BARCELONA, HISPANIA Katika mchezo huo ulioshuhudia kadi kumi za njano kutoka pande zote mbili, Barcelona ilitawala dakika zote za mchezo na kuwafanya Real Madrid kupoteana na kushindwa kabisa kufurukuta. Kwa matokeo hayo, Barcelona sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 34, huku Real Madrid ikishika nafasi ya pili kwa kuendelea kuwa na pointi 32. Barcelona ilipata bao la kwanza dakika ya tisa tu ya mchezo wakati Andres Iniesta alipompa pasi ya akili, Xavi aliyevunja mtego wa kuotea na kubaki na kipa Iker Casillas wa Real Madrid aliyekubali kuokota mpira kwenye nyavu zake. Barcelona iliongeza bao la pili dakika ya 17, lililofungwa na Pedro baada ya kuupata mpira kutoka kwa David Villa, ambaye alimhadaa Sergio Ramos kutoka wingi ya kushoto na kupiga shuti kali ambalo lilibabatizwa na kipa Casillas na kumkuta mfungaji aliyeukwamisha wavuni. Dakika ya 30, mchezo ulisimama kwa dakika kama mbili hivi baada ya Cristiano Ronaldo kumsukuma kocha wa Barcelona, Pep Guardiola na kuwafanya wachezaji wengi wa Barcelona kumvamia. Mpira ulikuwa umetoka nje, ndipo Guardiola alipoukamata, lakini Ronaldo alipoufuata kocha huyo akasita kumpa na ndipo Mreno huyo alipoamua kumsukuma kocha huyo. Dakika yak 57, Villa alifunga bao la nne baada ya kupokea tena pasi ya Messi ambaye alikuwa katika kiwango cha juu katika mchezo huo. Lakini Jeffren aliyeingia dakika za mwisho za mchezo akafunga bao la tano na kusababisha kilio Madrid. Jambo jingine la kuvutia katika mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki 98,000 ilikuwa ni kuona Barcelona ikitimiza miaka 111 tangu ianzishwe. Hata hivyo, mashabiki wengi wa Dar es Salaam waliokuwa wanajiandaa kuangalia pambano hilo kupitia runinga walijikuta wakitoka kapa baada ya umeme kukatwa katika maeneo mbalimbali. Real Madrid ilimkosa Gonzalo Higuain ambaye ni majeruhi na nafasi yake ilichukuliwa na Karim Benzema mwenye thamani ay pauni million 35. Kabla ya mchezo huo wa jana, Cristiano Ronaldo alikuwa anaongoza kwa ufungaji kwani alikuwa na mabao 14 akiafutiwa an Lionel Messi aliyekuwa na mabao 13. Real Madrid: Casillas, Sergio Ramos, Marcelo, Carvalho, Pepe, Khedira, Xabi Alonso, Ozil, Di Maria, Ronaldo, Benzema. |
Comments
Loading…