in , ,

Arsenal na Wenger tu

Wasiompenda Arsene Wenger au waliochoka na mbinu na uwapo wake Arsenal
inaelekea wataula wa chuya, baada ya mmiliki mwenza aliyetarajiwa
angeweza kushinikiza aondoke kummwagia sifa, akisema ndiyo ‘mali
muhimu’ zaidi kwa klabu.

Mwanahisa huyo wa pili kwa umiliki wa hisa nyingi, bilionea Alisher
Usmanov aliyepata kumchagiza Wenger kwa kutonunua wachezaji wakubwa,
amesema Arsenal wanamhitaji Wenger na bosi huyo ataamua mwenyewe akae
kwa muda gani hapo.

Kumetokea shinikizo kwamba Wenger amechoka, hana mbinu mpya,
anawakosesha Arsenal ubingwa na hivyo aondoke, huku hata Jose Mourinho
aliyefutwa kazi Chelsea akipewa nafasi ya kuingia Emirates.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo walishaona kwamba ingekuwa ngumu,
ikizingatiwa mmiliki namba moja wa Arsenal, Mmarekani Stan Kroenke
anampenda Wenger na haambiwi lolote na yeyote juu ya kutofaa kwa bosi
huyo.

Usmanov, raia wa Urusi anasema kwamba klabu lazima wabakie na nembo
yao kuu – Arsene Wenger, lakini akakiri kwamba wamekuwa na matatizo
kwa miaka mingi na si rahisi mwaka huu kutwaa ubingwa wa England
waliokuwa wameusogelea kabla ya kuanza kufungwa na kwenda sare.

Arsène Wenger
Arsène Wenger

Arsenal wametolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) katika hatua ya
16 bora, msimu huu ukiwa ni wa sita mfululizo wanashindwa kutinga robo
fainali, lakini hata Kombe la FA walilotwaa mara mbili mfululizo
wameshindwa kulitetea baada ya kutupwa nje na Watford katika hatua ya
robo fainali.

Walishalikosa Kombe la Ligi na wanashika nafasi ya tatu katika Ligi
Kuu ya England (EPL), wakiwa na pointi 11 nyuma ya Leicester
wanaoongoza na hawajapata kutwaa ubingwa tangu 2004.

Wenger amekuwa klabuni hapo tangu 1996 na ndiye kocha anayeongoza sasa
kwa kukaa kwenye klabu moja kwa muda mrefu jinsi hiyo. Usmanov
ameongeza hisa zake Arsenal na sasa ana asilimia 30.

Alipata kulalamika kwamba ni ajabu kwa mmiliki mwenza kama yeye
kutoingizwa kwenye bodi ya klabu wala katika kufanya uamuzi mkubwa,
akiachiwa Kroenke na warasimu wengine sampuli ya Wenger klabuni hapo.

Usmanov anasema lazima Wenger abakie klabuni kwa sababu ni kocha
mkubwa na maarufu na pia baadaye atapewa fursa ya kuandaa mrithi wake
ili kuendeleza mazuri yaliyopo na anatambuliwa kuwa alama kubwa
klabuni hapo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

KANTE ANASTAHILI NAFASI YA UHAKIKA KWENYE KIKOSI CHA UFARANSA

Tanzania Sports

Taifa Stars, kushuka dimbani kesho..