini Dar Es Salaam katika 89.5 FM, Arusha katika 95.3 FM, Dodoma katika 100.8 FM, Mwanza katika 102.5 FM, Moshi katika 1323 AM na katika 1440AM kwenye maeneo mengine yote. Radio 5 mjini Arusha katika 105.7 FM, na Sky FM katika 101.4 mjini Dar es Salaam.
BBC Ulimwengu wa Soka pia inapatikana kote Afrika Mashariki na Kati kwenye masafa Mafupi katika 11705 kHz, na vilevile kwenye tovuti: www.bbcswahili.com
BBC Idhaa ya Kiswahili pia itakuletea matangazo ya mechi zifuatazo:
Jumamosi, Agosti16, 2008
Hull v Fulham Jumamosi, Agosti 23, 2008
Liverpool v Middlesbrough
Jumamosi, Agosti 30, 2008
Everton v Portsmouth Jumamosi, Septemba 13, 2008
Blackburn v Arsenal
Jumamosi, Septemba 20, 2008
Liverpool v Stoke Jumamosi, Septemba 27, 2008
Man Utd v Bolton
Jumamosi, Oktoba 04, 2008
Chelsea v Aston Villa Jumamosi, Oktoba 18, 2008
Liverpool v Wigan
Jumamosi, Oktoba 25, 2008
Tottenham v Bolton Jumamosi, Novemba 01, 2008
Chelsea v Sunderland
Jumamosi, Novemba 08, 2008
Man City v Tottenham Jumamosi, Novemba 15, 2008
Arsenal v Aston Villa
Jumamosi, Novemba 22, 2008
Chelsea v Newcastle Jumamosi, Novemba 29, 2008
Tottenham v Everton
Jumamosi, Disemba 06, 2008
Bolton v Chelsea Jumamosi, Disemba 13, 2008
Tottenham v Man Utd
Jumamosi, Disemba 20, 2008
Arsenal v Liverpool
Ratiba hii inaweza kubadilishwa wakati wowote na mamlaka husika. BBC haihusiki na mabadiliko hayo.
Mwisho.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
Solomon Mugera, Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC
[email protected]
Christine George, Assistant International Publicist, BBC World Service
+44(0)207557 1142 ; [email protected]
Taarifa kwa Wahariri.
BBC Idhaa ya Kiswahili ni Shirika la Utangazaji ambalo hutoa huduma zake kupitia redio na kwenye mtandao kwa wasikilizaji wanaozungumza Kiswahili barani Afrika na ulimwengu mzima kwa ujumla. Kipindi cha BBC cha asubuhi Amka na BBC hurushwa hewani saa 12.00 asubuhi saa za Afrika mashariki, na hukuletea habari za eneo zima na duniani, pamoja na muziki na habari mbalimbali za kijamii. Kipindi maarufu cha BBC cha habari na uchambuzi Dira ya Dunia huanza saa 12 na nusu jioni. Leo Afrika husikika saa tatu kasorobo Afrika Mashariki, na hukuletea habari mbalimbali zilizotokea barani Afrika kwa siku hiyo. Mtandao wa BBC kwa kiswahili unapatikana katika bbcswahili.com. Katika mtandao huu, unaweza kupata taarifa za maandishi, matangazo yetu, makala na uchambuzi wa habari za Afrika na dunia nzima. Pia katika mtandao huu utapata taarifa na matangazo ya kipindi maarufu cha Kimasomaso, ambacho hutoa elimu ya afya ya uzazi na kuchambua mila na desturi zinazozingira suala zima la uzazi. Kipindi hicho kilianzishwa na kitengo cha kimataifa cha BBC cha misaada – BBC World Service Trust.
BBC World Service – Idhaa ya Dunia ni shirika la habari la kimataifa la utangazaji linalotoa huduma za matangazo kwa lugha 33 mbalimbali. Shirika hili linatumia njia kadhaa kuwafikia wasikilizaji wake milioni 183 ulimwenguni kote, kwa kupitia masafa mafupi, masafa ya kati, FM, satellite na viunganishi. Vituo washirika vya redio vipatavyo 2,000 hupitisha matangazo ya BBC, huku vituo kadhaa vukirusha taarifa zake kupitia simu za mkononi na vifaa mbalimbali visivyotumia nyaya. Wavuti wa BBC unatoa habari mbalimbali kwa maandishi, sauti na video, na vilevile kutoa nafasi kwa wasikilizaji kushiriki moja kwa moja katika vipindi kufuatana na matukio ya duniani. Takriban watu milioni 700 huvinjari katika wavuti huu kwa mwezi, na hivyo kuvutia karibu watumiaji milioni 40 kwa mwezi. Kwa taarifa zaidi tembelea www.bbcworldservice.com. Kufahamu zaidi kuhusu Idhaa ya Kiingereza ya BBC, au kujiandikisha kupata majarida yaliyopo kwenye mtandao tembelea www.bbcworldservice.com/schedules.
Tatizo lenu nyie Bbc ni kiswahili cha baadhi ya watangazaji wenu ni kibovu! wengine wanatangaza mpira kama wanasoma hadithi za zama za mfalme.
Kwasababu ya kutaka usawa halisi wa watangazaji toka kila nchi inayozugumza kiswahili, mwishoni mnaharibu kabisa.
Nakupongeza sana Mr. Israel Saria kwa kutumia uanamichezo wako kutuhabarisha Kitakachojiri hivi karibuni kuhusu kutangazwa Ligi yenye msisimko mkubwa Duniani.
Sasa hivi nipo Emarati, TV Stations nyingi zinatangaza kuanza kwa Ligi hiyo.
Hongera BBC pia Hongera Mr. Saria kwa kutumia Blog yako kutuhabarisha mambo hayo mazuri.
Mkurugenzi wa Kiluvya Pub.