in , , ,

Arsenal shamba la bibi

*Man City kumchukua Bacary Sagna

Arsenal wanaendelea kuwa na wakati mgumu katika kila nyanja, safari hii ikiwa ni mwelekeo wa kuondokewa na wachezaji, na mmoja wao ni beki mahiri Bacary Sagna anayekaribia kwenda Manchester City.

Sagna aliyejiunga na Arsenal 2007 anamaliza mkataba wake msimu huu wa kiangazi na si ajabu akaondoka kama mchezaji huru pasipo Arsenal kupata hata ndururu, jambo litakalowaongezea majonzi Washika Bunduki na washabiki wao.

Mazungumzo ya mkataba mpya baina yake na Arsenal yalidorora kwa sababu klabu walitaka kumpa mkataba mfupi kwa mafao yale yale, lakini yeye alitaka walau miaka mitatu, na baada ya kuona klabu nyingine zinamhitaji, akapandisha dau pia.

Sagna amekataa mazungumzo ya kujiunga na Inter Milan, hivyo Man City wakateka fursa hiyo mara moja ili kumchukua kutoka Arsenal, wakiongeza mnyororo wa wachezaji wengine waliotoka Emirates na kuingia Etihad ambao ni Emmanuel Adebayor, Samir Nasri, Kolo Touré na Gael Clichy.

Hizi si habari njema kwa Arsenal ambao wameanza kudorora dimbani siku za karibuni kwa kupoteza mechi za Ligi Kuu ya England (EPL), kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) lakini mbaya zaidi kukubali kisago cha mabao 6-0 wikiendi iliyopita mikononi mwa Chelsea.

Manchester City ambao wakishinda mechi zilizobaki watakuwa mabingwa wapya wa England, tayari wamempa Sagna (31) mkataba wa miaka mitatu wenye mafao mazuri na sasa anatakiwa autafakari kama ataona aondoke Arsenal au abaki.

Sagna alipata kuhoji sera za Arsenal na pia jinsi ilivyoachia nyota wake wengi, wakiwamo Robin van Persie, Cesc Fabregas na wengineo kuondoka, na sasa Arsene Wenger anasema yupo tayari kuvunja sera za jumla za klabu hiyo za kuongeza mkataba wa mwaka mmoja tu kwa mchezaji aliyezidi miaka 30, maana Sagna bado ni nguzo imara kwa timu.

Kwa sasa anapata mshahara wa pauni 50,000 kwa wiki ambapo akienda City atapata zaidi ya hapo kwa mbali. Wachezaji wengine walioajiriwa au kupata kuajiriwa na Man City kutoka Arsenal ni pamoja na Patrick Vieira, Brian Kidd, Brian Marwood, David Platt na Stuart Taylor na pia Yaya Touré alikuwa Arsenal kwenye mechi ya kirafiki kabla ya msimu wa 2003 akijaribiwa klabuni hapo.

Klabu nyingine zinazomtaka Sagna aliyedhihirisha ubora wake kwenye mechi nyingi ni pamoja na Liverpool na Tottenham Hotspur, Paris St-Germain Monaco za Ufaransa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Spurs watafuta kocha mpya

Kizungumkuti Ligi Kuu England