in , , , ,

Barcelona watenga £50m Arsenal kumtwaa Ramsey

TETESI NYINGINE ZA USAJILI

Barcelona wamevamia England na sasa wanataka kumchukua kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey, wakiwa tayari kumwaga kitita cha pauni zaidi ya milioni 50.

Ramsey (24) ni mchezaji muhimu kwa Arsenal, ambaye msimu uliopita kama si kuumia alishaanza kuwaelekeza kwenye hatua za karibu za kuufikia ubingwa, akifunga mabao 16.

Licha ya kupata tena majeraha msimu huu, amekuwa na mchango mkubwa kwa Arsenal hadi hatua waliyofika. Barcelona wanarudi London Kaskazini ambako waliwahi kumpata kiungo Cesc Fabregas.

Msimu uliopita Barca walibisha hodi tena, wakamchukua nahodha na mlinzi wa kati, Thomas Vermaelen, ambaye hata hivyo alikuwa kachuja. Arsenal walikwenda Camp Nou na kumpata Alexis Sanchez.

Kuna taarifa kwamba Barca wapo tayari kumwaga hadi pauni milioni 60 kumpata kiungo huyu na Arsenal wanaweza kufikiria mara mbili, ikizingatiwa pia akili yao kwenye kutunisha akiba yao ni kubwa.

Ramsey anacheza pia Timu ya Taifa ya Wales na amepata kupangwa kwenye wingi zote – kulia na kushoto. Akiwa mwanafunzi alicheza soka Cardiff kwa miaka minane akiweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi.

Alisonga nao hadi kwenye fainali ya Kombe la FA 2008, mwaka ambao alijiunga na Arsenal kwa dili la pauni milioni tano na kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza.

Alikwazwa na kuvunjika mguu kwenye mechi dhidi ya Stoke Februari 2010, lakini baada ya kupelekwa kwa mkono Nottingham Forest na Cardiff kati ya 2010 na 2011 alirejea na kuchukua nafasi yake kikosi cha kwanza.

TETESI NYINGINE ZA USAJILI
Depay

Baada ya kumpata winga Memphis Depay aliyekwishafuzu vipimo vya afya, Manchester United wanalenga kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger (30), ili kujiimarisha na kuwa na ushindani katika kutwaa ubingwa msimu ujao.

Liverpool wamefuta mkutano baina yao na mshambuliaji kinda Raheem Sterling, baada ya wakala wa mchezaji huyo, Aidy Ward kudai kwamba hatahuisha mkataba wake hata kama Liver wangemlipa mshahara wa pauni 900,000 kwa wiki.

Ilikuwa Ijumaa hii kocha Brendan Rodgers na Ofisa Mtendaji Mkuu, Ian Ayre wamkalishe chini Sterling kumshawishi juu ya mkataba mpya baada ya kukataa wa mwanzo ambapo angelipwa pauni 90,000 kwa wiki.

Kauli ya Ward imewachefua Liverpool na wamesema jambo zuri analoweza kufanya Sterling ni kuachana na wakala huyo.

Inter Milan wanaofundishwa na Roberto Mancini wanaamini kwamba wamefikia pazuri katika kumnasa kiungo wa Manchester City, Yaya Toure (32), licha ya City kudai kwamba hawajapokea ofa yoyote.

Mabingwa wa Italia waliofika fanali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), Juventus wanafikiria kutoa pauni milioni 25 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Erik Lamela (23) wakilenga kujiimarisha kuwa kikosi hatari zaidi Ulaya msimu ujao.

Liverpool wanapokea ofa kwa ajili ya kiungo wao, Lucas Leiva (28) wanayetaka kumuuza na amekuwa akihusishwa na klabu ya Inter Milan.

Kiungo wa kimataifa wa England anayekipiga Man City, James Milner (29) anajiandaa kuondoka klabuni hapo akiwa mchezaji huru, na anavutia klabu za Arsenal na Liverpool.

Beki wa Brazil, Dani Alves (32) ameshindwa kuelewana na Barcelona juu ya mkataba mpya, hivyo naye anaondoka mwishoni mwa msimu akiwa mchezaji huru.

Kocha wa West Ham United, Sam Allardyce anayetarajiwa kuondoka kiangazi hiki amesema atakakokwenda kutajulikana akiwa nje ya klabu hiyo.

Habari hizo zinakuja huku mlinzi wa zamani wa klabu hiyo, Slaven Bilic akielezwa kwamba ataacha kazi ya ukocha Besiktas mwisho wa msimu, akidhaniwa kwamba tachukua nafasi ya Allardyce.

Sunderland wamempa kocha wao wa muda aliyewaokoa dhidi ya kushuka daraja, Dick Advocaat ofa ya kuwa kocha wa kudumu, lakini mwenyewe bado hajaamua.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Sunderland waokoka kushuka

Kikosi cha England chatajwa