Menu
in

Azam Bingwa Chini Ya Yanga Na Simba

Tanzania Sports

Lengo la timu ya Azam msimu huu kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, hili walilisema kabla ligi haijaanza na sasa inaonekana kweli wana kitu wanakihitaji.

Tuanze na rekodi ambazo zinaonesha jinsi gani msimu huu timu hiyo inaweza ikanyanyua kwapa katikati ya Yanga na Simba.

Katika rekodi hizi tunaangalia baada ya kutimiza mechi saba imevuna alama ngapi, imepata magoli mangapi, ‘Clean Sheets’, mechi ilizoshinda na vipigo.

Yanga 2015-2016

Msimu huo timu ya Wananchi ilikuwa katika kilele chake cha mafanikio, na ulikuwa msimu ambao walichukua ubingwa wa pili mfululizo.

Katika michezo saba timu hiyo ilifunga magoli 18, ilifungwa magoli 3, ‘Clean Sheets’ 4, ilishinda mechi sita haikufungwa mchezo wowote na ikatoka sare moja, ilikusanya alama 18, ikafungwa magoli 3.

Simba 2019-2020

Katika michezo 7, ilishinda sita ikapigwa mmoja, ilifunga magoli 12, ‘Clean Sheets’ 4, ikafungwa magoli 3, ilijikusanyia alama 18.

Azam FC 2020-21

Hadi sasa imecheza michezo 7, imefungwa magoli 2, imefunga magoli 14, ‘Clean Sheets’ 6, imeshinda michezo yote saba, haijafungwa hata mchezo mmoja wala kutoa sare.

Ubingwa hauji kwa kuangalia namna wanavyoshinda mechi zao bali unaangalia timu nzima inafanya nini.

Katika misimu yote hiyo ambayo nimekutajia hapo juu Yanga na Simba walifikisha alama hizo kwa michezo saba walichukua ubingwa.

KWANINI AZAM FC BINGWA?

Zinaweza zikwa sababu nyingi za kuona maendeleo ya timu hiyo ila nakupa mchache kisha utaamua kukubai au kutokukubali.

USAJILI
Timu ya Azam FC msimu huu imefanya machaguo mazuri sana kwa wachezaji wake.

Hawakuwa na papara kama walivyokuwa zamani wanasubiri Simba au Yanga wawateme wao wawachukue.

Mfano nyota kadhaa wa Yanga waliowahi kucheza hapo ni pamoja na Frank Domayo, Didie Kavumbagu na Abdi Kassim.

Wakati Simba aliwahi kucheza Ramadhani Singano baadae akatimkia Azam.

Hii yote ilikuwa kukosa mitazamo chanya ya kutafuta wachezaji walio bora.

Ila baada ya kuona udhaifu huo wameona isiwe taabu wakachukua wachezaji wazuri kwa ajiri ya kutumika kwa mwaka huu.

Angalia uwepo wa wachezaji hawa wafuatao katik timu hiyo iliyopo nje kidogo za jiji la Dar es Salaam.

Prince Dube

Hadi sasa nyota huyo amecheza michezo 7 ya mashindano, amefunga magoli 6 amechangia kusaidia magoli 2, huku akifunga magoli 2 katika mechi za kirafiki.

Nyota yake kwa sasa inang’aa sana na uwezo anao huu ni usajili wa mfano sana.

Kiwango chake kila mmoja anakifahamu kwani anatesa sana na huenda  Medie Kagere amepata mtu wa kumpa usumbufu katika kinyang’anyiro  ufungaji bora.

Obrey Chirwa

Huu usajili wa muda mrefu ila sasa kama amezaliwa upya ameshafunga magoli 3 ligi kuu Tanzania bara.

Djodi

Alisajiliwa msimu uliopita hajaonesha uwezo wake mkubwa ila bado anaweza kufanya lolote na muda wowote.

Sehemu ya viungo bado kuna watu wakali walio na uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu.

Ally Niyonzima

Kiungo hodari kabisa amefunga goli moja na uwezo wake inatakiwa uwe unaujua mpira anasaga sana pale kati.

Kuna mtu anawasiwasi na Niyonzima, basi tusubiri na tuone watakapochukua ubingwa kisha tuongee mengine.

Never Tigere

Huyu mtu anachukua sehemu kubwa ya ushambuliaji kiungo ya pembeni, mimi binafsi namkubali ila uwezo wake ndio umenifanya niwe na hisia za kuipa ubingwa Azam.

Iddi Nado

Unataka useme nini hadi wakuelewe watu wa Azam katika kikosi cha kwanza cha Wanarambaramba hao.

Juzi aliweka goli moja akipokea pasi safi kutoka kwa Dube, hivyo ni mchezaji mzuri sana.

Safu ya mabeki sasa pamesimama vizuri sana, wameruhusu magoli 2 pekee.

Aggrey Morris, Abdalla Heri, Yakubu Mohamedi, Bruce Kangwa pamoja na Nicolas Wadada.

Kipa akisimama David Kisu ambaye hadi sasa ana ‘Clean Sheets’ 6 jamani hebu tufungueni midomo tuipe nafasi Azam.

Huo ni mtazamo tu kila mmoja ashinde mechi zake ili tuje kuhesabu aliyepata alama nyingi.

Yanga, Simba na Azam moja ya timu ninazozipa nafasi kubwa kuchukua ubingwa kutokana na wachezaji walio nao pamoja na uwezo wa kifedha.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version